Maoni yangu juu mabadiliko ya katiba kwenye ukomo wa Urais

Maoni yangu juu mabadiliko ya katiba kwenye ukomo wa Urais

Habari wanajamii

Kwa mujibu wa katiba yetu inayotumika hadi sasa ukomo wa kugombea nafasi ya urais ni miaka 10 kwa kila kiongozi ikiwa ni awamu mbili yaani uchaguzi wa raisi kila baada ya miaka mitano.
Asili hii ya ukomo wa raisi imeasisiwa toka taifa la Marekani

"....Utaratibu wa kuweka ukomo wa viongozi kubaki madarakani una asili yake nchini Marekani. Nchi hiyo ambayo ndiyo kinara wa mfumo wa dunia baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ilifanya hivyo mwaka 1951......Walioweka vifungu hivyo kwenye Katiba ya Marekani walijiridhisha kwamba jambo ambalo kiongozi atashindwa kulifanya ndani ya miaka minane madarakani, hawezi kulifanya hata akiongozewa muda kiasi gani.....Inajulikana kwamba pamoja na kuweka mifumo hiyo, zimekuwapo sauti za kutaka kubadili utaratibu huu wa ukomo ndani ya Marekani na China pia. Mwaka 1987, kulikuwapo na kikundi cha Wamarekani waliotaka Katiba ibadilishwe ili aliyekuwa Rais wakati huo, Ronald Reagan, aendelee kubaki madarakani......BBC SWAHILI"

Maoni yangu yanaungana na wale wanaotaka kuondoa ukomo huo na kuweka utaratibu huu
1.KUWEPO NA KURA YA MAONI KILA BAADA YA MIAKA 5 YAKUAMUA AENDELEE AU ASIENDELEE

2.UKOMO WA KIONGOZI HUSIKA NI PALE TU KURA ZA MAONI ZA ASIENDELEE ZITAKAPOKUWA NYINGI KULIKO KURA ZA AENDELEE (WENGI WAPE) AMA KIFO.

3.TUME YAKUSIMAMIA KURA IWE TUME HURU ISIYO NA MUINGILIANO NA IKILU (SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI)

Faida za kuondoa Ukomo
1.Kutekeleza miradi aliyoianzisha....Tunafahamu kwamba miradi mingi ya serikali ni miradi ya muda mrefu miaka 5-10-20 nk hivyo inahitaji ufuatiliaji na usimamiaji.Kitendo cha kuingia uongozi mwingine mambo huenda kombo ama kuzorota.Hii nipale kiongozi husika anapoliona jambo alilolianzisha mwenzake halitakuwa na manufaa nae kisiasa bali sifa huenda kwa mwasisi wake.Ama kugundua kwamba mradi huo haukuwa rafiki kwa maslahi ya nchi (hauungi mkono) hasa ikiwa mradi huo ameugundua umepitishwa kwa mikataba ya hovyo.Kila kiongozi akija na jambo lake nchi itakuwa na mipango mingi isiyotekelezeka au kubaki nusunusu.

2.Kuna viongozi hawakustahili kutoka madarakani.Kila raia anafahamu ni kiongozi gani alifaa aendelee na madaraka ila katiba ndio ilimuondoa.Kuna viongozi tunaimani nao hivyo kuendelea kushika usukani tunaamini tungefikishwa mahala pazuri.Huenda kwa maoni yako kiongozi wa namna hiyo hajatokea nchini sasa vipi akitokea je nisawa katiba ituondolee mpendwa wetu.

3.Uzoefu Na Ufahamu.Kiongozi aliyeanzisha jambo niwazi atakuwa na ufahamu nalo kwa kipindi chote awapo madarakani na atajua lipi aliwahishe na lipi alichelewe.Yani wewe kama kiongozi tayari unaramani yako njema ya mwenendo wa nchi wakati upo katika utekelezaji unaambiwa muda wako umeisha huwezi kuendelea nalo kwa mujibu wa katiba...Anakuja kiongozi mpya na ramani yake na uzoefu mpya lazima mambo yawe sivyo nawe mstaafu utayashuhudia yaendavyo.Embu fikiria mradi mmoja usimamiwe na watu watatu tofauti kila mmoja ako na maono yake au kupinga kabisa.

4.Uwajibikaji. Ukishajijua kwamba jambo ulilolianzisha ndio utaishi nalo kipindi chote ama mkataba ulioingia utaishi nao kipindi chote basi haotokubali kuharibu nafasi yako.Nasema hivi nikihisi kwamba huenda kuna viongozi wanaingia mikataba ya hovyo ambayo athari zake zinakuja kuonekana awamu nne mbele.Mfano mzuri ni kama tunavyosema kutunza rasilimali kwaajili ya kizazi kijacho,hii inafahamika kwamba tunaouwezo wa kuvuna misitu na sisi wazama hizi tukanufaika nakusaza lakini baada ya miongo kadhaa watoto wetu wakaishi katika jangwa lililotokana na sisi.Hivyohivyo kiongozi anafaa afanya jambo akiwa pia na hofu ya kuwajibika kwako sio jipu likamtumbukie aliyemfuata.

5. Miaka 10 ni michache.Ukizungumzia nchi bila shaka ni jambo kubwa sana ambalo hata mipango yake huwa niya milenia na karne ama mingo kadhaa.Sasa vipi uwambiwe unapewa miaka 10 tena ni 5 kama hukupita uchaguzi na unaambiwa ndani ya iyo miaka 5 ufanye nchi mapinduzi ya viwanda toka kwenye kilimo.Unapata picha gani zaidi tu ya kuanzisha mambo ambayo hadi unastaafu hayajatimia.Embu fikiria umeingia madarakani unakutana na agenda za miaka 60 nyuma zipatazo 100 nawe unaingia ukiwa na ajenda zako 50 ambazo pia kwa muda uliopo utakazozikamilisha kwa 100% huenda ni 5 tu.

Zingatio; Maoni hapo juu yamezingatia ajenda za kiongozi ila tunafahamu na kusikia kwamba kila kiongozi huenda kutekeleza agenda za chama chake kwamba haji na agenda zake bali zilezile alipoishia mwezake katika utekelezaji.Kama hivyo ndivyo basi ni nafuu kidogo ijapo tunafahamu kila kiongozi ako na maono ya utofauti juu ya utekelezaji huo.Na ikiwa chama ndio kinahusika na usimamiaji wa agenda izo basi kuna haja ya raia kuchagua chama kingine kitakachokuwa agenda chanya na kupendekeza mgombea mwenye maono chanya zaidi ila suala la muda wa uongozi litabaki palepale kuwaongezea muda kuweza kutekeleza majukumu yako.

Hitimisho. Haya ni maoni binafsi yasiyo na mashiko na chama chochote wala utawala wowote zaidi nimesisitiza kuongezewa muda viongozi wa kutekeleza majukumu yao (kutawala) ili kiongozi aonje tamu ya alichokianzisha na chungu ya baya alilolianzisha.Naamini hadi sasa Mheshimiwa Mwinyi angejua RUKSA inaendeleaje wapi aboreshe wapi aondoe kusudu ile RUKSA iliyo kichwani mwake ikae vyema kama alivyoitaraji.Nae hayati Mkapa angejua wapi UBINAFSISHAJI upofikia na vipi ausimamie hadi alipofikwa na umauti.Nae Mheshimiwa Kikwete angefahamu hadi sasa sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA hadi sasa angefikia wapi vipi aboreshe vipi abadili.Nae Hayati Magufuli angefahamu vipi TANZANIA YA VIWANDA YAKUJITEGEMEA wapi imefikia kwenye ramani yake na angefanya nini kuhakikisha kile alichokiamini kinakuwa kwa kadiri umri ungeongezeka.Naamini sera za viongozi hawa zimekwamishwa na ukomo kikatiba na kama watakiri kwamba zimetekelezeka kama walivyozipanga ndani ya muda wao wa miaka 10 basi hatuna haja ya kuulizana mana kila mtu ako na macho anaona nchi ilipofikia hivyo huenda zipo yes na no.Tunaomba raia ndio waamue uko wa uraisi sio katiba.
Mkuu kwa andiko lako nafikir hata mfumo wa Democracy pia hautufai bora turudi kwenye mifumo ya U-monarchy watu tutawalane kifalme......

Mkuu hivi kweli upo serious kabisa na hili andiko lako au maana unaona miaka 10 michache bhasi tutawale kiukoo tu ili turudi kabisa utumwani
 
hapana ni kura kuendelea na uongozi au kuitishwa uchaguzi mwingine bada ya miaka mitano...nilichoshauri kuondolewa ni ukomo wa miaka 10 na kuwepo kwa kura ya maoni kila miaka 5 ya kuendelea ama asiendelee kuongoza
Ndo nikakuuliza, nyie mkamuongezea huo muda halafu Mungu akamchukua itakuwaje? Sijui hata kama unaelewa
 
basi ndio maana nikapendekeza kura ya maoni ya aendelee ama laa
Watawala wa kiafrika hawaitaji kura kendelea kutawala watafanya lolote kuendelea kubaki pale uchaguzi ni kiini macho, Bongo alie pinduliwa juzi kati tuu hapo baadhi ya wananchi walinukuliwa na BBC Swahili walisema hata kama ange gombea na mbwa wange mpigia kura mbwa lakini kwenye uchaguzi akashinda
 
Mkuu kwa andiko lako nafikir hata mfumo wa Democracy pia hautufai bora turudi kwenye mifumo ya U-monarchy watu tutawalane kifalme......

Mkuu hivi kweli upo serious kabisa na hili andiko lako au maana unaona miaka 10 michache bhasi tutawale kiukoo tu ili turudi kabisa utumwani
kuna kura ya maoni mkuu kila baada ya miaka mitano kuamua aendelee ama asiendelee
 
Watawala wa kiafrika hawaitaji kura kendelea kutawala watafanya lolote kuendelea kubaki pale uchaguzi ni kiini macho, Bongo alie pinduliwa juzi kati tuu hapo baadhi ya wananchi walinukuliwa na BBC Swahili walisema hata kama ange gombea na mbwa wange mpigia kura mbwa lakini kwenye uchaguzi akashinda
so changamoto iliyopo hapa ni mfumo wa kura sio rafiki ili kuunga hoja hii...kwamba ikiwa utakuwepo usimamizi wa kura wa haki basi wazo hili ni jema kwa namna ingine
 
kuna kura ya maoni mkuu kila baada ya miaka mitano kuamua aendelee ama asiendelee
àMkuu una miaka mingapi, Maana unataka kuturudisha nyuma unachokisema kilikuwepo Tangu tupate uhuru mpaka miaka ya 1992 pale ambapo Palipoanzishwa vyama vingi...
Maana uliyohadithia hiyo sio Ajenda mpya ililuwepo kipindi cha monoparty system na ndo maana unaona mpaka nyerere mwenyew aliomba poo maana aliongoza kwa muda mrefu sana
 
Shukrani mkuu ila kama wataweka ukomo basi walau hata 20 walau mtu anaweza kufanya mambo yakaeleweka
 
so changamoto iliyopo hapa ni mfumo wa kura sio rafiki ili kuunga hoja hii...kwamba ikiwa utakuwepo usimamizi wa kura wa haki basi wazo hili ni jema kwa namna ingine
Hapana labda tuu tungekua na mfumo wa kua na vipaumbele vya taifa ambavyo yeyote atakae ingia madarakani lazima avifanye kama ni viwanda au ni teknolojia au Kama ni kilimo basi yeyote atakae kuja lazima andeleze
kwa mfano Marekani haijalishi mgombea atakae shinda ni chama tawala au ni upinzani lakini kuna vitu lazima aendeleze kama kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya silaha na vitu vingine vingi,
lakini huku ni kanyaga twende na kwa tabia yetu waafrika ukiruhusiwa mfumo kama huo itakua ni fimbo ya kuwachapa wanyonge, kama sasa hivi mtu anapata jeuri ya kusema "nilisema na ninasema tena kama unaonewa hamia Burundi" vipi huyu ukimpa mfumo kama huo kitatokea nini hapo 🤔🤔
 
shukrani mkuu basi hapa naona tupambane kwanza kupata uchaguzi huru nawa haki huenda mambo mengi yakawezekana
 
Back
Top Bottom