Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412

Ni model ya gari ya Toyota Harrier kizazi cha vvt-i (umeme mwingi mafuta kidogo).

Huku kwetu tunaita new model lakini kimsingi sio new model kwa huko Japan.

Kwa kawaida Harrier ni gari zinazosifika kwa ulaji mbaya wa mafuta lakini model hii TAKO LA NYANI ni tofauti na model nyingine

Uundwaji wake umezingatia starehe zaidi, kasi, nguvu na ulaji mdogo wa mafuta. Hivi vigezo vimewavutia wa bongo wengi mpaka kuifanya ndio gari ya kuuzia sura kwa sasa yani ndio gari inayouza.

Huwezi kukaa dakika kumi mahali yanapopita magari bila kuiona hii gari mpaka sasa inaelekea kuwa kama sare ya taifa

Neno TAKO LA NYANI limetokana na hii gari taa zake za nyuma zilivyo.Yani zimekaa kama makalio ya nyani gendaeka yule mwenye makalio mekundu.


Lakini ni wangapi wanajua hatari za hii gari gumzo la jiji? Kwa taarifa yako ndio gari zinazoongoza kwa ajali zikifuatiwa na Alphard.

Unaweza kudhani zina tatizo lakini shida ni sisi wenyewe. Hatujazoea gari zenye take over kubwa na mwendokasi wa fasta.

Hivyo ndugu zangu kama kuna mwenye mpango wa kununua hii gari azingatie haya wepesi, mwendokasi na nguvu ya hii gari

Jr[emoji769]
 
Mkuu, nimenunua hii kitu kwa mtu miezi sita iliyopita ikanishinda nikauza niliyemuuzia kapiga mzinga maeneo ya senkenke kwa mbele mwezi uliopita, nilipata mshituko sana nikahisi kama ilikuwa inanitafuta.
.....
Ila jamaa mzima
 
Tumekusikia kiongozi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilichoelewa tu ni tako la nyani a.k.a tako jekundu...halafu linakuwaga limenona[emoji23][emoji8][emoji39][emoji39][emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…