Maoni yangu: Tundu Lissu agombee uenyekiti wa CHADEMA taifa

Maoni yangu: Tundu Lissu agombee uenyekiti wa CHADEMA taifa

Hivi Mbowe alisema kwamba hatagombea UENYEKITI WA CDM au Alisema kwamba HATAGOMBEA NAFASI YA KUPEPERUSHA BENDERA YA CDM kwenye nafasi ya URAIS wa JMT?
 
Kwakweli nimekaa na kutafakari kwa kina juu ya nani hasa anayeweza kufaa kuchukua nafasi ya Mbowe ya uenyekiti wa CHADEMA taifa na kujiridhisha kuwa ndugu Tundu Lissu anaweza sana kuitwaa nafasi hiyo na kukiongoza chama kwa mafanikio zaidi kuelekea 2015.

kimsingi Vigezo muhimu nilichotumia ni

1.umahiri wa ndugu Lissu awapo bungeni na hata nje ya bunge katika kujenga hoja na kuisimamia.

2. Pia Lissu sijasikia akitajwa kwenye yanayodaiwa kuwa makundi ya wanaodaiwa kuusaka urais ndani ya cdm na hata nje ya cdm.

3.ana msismamo usioyumba wala kutikiswa na nguvu ya fedha wala umaarufu wa bandia.

4.hatoki pia kanda ya kaskazini hivyo atawazima wale wachache wanaobeba hoja mufilisi ya ukanda ndani ya cdm

5.atasaidia kuiinua CHADEMA katika kanda ya kati yaani mikoa ya singida,dodoma na manyara kwa kuleta hamasa

6.sio mtu mwenye ndimi mbili katika jambo moja.

Hizi ni baadhi tuu ya sifa chache nilizoziona kwa ndugu huyu mabazo kwakweli pamoja na nyingine nyingi nimeshawishika na kuamini kuwa anaweza kuiongoza CHADEMA kwa mafanikio makubwa.

Naomba maoni yenu

Ni sawa mkuu ila huyu jamaa anafiti sana kuchukua mikoba ya Dr. Slaa,kuwa mtendaji mkuu wa chama
 
Swala siyo nani anaweza kuwa mwenyekiti mzuri. Swala ni je Mtei atamkubali?
Mzee wa watu kaanzisha chama kwa gahrama kubwa sana, msimuingilie kwenye maamuzi yake.
 
Swala siyo nani anaweza kuwa mwenyekiti mzuri. Swala ni je Mtei atamkubali?
Mzee wa watu kaanzisha chama kwa gahrama kubwa sana, msimuingilie kwenye maamuzi yake.

Lema atafit uenyekiti. Ana kila sifa - hekima na kipaji cha uongozi. Ni mtu makini asiyekurupuka. Lema ni zaidi ya Mbowe.
 
Kuna vitu muhimu vya kuangalia katika kuchagua au kuteua. Kuna vichwa vinafaa nafasi fulani fulani kwa hiyo CDM wawe makini. Tunahitaji watu wenye upeo wa mambo na kujitoa kwa kujituma au kujitolea kuokoa taifa hili. Mkiti mstaafu yeye atupe busara zake sio kututeulia mtu! Viva CDM.
 
Kwakweli nimekaa na kutafakari kwa kina juu ya nani hasa anayeweza kufaa kuchukua nafasi ya Mbowe ya uenyekiti wa CHADEMA taifa na kujiridhisha kuwa ndugu Tundu Lissu anaweza sana kuitwaa nafasi hiyo na kukiongoza chama kwa mafanikio zaidi kuelekea 2015.

kimsingi Vigezo muhimu nilichotumia ni

1.umahiri wa ndugu Lissu awapo bungeni na hata nje ya bunge katika kujenga hoja na kuisimamia.

2. Pia Lissu sijasikia akitajwa kwenye yanayodaiwa kuwa makundi ya wanaodaiwa kuusaka urais ndani ya cdm na hata nje ya cdm.

3.ana msismamo usioyumba wala kutikiswa na nguvu ya fedha wala umaarufu wa bandia.

4.hatoki pia kanda ya kaskazini hivyo atawazima wale wachache wanaobeba hoja mufilisi ya ukanda ndani ya cdm

5.atasaidia kuiinua CHADEMA katika kanda ya kati yaani mikoa ya singida,dodoma na manyara kwa kuleta hamasa

6.sio mtu mwenye ndimi mbili katika jambo moja.

Hizi ni baadhi tuu ya sifa chache nilizoziona kwa ndugu huyu mabazo kwakweli pamoja na nyingine nyingi nimeshawishika na kuamini kuwa anaweza kuiongoza CHADEMA kwa mafanikio makubwa.

Naomba maoni yenu

Wewe Gamba,

- Mambo ya ukanda ni ya kwenu huko,
- Mambo ya ndimi mbili ni ya kwenu huko
- Singida, dodoma na manyara sio jukumu lake pekee ni la Chadema kwa ujumla: lakini hiyo mikoa sio kweli kuwa ni ya CCM kwa sasa bali ni propaganda zetu tu. Kilichotokea Ndago ni ushahdi kuwa CCM haipendwi kabisa Singida. Manyara sehemu kubwa ni CDM
 
Yap hata mimi kura yangu anayo anaweza, Vilevile ningependa Pro.Safari awemo kwenye list ya viongozi
 
sawa mawazo yako ni mazuri ni vizuri ukamshauri. Lakini kwa qualities zote hizo ni lazima mtu awe mwenyekiti?
sio lazima lakini kama nimejiridhisha na sifa zake kwanini nisimpendekeze?hata wewe una haki ya kumpendekeza unayefikiri anafaa na uweke sifa zake
 
Nilijua tu mada hii ni kutaka tu kumchafua ZITTO, siasa feki hizo, usipende sana kuongelea watu, ongelea mambo ya msingi.

wewe masalia nini?
Unabisha kuwa zzk sio mshirikna; hukumbuki kauli yake mwenyewe humu ya "HATA PANYA HAYATASALIMIKA"

Usipende kujitoa ufahamu; mtu/kiongozi mkubwa kama yeye unamsapoti kwa ushirikina huo
 
Ahsante sana kwa mapendekezo mkuu, ni vema ungeainisha na udhaifuwa huyu wa sasa na kwa nini asiendelee kuwa mwenyekiti!??

Wee Baba V hujitaki? Viongozi wote wa CDM ni Miungu watu hawna kasoro ni wakamilifu hao waguse uone maneno ati masalia, PM7......
 
Afadhali maana hapa Ikungi Lissu hana chake..na mwenyewe anahua sana. Hakuna mipango yeyote ya kurudi anachojua ni kufukia visima huku yy akinywa maji ya chupa sie twahaha.......

Na anakimbilia Singida mjini na huo ndio utakuwa mwisho maana hamuwezi MO hata kwa theluthi.....Jamani mpeni uenyekiti tuzidi kumsikia huku jimboni hana chake
 
Baada ya Mbowe kufika at the point of no return, ni wakati sasa wa kuendesha chama kisomi.

Nashauri yafuatayo kutengeneza mstakabali wa CHADEMA mpya yenye nidhamu ya hali ya juu.

Tundu Lissu apewe uenyekiti wa chama kuanzia sasa mpaka baada ya uchaguzi mwaka 2026.

Tundu Lissu apewe majukumu yote ya kuongoza harakati za kutengeneza katiba mpya.

Sababu zangu za kumtaka Tundu Lissu ni kama zifutazo...

1: Ndiye mpinzani pekee aliyebaki anayeweza kuiangusha serikali iliyoko madarakani.

2: Ndiye msomi ambaye elimu yake si ya kutilia shaka hata kidogo

3: Ni mtetezi na nwakilishi wa mawazo ya watanzania walio wengi.

4: Anatoka maeneo ya katikati mwa nchi ambapo ni rahisi kwake kuanza kutengeneza network ya kushinda urais.

5: Ndiye mtu asiyependa Rushwa kwa tabia yake.

Mbowe kazi uliyoifanya imetosha kiukweli tuhuma ulizopewa zinatosha wewe kukaa pembeni na kufanya biashara zako maisha yakaendelea.

Muachie chama Tundu Lissu apambane na mkulu.

Lissu akiungana na msomi mwenzie Mashiji naamini chadema itaenda vizuri..
 
Unamtafutia balaa wewe. Unataka ajenge bifu na Mtukufu Mwenyekiti ili afukuzwe uanachama? Unajua nini kilimuondoa Zitto Kabwe? Ama kilimuua Chacha Wangwe?
 
Back
Top Bottom