Maoni yangu: Usiingie mkenge wa router za 5G za mitandao ya simu

Tigo fiber ndo habari. Sema nmegundua niko sensitive na 5g naumwa kichwa
 
Gharama za kujiunga ni tsh ngapi mkuu?
Gharama ni kifurushi tu unachotaka, router unapewa Free.

Japo unaweza amua nunua router yao kwa matumizi yako binafsi

Gharama za router zimetofautiana
 
Kwa tulio nje ya mji ambako hakuna 5G,hiyo 4G/3G inatufaa?
 
Acheni na ujinga wa router watafute Simbanet Tanzania kwa business connection au Zuku fibre utakuja kunishukuru.... speed kubwa muda wote alafu unlimited...
 
Gharama ni kifurushi tu unachotaka, router unapewa Free.

Japo unaweza amua nunua router yao kwa matumizi yako binafsi

Gharama za router zimetofautiana

Ndiyo zile wanazosema home internet postpaid? Supa Kasi? Kuna mtu aliniambia unalipia kwanza miezi miwili ndiyo wanakupa.
 
Asante mkuu, hiyo ya 20mbps unalipia shilingi ngapi kwa mwezi? je kuna malipo mengie kabla ya kupata huduma yenyewe? Hiyo ya Voda itanifaa sana. Watu 4, devices 5 tu.
 
The cheapest of them all ni airtel, kwa mantiki wanakupa 30mbs kwa 110, voda ni 20mbps kwa 115, japo speed yao una stream 4k video bila shida
Hiyo ya airtel ya 30mbps huwezi kustream 4K?
 
Kuwa na router za kampuni zote hizo ni mzigo. Kwanini usiwe na router moja universal na ukawa una badili simcards? 🤔
 
Ahsante sana.

Tigo wakiona huu uzi wataenda lilia washroom.
Ndio niko kwenye window-shopping ya kufanya manunuzi ya hii bidhaa. Huyu mwamba amenisaidia kuwapangua Tigo. Ilikuwa nimeiweka top kwenye priority list zangu ikifuatiwa na Voda kisha Airtel. Kwa style hii ya huu uzi na madini aliyoshusha mwamba hapa nimebakiza Airtel kama ya kwanza kisha Voda ya pili. Ngoja niendelee kusoma wadau nipate uzoefu wao
 
Kuwa na router za kampuni zote hizo ni mzigo. Kwanini usiwe na router moja universal na ukawa una badili simcards? 🤔
Hii itakulazimu ununue line tatu zote ziwe registered for unlimited data service. Wasiwasi wangu ni kwamba, hili linawezekana? Maana wanasema ili wakuunganishie line inabidi uende na router yako waiconnect kwa kutumia IMEI number ya router yako na simCard. Sijui limekaaje hili kitaalamu wataalamu msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…