Maoni yangu: Usiingie mkenge wa router za 5G za mitandao ya simu

Maoni yangu: Usiingie mkenge wa router za 5G za mitandao ya simu

Mimi ni mtumiaji wa 5G router zote Airtel,voda na Tigo.

Ukweli katika hizi router 3 mitandao ya ukweli ambayo naweza mshauri mtu atumie ni miwili tu.

Airtel na Vodacom.

Tigo ni wezi sio unlimited wanakupa unlimited kwa speed uliyolipia kisha wakiona unakamua kweli kweli bando kwa limit walokuekea wanashusha speed up to 0.1kb/sec.

Hii speed itakua hovyo mpaka saa 6 usiku ikibadilika siku wana reset wanakuoa tena speed yako. Ukiendelea kupakua matonge unabugia ukifikisha limit yao wanakata tena mpk kesho yake.

Dont go for tigo...kama unaipenda pesa yako. Kwa mnaotaka LIMITED PACKAGe speed yao iko njema.

Airtel

Hawa ni pure unlimited hawana janja janja unaserereka utakavyo ila tu router yao ili i perform vizuri hakikisha haipati joto, ikipata joto ikichemka inaathiri speed kwakua ofisini kuna AC huwa naitega sehemu ambapo najua itapgwa barid haswa naiongezea na fan inakua baridi muda wote.

Ina perform vizuri sana na zaidi ninachoipendea airtel ni power bank hao ya router inayokupa uwezo wakuzurura na router yako kwa begi anywhere.

Go for airtel,na recommend.

Vodacom

HAwa wako poa sana tena wana pure unlimited ila na wao router yao hakikisha isipate joto ila kuna muda notification light inawaka tu red ujue isha heat unachotakiwa ni kui zima na kutulia dk 1 unaiwasha tena unaendelea kuserereka.

Voda wako njema hawana shida go for it... wana router yao ya NOKIA tamu sana kali mnoo..

Faida ya voda kwenye malipo mwezi ukiisha huduma inaendelea hawakati huduma unaweza usilipe hata miezi mi 3.

Ila Airtel na Tigo mwisho wa mwezi ukifika huduma inazima kama umeme wa tanesco.

Airtel ukifanya malipo inawaka on spot.. tigo mpka uwasiliane nao sjui nn ki ufupi TIGO NI HOVYO.
Voda wao nao ukisubiri wakuzimie ukifanya malipo lazima upge simu wakuwashie ila airtel ni ukishajiunga tu unasererekA..

VODA na TIGO kipengele kwenye kuwashiwa huduma utapga wee hadi ukome.
Tigo fiber ndo habari. Sema nmegundua niko sensitive na 5g naumwa kichwa
 
Gharama za kujiunga ni tsh ngapi mkuu?
Gharama ni kifurushi tu unachotaka, router unapewa Free.

Japo unaweza amua nunua router yao kwa matumizi yako binafsi

Gharama za router zimetofautiana
 
Ilikuwa ni swala la kuingia kwenye settings tu, na kutatua tatizo:

1. Ondoa default settings Hiyo ya mwishoni: ( Default settings inaruhusu router kubadili network mode)
View attachment 3073429
2. Na badala yake weka: (Hapa tumezuia roter isitmie netwok mode zingine kama 4G zenye kasi ndogo)
View attachment 3073430
- Hapo kasi ya internet huwa haishuki. Hata kama signal bar imeshuka na kubakia 1 .

Kwa mwingine yeyote ajaribu na alete mrejesho.
Kwa tulio nje ya mji ambako hakuna 5G,hiyo 4G/3G inatufaa?
 
Acheni na ujinga wa router watafute Simbanet Tanzania kwa business connection au Zuku fibre utakuja kunishukuru.... speed kubwa muda wote alafu unlimited...
 
Gharama ni kifurushi tu unachotaka, router unapewa Free.

Japo unaweza amua nunua router yao kwa matumizi yako binafsi

Gharama za router zimetofautiana

Ndiyo zile wanazosema home internet postpaid? Supa Kasi? Kuna mtu aliniambia unalipia kwanza miezi miwili ndiyo wanakupa.
 
Inategemea na unafanya nini, ila kwa nyumban kama wote mnatumia simu tu inaweza tosha, ila kama mnatumia kwa video streaming haitoshi!
Natumia vodacom ile ya 20mbps, inatoshea watu wanne wenye smartphone na tv na stream had 1080p ambayo ni almost hd.
Asante mkuu, hiyo ya 20mbps unalipia shilingi ngapi kwa mwezi? je kuna malipo mengie kabla ya kupata huduma yenyewe? Hiyo ya Voda itanifaa sana. Watu 4, devices 5 tu.
 
The cheapest of them all ni airtel, kwa mantiki wanakupa 30mbs kwa 110, voda ni 20mbps kwa 115, japo speed yao una stream 4k video bila shida
Hiyo ya airtel ya 30mbps huwezi kustream 4K?
 
hii spidi ya 10mbps kwa matumizi ya kawaida tu ya familia si inatosha kabisa? au ni slow sana
Ni kweli hii kasi inatosha kabisa.
1724016978702.png

=
1724017024319.png
 
Kuwa na router za kampuni zote hizo ni mzigo. Kwanini usiwe na router moja universal na ukawa una badili simcards? 🤔
 
Ahsante sana.

Tigo wakiona huu uzi wataenda lilia washroom.
Ndio niko kwenye window-shopping ya kufanya manunuzi ya hii bidhaa. Huyu mwamba amenisaidia kuwapangua Tigo. Ilikuwa nimeiweka top kwenye priority list zangu ikifuatiwa na Voda kisha Airtel. Kwa style hii ya huu uzi na madini aliyoshusha mwamba hapa nimebakiza Airtel kama ya kwanza kisha Voda ya pili. Ngoja niendelee kusoma wadau nipate uzoefu wao
 
Kuwa na router za kampuni zote hizo ni mzigo. Kwanini usiwe na router moja universal na ukawa una badili simcards? 🤔
Hii itakulazimu ununue line tatu zote ziwe registered for unlimited data service. Wasiwasi wangu ni kwamba, hili linawezekana? Maana wanasema ili wakuunganishie line inabidi uende na router yako waiconnect kwa kutumia IMEI number ya router yako na simCard. Sijui limekaaje hili kitaalamu wataalamu msaada
 
Back
Top Bottom