Maono: 2039 wimbi la wanawake litakuwa kubwa. Watauana kwa kugombania wanaume

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Naliiona hali ikianza katika hali ya utani. Taarifa ya kwanza ya habari kuhusu kukatiliwa kwa mwanamama mwenye umri wa miaka zaidi ya arobaini dhidi ya binti wa miaka 20+ itasikika kwenye kituo cha runinga. Habari hii itawaacha midomo wazi wanadamu, ndipo itasikika kauli ya "Wanaume wamejazana kibao tu, wenzetu wanagombania mwanaume mmoja. Ni ajabu"

Hivyo hivyo kimasihala, itasikika habari nyingine na nyingine, kisha nyingine tena. Hali haitokuwa shwari, wanawake wataumizana vibaya, watavunjana viungo vya mwili, watafanyiana ukatili wa kila namna na mwisho wa siku watauana.

Hali hii itaanzia nchi za wenzetu. Ukatili wa kwanza kushangaza akili za mwanadamu utatokea kwenye nchi moja kubwa ya bara la Asia. Haitoishia hapo tu, itafika hadi barani Afrika.

Hakutokuwa na mwanamke wa kuringa tena pindi atakapotongozwa na mwanaume. Awe ni mwanamke mzuri wa shepu, wa sura, mnene, mfupi, mrefu, mwembamba, hawa wote watajigonga kwa mwanaume mmoja

Itafikia mahala wanawake wataingia makubaliano wao kwa wao kuwa watoke na mwanaume mmoja. Familia zitaishi sawa na maisha ya kuku ya jogoo mmoja na mitetea kumi.

Nalimuona mwanamke mrembo akimbembeleza mwanaume asiye na pesa, "Ewe baba yangu, nakuomba unistiri na hii aibu, walau unioe tu, kuhusu mahitaji nitajitegemea mimi kama mimi.

Mashoga wote watajidhihirisha hata mchana kweupe. Italazimika kupishana na wanawake 20 barabarani ili ukutane na mwanaume mmoja. Pia naliwaona wanaume ambao hawatokuwa na hamu ya kuwa na wanawake, rundo la wanaume wasiowaza kuoa kabisa. Wengi watajikita katika kuyasaka maisha.

Nalisikia kilio kingine cha wanawake kudai haja za kimwili kutoka kwa wapenzi na marafiki zao pasi na mafanikio, hata wale waliowaoa wasiwatimizie.

Hali hii itakuja kama jinsi ambavyo ugonjwa wa covid 19 ulivyokuja, hali hii itachelewa sana kutoweka, lakini mwisho wa siku itapotea kusikojulikana na kuacha makovu yasiyo na kifani. Chuki ya mwanamke dhidi ya mwanamke mwenzie haitojificha tena.

Maono mengine bado sijayapatia tafsiri, pindi nitakapofanikiwa tafsiri zake, nitaweka hapa

Iweni na siku njema

1678355754549.png
 
Kwani tukigombaniwa kutakuwa na shida gani?

Si ndiyo mtakuwa na nyie mmeshafika kwenye akhadi ya 72 kwa 1?

Sisi wengine hadi hivi sasa tayari tupo huko kwenye 72 kwa 1.

Tunasubiri TBL watutengenezee mifereji ya pombe tu.
 
Naliiona hali ikianza katika hali ya utani. Taarifa ya kwanza ya habari kuhusu kukatiliwa kwa mwanamama mwenye umri wa miaka zaidi ya arobaini dhidi ya binti wa miaka 20+ itasikika kwenye kituo cha runinga. Habari hii itawaacha midomo wazi wanadamu, ndipo itasikika kauli ya "Wanaume wamejazana kibao tu, wenzetu wanagombania mwanaume mmoja. Ni ajabu"

Hivyo hivyo kimasihala, itasikika habari nyingine na nyingine, kisha nyingine tena. Hali haitokuwa shwari, wanawake wataumizana vibaya, watavunjana viungo vya mwili, watafanyiana ukatili wa kila namna na mwisho wa siku watauana.

Hali hii itaanzia nchi za wenzetu. Ukatili wa kwanza kushangaza akili za mwanadamu utatokea kwenye nchi moja kubwa ya bara la Asia. Haitoishia hapo tu, itafika hadi barani Afrika.

Hakutokuwa na mwanamke wa kuringa tena pindi atakapotongozwa na mwanaume. Awe ni mwanamke mzuri wa shepu, wa sura, mnene, mfupi, mrefu, mwembamba, hawa wote watajigonga kwa mwanaume mmoja

Itafikia mahala wanawake wataingia makubaliano wao kwa wao kuwa watoke na mwanaume mmoja. Familia zitaishi sawa na maisha ya kuku ya jogoo mmoja na mitetea kumi.

Nalimuona mwanamke mrembo akimbembeleza mwanaume asiye na pesa, "Ewe baba yangu, nakuomba unistiri na hii aibu, walau unioe tu, kuhusu mahitaji nitajitegemea mimi kama mimi.

Mashoga wote watajidhihirisha hata mchana kweupe. Italazimika kupishana na wanawake 20 barabarani ili ukutane na mwanaume mmoja. Pia naliwaona wanaume ambao hawatokuwa na hamu ya kuwa na wanawake, rundo la wanaume wasiowaza kuoa kabisa. Wengi watajikita katika kuyasaka maisha.

Nalisikia kilio kingine cha wanawake kudai haja za kimwili kutoka kwa wapenzi na marafiki zao pasi na mafanikio, hata wale waliowaoa wasiwatimizie.

Hali hii itakuja kama jinsi ambavyo ugonjwa wa covid 19 ulivyokuja, hali hii itachelewa sana kutoweka, lakini mwisho wa siku itapotea kusikojulikana na kuacha makovu yasiyo na kifani. Chuki ya mwanamke dhidi ya mwanamke mwenzie haitojificha tena.

Maono mengine bado sijayapatia tafsiri, pindi nitakapofanikiwa tafsiri zake, nitaweka hapa

Iweni na siku njema

Hali hiyo ni ngumu kutokea endapo mfumo wa michepuko utaendelea kudumu. Ikiwa mfumo wa michepuko utasizi ndipo hali itabadilika.
 
Miaka hyo ni mbali ..Ebu angalia sasa jaribu kumwambia binti utamuoa kama haujawekwa do huko whatsap .

Maandiko yapo sawa muda wote kwa sasa wimbi ni kubwa sana na mashauzi yamepungua kabisa....wanashuka thamani ngono imekuwa Bei che mfano hapa Dar.
 
Mabint wa wapi Hao ukiwaambia ndoa wanakuweka whatsàp 😂😂😂
 
Ngoja nipostpone mipango yangu ya ndoa mpaka wakati huo,, ntakuwa bado kijana..
 
Siku hizi unakuta wanawake wengi wanakutaka huku wanajua una mke. Yaani unaweza kupata mke bila mahari
 
Back
Top Bottom