Maono: 2039 wimbi la wanawake litakuwa kubwa. Watauana kwa kugombania wanaume

Maono: 2039 wimbi la wanawake litakuwa kubwa. Watauana kwa kugombania wanaume

Naliiona hali ikianza katika hali ya utani. Taarifa ya kwanza ya habari kuhusu kukatiliwa kwa mwanamama mwenye umri wa miaka zaidi ya arobaini dhidi ya binti wa miaka 20+ itasikika kwenye kituo cha runinga. Habari hii itawaacha midomo wazi wanadamu, ndipo itasikika kauli ya "Wanaume wamejazana kibao tu, wenzetu wanagombania mwanaume mmoja. Ni ajabu"

Hivyo hivyo kimasihala, itasikika habari nyingine na nyingine, kisha nyingine tena. Hali haitokuwa shwari, wanawake wataumizana vibaya, watavunjana viungo vya mwili, watafanyiana ukatili wa kila namna na mwisho wa siku watauana.

Hali hii itaanzia nchi za wenzetu. Ukatili wa kwanza kushangaza akili za mwanadamu utatokea kwenye nchi moja kubwa ya bara la Asia. Haitoishia hapo tu, itafika hadi barani Afrika.

Hakutokuwa na mwanamke wa kuringa tena pindi atakapotongozwa na mwanaume. Awe ni mwanamke mzuri wa shepu, wa sura, mnene, mfupi, mrefu, mwembamba, hawa wote watajigonga kwa mwanaume mmoja

Itafikia mahala wanawake wataingia makubaliano wao kwa wao kuwa watoke na mwanaume mmoja. Familia zitaishi sawa na maisha ya kuku ya jogoo mmoja na mitetea kumi.

Nalimuona mwanamke mrembo akimbembeleza mwanaume asiye na pesa, "Ewe baba yangu, nakuomba unistiri na hii aibu, walau unioe tu, kuhusu mahitaji nitajitegemea mimi kama mimi.

Mashoga wote watajidhihirisha hata mchana kweupe. Italazimika kupishana na wanawake 20 barabarani ili ukutane na mwanaume mmoja. Pia naliwaona wanaume ambao hawatokuwa na hamu ya kuwa na wanawake, rundo la wanaume wasiowaza kuoa kabisa. Wengi watajikita katika kuyasaka maisha.

Nalisikia kilio kingine cha wanawake kudai haja za kimwili kutoka kwa wapenzi na marafiki zao pasi na mafanikio, hata wale waliowaoa wasiwatimizie.

Hali hii itakuja kama jinsi ambavyo ugonjwa wa covid 19 ulivyokuja, hali hii itachelewa sana kutoweka, lakini mwisho wa siku itapotea kusikojulikana na kuacha makovu yasiyo na kifani. Chuki ya mwanamke dhidi ya mwanamke mwenzie haitojificha tena.

Maono mengine bado sijayapatia tafsiri, pindi nitakapofanikiwa tafsiri zake, nitaweka hapa

Iweni na siku njema

Sawa Nabii..tukutane 2039
 
"Wakati dunia ikiwa na uhaba wa wanaume, wanaume hao hao wachache mzungu anajitahidi kuwabadili ili wawe mashoga kabisa na useless! "
 
Hali uliyoandika yalishaandijwa kwenye biblia. Na saivi hali ni mbaya. Wanawake wana ushindani mkubwa kwa sababu ya mashoga na mateja.
 
Naliiona hali ikianza katika hali ya utani. Taarifa ya kwanza ya habari kuhusu kukatiliwa kwa mwanamama mwenye umri wa miaka zaidi ya arobaini dhidi ya binti wa miaka 20+ itasikika kwenye kituo cha runinga. Habari hii itawaacha midomo wazi wanadamu, ndipo itasikika kauli ya "Wanaume wamejazana kibao tu, wenzetu wanagombania mwanaume mmoja. Ni ajabu"

Hivyo hivyo kimasihala, itasikika habari nyingine na nyingine, kisha nyingine tena. Hali haitokuwa shwari, wanawake wataumizana vibaya, watavunjana viungo vya mwili, watafanyiana ukatili wa kila namna na mwisho wa siku watauana.

Hali hii itaanzia nchi za wenzetu. Ukatili wa kwanza kushangaza akili za mwanadamu utatokea kwenye nchi moja kubwa ya bara la Asia. Haitoishia hapo tu, itafika hadi barani Afrika.

Hakutokuwa na mwanamke wa kuringa tena pindi atakapotongozwa na mwanaume. Awe ni mwanamke mzuri wa shepu, wa sura, mnene, mfupi, mrefu, mwembamba, hawa wote watajigonga kwa mwanaume mmoja

Itafikia mahala wanawake wataingia makubaliano wao kwa wao kuwa watoke na mwanaume mmoja. Familia zitaishi sawa na maisha ya kuku ya jogoo mmoja na mitetea kumi.

Nalimuona mwanamke mrembo akimbembeleza mwanaume asiye na pesa, "Ewe baba yangu, nakuomba unistiri na hii aibu, walau unioe tu, kuhusu mahitaji nitajitegemea mimi kama mimi.

Mashoga wote watajidhihirisha hata mchana kweupe. Italazimika kupishana na wanawake 20 barabarani ili ukutane na mwanaume mmoja. Pia naliwaona wanaume ambao hawatokuwa na hamu ya kuwa na wanawake, rundo la wanaume wasiowaza kuoa kabisa. Wengi watajikita katika kuyasaka maisha.

Nalisikia kilio kingine cha wanawake kudai haja za kimwili kutoka kwa wapenzi na marafiki zao pasi na mafanikio, hata wale waliowaoa wasiwatimizie.

Hali hii itakuja kama jinsi ambavyo ugonjwa wa covid 19 ulivyokuja, hali hii itachelewa sana kutoweka, lakini mwisho wa siku itapotea kusikojulikana na kuacha makovu yasiyo na kifani. Chuki ya mwanamke dhidi ya mwanamke mwenzie haitojificha tena.

Maono mengine bado sijayapatia tafsiri, pindi nitakapofanikiwa tafsiri zake, nitaweka hapa

Iweni na siku njema

Hakuna jipya chini ya jua. Kama hadithi kama hii imo mpaka ndani ya biblia, nini kitaishangaza hii dunia iliyojaa wana laana?
 
Kanisa lako linapatikana wapi ndugu
Hapana mkuu, sina kanisa. Wala sio mtu wa ibada sana. Ila nimejikita kwenye Yoga, meditaton, Lotrinatuon, Realm Camic na Spiral Soul. Kufungua third eye kwangu ni kawaida tu, aura za watu naziona sana hasa nyakati za jioni
 
Biblia imeandika itafika wakati wanawake 7 watataka mwanamme 1 angalau hata waitwe kwa jina lake

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hawa wanawake lazima watakuwa wameshafika kuanzia 40+ maana ndio umri ambao mwanamke hana cha kuringia tena na hata akisema asiwe na time na mahusiano hakuna mtu anakuwa na time nae so anateseka kwa upweke hadi anakuwa kama mwehu.

Kuna siku nipo kitambaa cheupe kuna kona namuona mwanamke wa makamo umri nadhani ni 40+ amesimama sehemu ya pekee yake. Ukimtazama unaona kabisa huyu anaishi mwenyewe tu lazima hakuna namna. Amekaa anacheza cheza miziki ya Amapiano anakeep up na generation ya ujana wakati umri umeshasema baba jeni bai bai.

Nikamtazama nikamuonea huruma yaani kwa muda nilipotea nikawa namtazama na kujiuliza maswali kuwa huyu kuna kipindi kuna mwanaume alimtaka kwa mahaba sana na akamuomba twende tukaishi pamoja na kujenga familia ya baba mama na watoto ila kwasababu ya mvuto na usichana alimchomolea na kumwambia yeye bado hayupo tayari kuna ndoto zake bado anafukuzia. Leo huyo hapo amekaa anazuga kula bata. Miaka 40+ kwa mwanamke sio umri wa kuwa viwanja vya bata ambavyo vimejaa mabinti wa umri chini ya 23 kwa wingi sana. Hao wanaenda huko kujifunza ya Dunia na kuvutia wanaume sehemu ya starehe, wewe wa miaka 40+ unakwenda kufanya nini hapo?! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kimsingi mwanamke wa kuanza 30+ ukienda viwanja basi kuna sehemu za kwenda tena na familia yako ya mume, na watoto na wageni wako. Ila sio kama nguruwe tu unakwenda maeneo ya kula bata.
 
Ila kwa mwenendo wa mabinti wa sasa hii hali kuna uwezekano mkubwa ikaja kutokea kweli. Katika kizazi cha wanawake wa hovyo kuwahi kutokea tokea uhuru basi ni hawa mabinti waliozaliwa kuanzia miaka ya 1980's.

Maana wana maamuzi ya hovyo sana na huwa hawajitazami kuwa wataangukia wapi kesho yao. Na idadi inazidi kuongezeka. Sasa hawa wakifika 35+ na hali hizi za sasa ndio basi tena.
 
Siku hizi unakuta wanawake wengi wanakutaka huku wanajua una mke. Yaani unaweza kupata mke bila mahari

Hili nimeliexperience Yani mwanamke anakutongoza kabisa akijua wewe mme wa mtu.
 
Back
Top Bottom