Moja kwa moja.
Katika harakati zote za maandamano bongo hakuna maandamano ambayo yanajoto , hamasa , vuguvugu na muamko mkubwa kama hii ya safari hii , pamoja na hayo sioni kabisa kufanikiwa kutokana na sababu nyingi miongoni mwa hizo ni zifuatazo ;
1. Nguvu yake , umaarufu na hamasa ni mitandaoni pekee wakati mtaani na kwenye ground nguvu ndogo mno .
Hapa tuna la kujifunza mwaka 2015 kipindi cha uchaguzi mkuu Lowasa aliwekeza nguvu nyingi mtaani huku gruondini akawa akapenyeza ushawishi wake akawa habari ya Mjini na Chadema mitaani ilipenyeza sera zako ipasavyo haswa kwa vijana kila mtu akawa anaimba mabadiliko kipindi hiko nipo sekondari mpaka madarasani stori za Lowasa na Mabadiliko zilitawala.
Haya maandamano kwa uchunguzi wangu Kuna utofauti mkubwa kati ya nguvu yake mtandaoni na mitaani , Mimi kipindi cha karibuni nimepita na kukaa mikoa takribani Mi4 na Dar ikiwemo kuanzia vijiweni mpaka mtaani hakuna hamasa kabisa na wengine hawajui nini kinaendelea.
More analysis
Ukitaka jambo bongo lifanikiwe haswa kisiasa usitegemee nguvu ya mtandaoni pekee, nguvu ya mtaani ni msingi mkubwa , maana Watanzania wengi hawana access ya mitandao ya kijamii wengine wengi hata smart phone hawana.
Then
Watu ambao wako na hamasa zaidi na maandamano ni watu wa mitandaoni ambalo ni kundi chache na ndani yake kuna Keyboard warriors wengi mno . Na ikizimwa mitandao siku hiyo ndio basi washapoteana mapema hakuna kushikana masikio na kujazana hamasa.
Kumbuka wabongo ni wazuri wakishambulia kutokea pembeni mitandaoni hapo watashambulia sana na kukujaza, watakujaza kama kipindi Bernard Membe alisepa na kijiji mitandaoni ila fanbase yake mtaani na influence ilikuwa ndogo mno matokeo yakaanza kwenye kampeni kulikuwa kweupe Kisha akaamua Bora akaepembeni tu.
2. Kufeli kimipango na Mbinu : Hakuna Mikakati Maalumu Wala mpango mmoja wa kueleweka.
If you fail to plan , you plan to fail .
Mikakati na mipango ni silaha muhimu katika kufanikisha mambo . Ukichunguza maandamano hayana muelekeo tunaanza wapi na kuishia wapi bali wako verry diverse and disorganized . Kila mtu ana mpango wake na bila mpango na mpangilio maalumu. Mara kuvamia vituo vya kupiga kura , mara kuvamia polisi mara maandamano ya Amani nk full mvurugano .
3. Asili ya uoga ya wabongo na kusalitiana .
Mnaweza kupanga jambo vizuri na mkawa pamoja ila ikitokea shida kidogo ni rahisi kukukimbia na kusaliti , spirit kama hiyo hamuwezi kutoboa kufanya makubwa
👇
Kisa cha kweli yaliowahi kunikuta.
Mwaka mmoja katika Mtaa Fulani Dar es Salaam katika eneo tunaloishi ghafla yalikuja Magreda na Askari kadhaa wachache Wenye mitutu kubomoa majumba bila ya kibali Cha kueleweka Wala Tangazo wakidai Wananchi tumevamia eneo la mtu eneo na Raia tulikuwa wengi ila tuliangalia tu uvunjaji usikuwa wa kisheria bila kutoa Tangazo mapema walamuda wa kuhamisha vitu unavunjiwa kikatili ukiwa na Kali zako ndani haupewi muda wa kuhamisha na nyumba zilivunjwa nyingi sana katika eneo kubwa.
Baada ya hapo Raia tukaweka Kikao tuandamane mpaka ikulu Magogoni tukaonane na Mzee Magi Raisi wa wanyonge atusaudia , basi likakodiwa gari kubwa (Eicher) na wakaahidi na kukubaliana wote tutafua ikulu mpaka kieleweke hadi tutrend bongo nzima tusikike vilio vyetu
Kufika maeneo Karibu na Ikulu Raia wakashuka kuelekea getini walinzi wakawasimamishwa na watu wa usalama pale wakasema shida zao wakaambiwa wasubiri pembeni wafanye process ili wamuone Rais waongee nae, kumbe mtu yule akapiga simu kuongeza nguvu ya ulinzi kwa askari wengine wengi zaidi , Raia ghafla wakaona askari wanazidi kuongezeka wakastukia mchongo mmoja mmoja akaanza kuzuga wengine kujichanganya na raia wengine wakijifanya wapita njia na wanunuzi wa bidhaa ,wengine wakakimbia kabisa eneo lile na wengine
wachache waliobaki wakamatwa kupelekwa polisi bila kufanikiwa lolote , hapo ndipo nikagundua wabongo hata tukidhulumiwa hatuna umoja , ushirikiano na utayari wa kupambana mpaka mwisho kishujaa.
Hii inafikirisha sana .
Acha tunyooshwe sisi Wapumbavu , wezi , madhalimu na hatujui tunachotaka .
Wakati wa Magu Kuna watu mpaka wakavuka mipaka katika kumsema na kumsingizia mengi pasipo na ushahidi , wengine mlisema bora tuongozwe na yeyote hata sufuria kuliko Magu. Hadi alipofariki mkazidi kumtukana na kufurahi kila siku na kuendelea kumsema mlikuwa mnamuita Shetani Magu sasa kimya hasemwi tena baada ya kisanga kipya mnamkumbuka na wengine kuanza kumuona shujaa.
Kutoa uongozi madarakani ni False hopes.
Nashangaa disorganized people wanajipa matumaini kwenye disorganized yao protest wanaweza kutoa uongozi madarakani kiurahisi , hilo sidhani labda kwa backup kubwa ya wakubwa na hata ikifanikiwa kwa nguvu za raia labda ni Fujo tu za hapa na pale .
Kama Kenya na uchizi wao #RutoMustGo Ruto mpaka sasa anadunda halafu sisi na Madhaifu yetu kibao tunaweza kweli ?
Maoni yangu .
Mimi binafsi napinga njia ya maandamano sababu ndani yake unakuta Kuna mengi maovu , vifo vya raia , Fujo , wizi , uharibifu wa Mali za Umma n.k na wanaomia na kuathirika wengi ni raia wa kawaida . Inashangaza mtu haumtaki kiongozi kwa nini uharibu miundombinu ya nchi , uchome moto na ufunge barabara ?
Watanzania wengi zitokee Fujo za kutosha kiasi Cha kupelekea kutofanya kazi na biashara wiki nzima ni pigo kubwa sana halafu kibaya zaidi hakibaliki chochote positively.
#LindaAmaniYaNchiYako
View attachment 3484664