Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ni wazi kuwa uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na udanganyifu mkubwa kuliko uchaguzi mwingine wowote tuliowahi kuufanya. Ushahidi ni mwingi mno hadi imekua kama kichekesho hivi.
Sasa, kuna scenario mbili hapa za kujaribu kuelezea kwanini hali imekua hivyo na kila moja ina consequences zake tofauti.
Scenerio 1. Haya ni matokeo ya Rais JPM, amefanikiwa kuvunja nguvu za vyombo vyote vya dola na mihimili yake, sasa kila mtu anajaribu kumfurahisha boss kwa kutekeleza maagizo wanayopewa kama yalivyo.
Scenario 2. Huu ni mpango wa kizalendo wa 'deep state', wenye lengo la kurahisisha mabadiliko ya kikatiba kwa mslahi mapana ya Taifa.
********************
Tuanze na scenario ya pili, ndani ya state machinery iko wazi kuwa nchi yetu inahitaji katiba mpya, katiba yetu inahitaji marekebisho makubwa ili kuendana na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi pasipo kuhatarisha maslahi ya nchi.
Kwa mfano, muundo wa Muungano wetu ni kitendawili kikubwa kwenye hizi siasa za vyama vingi, ikitokea Rais wa Zanzibar na Rais wa JMT wanatoka vyama tofauti basi kuna hatari kubwa ya kutokuelewana ndani ya Muungano na hata kuhatarisha uhai wa Muungano wenyewe.
Kwa kulitambua hitaji hilo, wakati wa awamu ya Mh. Kikwete ulianzishwa mchakato wa kutafuta katiba mpya lakini kutokana na mawazo kinzani ambayo yalikua ni mazuri lakini yanahatarisha uhai wa taifa ilibidi mchakato usitiswe.
Sasa kwa bunge lililochaguliwa la JMT ambalo ni la chama kimoja na linadhibitiwa kirahisi na mwenyekiti wa CCM na serikali ya Zanzibar chini ya Ndugu Mwinyi pamoja na baraza lake la wawakilishi ambavyo navyo vinadhibitiwa vilivyo na mwenyekiti wa CCM, ni wazi kuwa mchakato unaweza kurudishwa na kupita smoothly.
Kwenye senario hii, JPM hatojiongezea muda, bali ataacha legacy kubwa ya kutuachia katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi, mamlaka yaliyopunguzwa ya Rais, demokrasia ya kweli ya vyama vingi na muundo sustainable wa muungano (serikali moja). Pia vyama vya upinzani vitapata nafasi ya kuzaliwa upya.
Kwa senario hii, mabeberu watatuunga mkono, hakutakua na vikwazo vya kiuchumi wala kuharibika kwa mahusiano, after all wao wenyewe ni miongoni mwa wadau walio facilitate Muungano wetu. Mwisho wa siku mambo yote yatakwenda vizuri na sote (isipokuwa baadhi ya wazanzibari) tutafurahia nchi yetu.
2025 kutakua na uchaguzi safi ulio huru na wa haki.
****************
Tukirudi kwenye Scenario ya kwanza, hii inatisha kwa kweli na kama matokeo ya uchaguzi huu yametokana na tamaa tu ya JPM isiyo na malengo yoyote ya kizalendo basi tujiandae kisaikilojia.
Nchi yetu itakwenda kupita katika giza nene ambalo wengi wetu hatujawahi kuliona.
Kwanza, kuna uwezekano tukatumia fedha nyingi sana kwenye operations za kijeshi za kujaribu kuwazima wale magaidi wa Cabo Delgado Msumbiji au walau kuwazuia wasiingie upande wetu na hatutopata msaada wowote wa maana wa kifedha na kiintelijensia kutoka kwa mabeberu. Na kama unadhani tunaweza kukimbilia kwa Urusi basi nikutaarifu kuwa Msumbiji wameshafanya hivyo, Urusi ilituma hadi mercenaries wake lakini kwa hali inavyoendelea ni wazi kuwa wamegonga mwamba.
Ukizingatia utajiri mkubwa wa mafuta na gesi kwenye eneo la Cabo Delgado na Mtwara, Inaonekana kuna mkono mkubwa wenye nguvu nyingi nyuma ya wale magaidi, siku zinavyozidi kwenda wanazidi kujiimarisha kwa zana za kivita, idadi ya wapiganaji, inteligensia pamoja na eneo wanalodhibiti.
Vilevile, kutokana na matokeo ya uchaguzi huu, ni wazi kuwa kuna watu wengi watakua wanahisi kudhulumiwa haki yao na kuonewa, watu hawa hususani vijana ni perfect target kuwa recruited na vikundi vya kigaidi. Hii ni moja ya madhara mabaya zaidi ya kuminya haki. Watanzania hawa wema kabisa wanaweza kuishia mikononi mwa hao magaidi na kutumiwa kuiumiza nchi yao. Ikumbukwe tayari kuna taarifa za kuwepo watanzania wengi tu kwenye vikundi vya kigaidi kule Somalia na sasa Msumbiji.
Juu ya hayo yote, kutakua na vikwazo vya kiuchumi. Ikumbukwe vikwazo hivi huwa haiwekewi nchi moja kwa moja bali ni viongozi pamoja na makampuni ya kibiashara yenye uhusiano wa karibu na viongozi au serikali. Hii huwa inatosha kabisa kuvuruga uchumi wa nchi na kupafanya hapa nchini kuwa jehanamu ndogo.
Sasa haya yakitokea, kila mtu atateseka na hata wale waliomsaidia JPM kuiba uchaguzi na kuminya haki watajuuta, kwasababu nchi ikiharibika inaharibika kwa kila mtu.
Pia, kwakuwa JPM, amekwisha dhibiti bunge, mahakama, serikali na CCM, anao uwezo wa kufanya chochote kile, hata akitaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani basi atafanya hivyo na hakutakua na wa kupinga.