Ni wazi kuwa uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na udanganyifu mkubwa kuliko uchaguzi mwingine wowote tuliowahi kuufanya. Ushahidi ni mwingi mno hadi imekua kama kichekesho hivi.
Sasa, kuna scenario mbili hapa za kujaribu kuelezea kwanini hali imekua hivyo, na kila moja ina consequences zake tofauti.
Scenerio 1. Haya ni matokeo ya Rais JPM, amefanikiwa kuvunja nguvu za vyombo vyote vya dola na mihimili yake, sasa kila mtu anajaribu kumfurahisha boss kwa kutekeleza maagizo wanayopewa kama yalivyo.
Scenario 2. Huu ni mpango wa kizalendo wa 'deep state', wenye lengo la kurahisisha mabadiliko ya kikatiba kwa mslahi mapana ya taifa.
********************
Tuanze na scenario ya pili, ndani ya state machinery iko wazi kuwa nchi yetu inahitaji katiba mpya, katiba yetu inahitaji marekebisho makubwa ili kuendana na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi pasipo kuhatarisha maslahi ya nchi.
Kwa mfano, muundo wa muungano wetu ni kitendawili kikubwa kwenye hizi siasa sa vyama vingi, ikitokea rais wa Zanzibar na rais wa JMT wanatoka vyama tofauti basi kuna hatari kubwa ya kutokuelewana ndani ya muungano na hata kuhatarisha uhai wa muungano wenyewe.
Kwa kulitambua hitaji hilo, wakati wa awamu ya Mh. Kikwete ulianzishwa mchakato wa kutafuta katiba mpya lakini kutokana na mawazo kinzani ambayo yalikua ni mazuri lakini yanahatarisha uhai wa taifa ilibidi mchakato usitiswe.
Sasa kwa bunge lililochaguliwa la JMT ambalo ni la chama kimoja na linadhibitiwa kirahisi na mwenyekiti wa CCM, na serikali ya Zanzibar chini ya Ndugu Mwinyi pamoja na baraza lake la wawakilishi ambavyo navyo vinadhibitiwa vilivyo na mwenyekiti wa CCM, ni wazi kuwa mchakato unaweza kurudishwa na kupita smoothly.
Kwenye senario hii, JPM hatojiongezea muda, bali ataacha legacy kubwa ya kutuachia katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi, mamlaka yaliyopunguzwa ya rais, demokrasia ya kweli ya vyama vingi na muundo sustainable wa muungano (serikali moja). Pia vyama vya upinzani vitapata nafasi ya kuzaliwa upya.
Kwa senario hii, mabeberu watatuunga mkono, hakutakua na vikwazo vya kiuchumi wala kuharibika kwa mahusiano, after all wao wenyewe ni miongoni mwa wadau walio facilitate muungano wetu. Mwisho wa siku mambo yote yatakwenda vizuri na sote (isipokuwa baadhi ya wazanzibari) tutafurahia nchi yetu.
2025 kutakua na uchaguzi safi ulio huru na wa haki.
****************
Tukirudi kwenye Scenario ya kwanza, hii inatisha kwa kweli, na kama matokeo ya uchaguzi huu yametokana na tamaa tu ya JPM isiyo na malengo yoyote ya kizalendo basi tujiandae kisaikilojia.
Nchi yetu itakwenda kupita katika giza nene ambalo wengi wetu hatujawahi kuliona.
Kwanza, kunauwezekano tukatumia fedha nyingi sana kwenye operations za kijeshi za kujaribu kuwazima wale magaidi wa Cabo Delgado Msumbiji, au walau kuwazuia wasiingie upande wetu, na hatutopata msaada wowote wa maana wa kifedha na kiintelijensia kutoka kwa mabeberu. Na kama unadhani tunaweza kukimbilia kwa Urusi basi nikutaarifu kuwa Msumbiji wameshafanya hivyo, Urusi ilituma hadi mercenaries wake lakini kwa hali inavyoendelea ni wazi kuwa wamegongwa mwamba.
Ukizingatia utajiri mkubwa wa mafuta na gesi kwenye eneo la Cabo Delgado na Mtwara, Inaonekana kuna mkono mkubwa wenye nguvu nyingi nyuma ya wale magaidi, siku zinavyozidi kwenda wanazidi kujiimarisha kwa zana za kivita, idadi ya wapiganaji, inteligensia pamoja na eneo wanalodhibiti.
Vilevile, kutokana na matokeo ya uchaguzi huu, ni wazi kuwa kuna watu wengi watakua wanahisi kudhulumiwa haki yao na kuonewa, watu hawa hususani vijana ni perfect target kuwa recruited na vikundi vya kigaidi. Hii ni moja ya madhara mabaya zaidi ya kuminya haki. Watanzania hawa wema kabisa wanaweza kuishia mikononi mwa hao magaidi na kutumiwa kuiumiza nchi yao. Ikumbukwe tayari kuna taarifa za kuwepo watanzania wengi tu kwenye vikundi vya kigaidi kule Somalia na sasa Msumbiji.
Juu ya hayo yote, kutakua na vikwazo vya kiuchumi. Ikumbukwe vikwazo hivi huwa haiwekewi nchi moja kwa moja bali ni viongozi pamoja na makampuni ya kibiashara yenye uhusiano wa karibu na viongozi au serikali. Hii hua inatosha kabisa kuvuruga uchumi wa nchi na kupafanya hapa nchini kuwa jehanamu ndogo.
Sasa haya yakitokea, kila mtu atateseka na hata wale waliomsaidia JPM kuiba uchaguzi na kuminya haki watajuuta, kwasababu nchi ikiharibika inaharibika kwa kila mtu.
Pia, kwakua JPM, amekwisha dhibiti bunge, mahakama, serikali na CCM, anao uwezo wa kufanya chochote kile, hata akitaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani basi atafanya hivyo na hakutakua na wa kupinga.
Mkuu, waweza kuwa na hoja kwa kiwango fulani , lakini mtazamo wangu ni tofauti kidogo.
Scenario ya kwanza.
Raisi ni amiri mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama hivyo hawezi kuamuru tu majeshi hayo yafanye anavyotaka, zipo taratibu za kufuata.
Hiyo ni kwa sababu wapo washauri na washauri elekezi ambao wanamsaidia hata kuelewa hichi ulichoandika.
Sema kwa mtindo wa utawala wake hata vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa sasa vinatekeleza majukumu yao kwa uzuri zaidi kuliko huko nyuma na kila kiongozi wake anawajibika kwani kuna kitu chaitwa KPI ambacho raisi amekiweka.
Scenario ya pili, Deep state.
Hili limeongelewa sana hata kule jukwaa la intelligence kwamba hakuna nchi siyo na deep state.
Kabla ya 2015 Deep state iliona umuhimu wa mabadiliko kwenye ngazi ya juu na hiyo yote ikiwa ni kwa kulinda misingi ya amani na utulivu ambayo tulijengewa na hayati baba wa taifa.
Kulikuwepo na dalili za Tanzania kuingia kwenye "uncompromised state" kwamba hakuna mwenye sauti ya kukemea na kila mtu alikuwa anafanya yake wakiwemo wageni na kwa kutambua hilo CCM wenyewe hawakuwa na jibu la nini kifanyike.
Hivyo kwa maslahi mapana ya Tanzania ikabidi kuwepo mabadiliko ya haraka yaani "rapid transformation" ambayo yataendana na matarajio ya watanzania.
Hivyo ikaonekana raisi John Magufuli ni perfect candidate kwa utekelezaji wa kazi hiyo na ndicho kilichoamuliwa pale Dodoma October 2015.
Hao wengine wote Lowasa, Sumaye, Membe, Nyalandu na wengine ni sehemu ya DS na wana uhakika wa pensheni.
Deep State kwa sasa inajipa justification ya maamuzi mbalimbali ya CCM na serikali yake khasa baada ya yale tuliyoyashuhudia yakifanywa na Tundu Lissu, Robert Amsterdam na genge lao zima.
Ni kwamba kwa sasa Tundu Lissu ameachwa tu lakini kwa vyombo vya usalama chini ya DS, yeye na Robert Amsterdam na genge zima ni sehemu ya matishio au "threats" kwa usalama wa taifa Tanzania ingawa ni kwa "level" ya kati.
Hivyo Tanzania haiwezi kuchukua hatua zozote ambazo zitaingiza kwenye mtego ambao waendelea kutegwa.
WalterRodney katika kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" amesema wazi kwamba nguvu za kisiasa na uporaji wa rasilimali za Africa ndio sababu kubwa ya bara hilo kurudi nyuma kimaendeleo.
Anaamini kwamba kila mwafika anawajibika kujifunza na kuelewa mfumo wa kibepari na jinsi ya kukabiliana nao.
Walter Rodney ni kama Frantz Fanon na kitabu chake cha "The Wretched of the Earth".
Fanon anazungumzia athari za kisaikolojia ambazo ukoloni ulimpatia mwafrika na bara zima na madhara yake kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Hivyo jukumu la kiongozi na viongozi wa Afrika ni kuamka kifikra na kuachana na tabia ya kutegemea mawazo ya kuturudisha nyuma na kuondoa mazingira ambayo yanalifanya bara la Afrika kuendelea kuwa tegemezi kwa nchi za kibeberu.
Haiwezekani mtu kama seneta Mendes asimame leo aseme kwamba Tanzania haiheshimu mikataba ilosainiwa huko nyuma mikataba ambayo ilikuwa ikiwanufaisha kampuni kama Symbion ambayo yeye mwenyewe Mendes alikuwa ni dalali wao.
Hivyo hitimisho langu ni kwamba watanzania wameamua kuchagua maendeleo baada ya kuona mambo ambayo yamefanywa na CCM na serikali yake kwa miaka mitano ilopita.
Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza kabisa ulijikita kwenye maendeleo ya uchumi wa vitu na watu hivyo madaraja, barabara, reli, umeme hadi vijinini ni mambo ambayo yamewapa imani wapiga kura kutaka CCM itawale tena kwa miaka mingine mitano.
Hivyo miaka mitano ijayo raisi Magufuli atahukumiwa kwa kazi na utendaji wake ambao hauna shaka.