Uchaguzi 2020 Maono yangu juu ya Tanzania ndani ya miaka mitano ijayo

Uchaguzi 2020 Maono yangu juu ya Tanzania ndani ya miaka mitano ijayo

CCM wamejulishwa kuwa JPM anaendelea na mipango yake.

Kama wakumbuka uzuri JK na hayati BWM walikuwa hawaeshi kwenda mjengoni kujaribu kupooza lakini DS wakawa wanakumbusha umuhimu wa kuwa focused na ajenda zao.
Umeandika hisia zako tu sidhani kama una uhakika.
 
Ni wazi kuwa uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na udanganyifu mkubwa kuliko uchaguzi mwingine wowote tuliowahi kuufanya. Ushahidi ni mwingi mno hadi imekua kama kichekesho hivi.

Sasa, kuna scenario mbili hapa za kujaribu kuelezea kwanini hali imekua hivyo, na kila moja ina consequences zake tofauti.

Scenerio 1. Haya ni matokeo ya Rais JPM, amefanikiwa kuvunja nguvu za vyombo vyote vya dola na mihimili yake, sasa kila mtu anajaribu kumfurahisha boss kwa kutekeleza maagizo wanayopewa kama yalivyo.

Scenario 2. Huu ni mpango wa kizalendo wa 'deep state', wenye lengo la kurahisisha mabadiliko ya kikatiba kwa mslahi mapana ya taifa.

********************

Tuanze na scenario ya pili, ndani ya state machinery iko wazi kuwa nchi yetu inahitaji katiba mpya, katiba yetu inahitaji marekebisho makubwa ili kuendana na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi pasipo kuhatarisha maslahi ya nchi.

Kwa mfano, muundo wa muungano wetu ni kitendawili kikubwa kwenye hizi siasa sa vyama vingi, ikitokea rais wa Zanzibar na rais wa JMT wanatoka vyama tofauti basi kuna hatari kubwa ya kutokuelewana ndani ya muungano na hata kuhatarisha uhai wa muungano wenyewe.

Kwa kulitambua hitaji hilo, wakati wa awamu ya Mh. Kikwete ulianzishwa mchakato wa kutafuta katiba mpya lakini kutokana na mawazo kinzani ambayo yalikua ni mazuri lakini yanahatarisha uhai wa taifa ilibidi mchakato usitiswe.

Sasa kwa bunge lililochaguliwa la JMT ambalo ni la chama kimoja na linadhibitiwa kirahisi na mwenyekiti wa CCM, na serikali ya Zanzibar chini ya Ndugu Mwinyi pamoja na baraza lake la wawakilishi ambavyo navyo vinadhibitiwa vilivyo na mwenyekiti wa CCM, ni wazi kuwa mchakato unaweza kurudishwa na kupita smoothly.

Kwenye senario hii, JPM hatojiongezea muda, bali ataacha legacy kubwa ya kutuachia katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi, mamlaka yaliyopunguzwa ya rais, demokrasia ya kweli ya vyama vingi na muundo sustainable wa muungano (serikali moja). Pia vyama vya upinzani vitapata nafasi ya kuzaliwa upya.

Kwa senario hii, mabeberu watatuunga mkono, hakutakua na vikwazo vya kiuchumi wala kuharibika kwa mahusiano, after all wao wenyewe ni miongoni mwa wadau walio facilitate muungano wetu. Mwisho wa siku mambo yote yatakwenda vizuri na sote (isipokuwa baadhi ya wazanzibari) tutafurahia nchi yetu.

2025 kutakua na uchaguzi safi ulio huru na wa haki.
****************

Tukirudi kwenye Scenario ya kwanza, hii inatisha kwa kweli, na kama matokeo ya uchaguzi huu yametokana na tamaa tu ya JPM isiyo na malengo yoyote ya kizalendo basi tujiandae kisaikilojia.

Nchi yetu itakwenda kupita katika giza nene ambalo wengi wetu hatujawahi kuliona.

Kwanza, kunauwezekano tukatumia fedha nyingi sana kwenye operations za kijeshi za kujaribu kuwazima wale magaidi wa Cabo Delgado Msumbiji, au walau kuwazuia wasiingie upande wetu, na hatutopata msaada wowote wa maana wa kifedha na kiintelijensia kutoka kwa mabeberu. Na kama unadhani tunaweza kukimbilia kwa Urusi basi nikutaarifu kuwa Msumbiji wameshafanya hivyo, Urusi ilituma hadi mercenaries wake lakini kwa hali inavyoendelea ni wazi kuwa wamegongwa mwamba.

Ukizingatia utajiri mkubwa wa mafuta na gesi kwenye eneo la Cabo Delgado na Mtwara, Inaonekana kuna mkono mkubwa wenye nguvu nyingi nyuma ya wale magaidi, siku zinavyozidi kwenda wanazidi kujiimarisha kwa zana za kivita, idadi ya wapiganaji, inteligensia pamoja na eneo wanalodhibiti.

Vilevile, kutokana na matokeo ya uchaguzi huu, ni wazi kuwa kuna watu wengi watakua wanahisi kudhulumiwa haki yao na kuonewa, watu hawa hususani vijana ni perfect target kuwa recruited na vikundi vya kigaidi. Hii ni moja ya madhara mabaya zaidi ya kuminya haki. Watanzania hawa wema kabisa wanaweza kuishia mikononi mwa hao magaidi na kutumiwa kuiumiza nchi yao. Ikumbukwe tayari kuna taarifa za kuwepo watanzania wengi tu kwenye vikundi vya kigaidi kule Somalia na sasa Msumbiji.

Juu ya hayo yote, kutakua na vikwazo vya kiuchumi. Ikumbukwe vikwazo hivi huwa haiwekewi nchi moja kwa moja bali ni viongozi pamoja na makampuni ya kibiashara yenye uhusiano wa karibu na viongozi au serikali. Hii hua inatosha kabisa kuvuruga uchumi wa nchi na kupafanya hapa nchini kuwa jehanamu ndogo.

Sasa haya yakitokea, kila mtu atateseka na hata wale waliomsaidia JPM kuiba uchaguzi na kuminya haki watajuuta, kwasababu nchi ikiharibika inaharibika kwa kila mtu.

Pia, kwakua JPM, amekwisha dhibiti bunge, mahakama, serikali na CCM, anao uwezo wa kufanya chochote kile, hata akitaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani basi atafanya hivyo na hakutakua na wa kupinga.
Daaa.yn.nimeisoma.marambili.hadimachozi.yananitirirka.kwakweli.maskini.nchiyangu.hiiyooooooo.mpaka.rwandwaaaaaaaa
 
Scenario namba one inaendana na ukweli zaidi

Jambo moja niongezee tu hapo,ni gharama sana kuongoza watu wasiokutaka.

Utatumia nguvu nyingi sana za dola kuvunja wale wanaokupinga na katika kutenda hayo mambo mawili yatakumaliza.

La kwanza ni kuvunja haki za watu na sheria na hivyo kutengwa na dunia.Hili litaudhoofisha uchumi wako.

La pili matumizi ya fedha katika vyombo vya dola yatakuwa makubwa kutokana na nguvu inayotumika kutiisha umma usiotaka kutii.

Wale unaowatumia kufanya uharamia,watazidisha ziada ya uharamia wao kwa ajili ya ile principle ya "chukua chako mapema" na "sisi ndio machinery yake hawezi kutufanya kitu".

Corruption itaongezeka sehemu "takatifu" kama kwenye majeshi n.k huku kukiwa hakuna sauti za taasisi pinzani zinazopinga na kukusaidia kunyoosha mambo.Mwisho wake ni internal conflict between wale wale ambao leo wameconspire na wewe kuiitiisha nchi under your absolute rule,kukiwa hakuna adui mwingine wa kumnyooshea kidole na kila mtu akitaka kufaidika na kuonekana ni zaidi among you,mtaanza kugombana na kuvurugana,fedha hiyo kidogo kutokana na uchumi dhoofu nayo itatumika na dola na nyingine kupotelea kwenye corruption za ndani kwa ndani.

Mambo yasiyotegemewa kama ugaidi wa Kusini kule ndio itakuwa chumvi kwenye kidonda.Vijana kama wazanzibar itakuwa rahisi sana kujiunga na haya makundi.

Jamii isiyoridhika na mambo ni unpredictable na inajifunza kutoka juu.So suala la watu kuanza kubaguana kimaslahi katika jamii iliyobanwa na ufukara na isiyokuwa na tumaini kwa uongozi wake ni inevitable.Inatengenezwa jamii ambayo inaweza kuwa ngumu sana kuitiisha.

Haya yote yatauangusha uchumi kabisa na itafikia mahali yule "mbwa" uliyekuwa unamlisha vizuri na anakulinda "usiku" atageuka kuwa hostile pale utakaposhindwa kumlisha.!
Absolute power corrupt absolutely!
Umeona mbali mkuu
 
Kuhusu vikwazo, Robert Amsterdam ameandia hivi kupitia twitter akimjibu kamanda wa operation wa Polisi bwana Liberatus:

Libertus- here is a warning for you. There are millions of voters who have been defrauded by a Party that has absolutely no legitimacy. Conduct yourself peacefully or international law will follow you! Sanctions are coming!
 
Sikubaliani na mawazo yako kwenye hii scenario namba 2. Kwamba Deep State ilazimishe muungano wa serikali moja! Huoni kwamba huu ni ukatili kwa wazanzibari? Hio deep state ni nani mpaka ilazimishe kunyang'anya watu nchi yao?
Ina maana mnaamini katika kunyang'anya na kulazimisha kupora nchi bila ya ridhaa zao? Hivyo wewe unaona hili ni sawa? Kumbe ni kweli nyinyi watanganyika wengi mnatamani kuizamisha Zanzibar.
Mkuu kwani wazanzibari wamewahi kuridhia muungano?

Kama harumu moja imewahi kuhalalishwa huko nyuma basi ujue haitokuwa nongwa kwa hao watu kuhalalisha haramu nyingine.

BTW, ni kweli serikali moja sio haki kwa wazanzibari. Lakini CCM wakiamua iwe hivyo sidhani kama kuna kizingiti chochote mbele yao.
 
Off course anaweza kuwa na idea zake kama zile za alipokuwa waziri wa ujenzi lakini asilimia kubwa ya maamuzi yake anafuata mwongozo pia.
JPM kasha vuruga kila utaratibu wa nchi hi haya maneno ya deep state ya mebaki kama" political science theories" kuua kwa upizani kiujinga katika ulimwengu wa kimataifa kwasasa ni 'political suicide' kwa Tz hamna mjumbe wa deep state wakukishauri hivo, huyu JPM akuandaliwa na CCM kabla ya kupewa madaraka, anafanya political blunders nyingi. Sio mfasi wa political philosophy yoyote,.......Hata Urusi licha kua political giant wanaheshimu vyama vya upizani na wanavihitaji viwepo.
 
Hata tulupofika hatujafika Buhati mbaya ni mipango ya kuanzia 2014, na 2015 ilikiwa ni utekelezaji wake wa kutawaliwa kidikiteta kwa miaka 10, japo watekelezaji wa CCM hawakujua kama mambo yatakuwa hivi , sasa 2020-2025 kuna Mabadiliko makubwa yatatokea , Mosi KATIBA MPYA ambayo itakuwa iko sawa na matakwa ya deep state

Pili, CCM kwa sasa inatumika tu , ili Deep state wakamilishe mipango ya kutengeneza vizuri nchi ,

Tatu, Vyombo vya Dola vitahitaji kujivua toka CCM na hapo kutatengenezwa chama cha mizania au vilivyopo sasa lakini mamlaka makubwa wanasiasa wataondolewa ili kuepusha vibaraka
Nimekuelewa sana mkuu.
 
Mkuu, waweza kuwa na hoja kwa kiwango fulani , lakini mtazamo wangu ni tofauti kidogo.

Scenario ya kwanza.

Raisi ni amiri mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama hivyo hawezi kuamuru tu majeshi hayo yafanye anavyotaka, zipo taratibu za kufuata.

Hiyo ni kwa sababu wapo washauri na washauri elekezi ambao wanamsaidia hata kuelewa hichi ulichoandika.

Sema kwa mtindo wa utawala wake hata vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa sasa vinatekeleza majukumu yao kwa uzuri zaidi kuliko huko nyuma na kila kiongozi wake anawajibika kwani kuna kitu chaitwa KPI ambacho raisi amekiweka.

Scenario ya pili, Deep state.

Hili limeongelewa sana hata kule jukwaa la intelligence kwamba hakuna nchi siyo na deep state.

Kabla ya 2015 Deep state iliona umuhimu wa mabadiliko kwenye ngazi ya juu na hiyo yote ikiwa ni kwa kulinda misingi ya amani na utulivu ambayo tulijengewa na hayati baba wa taifa.

Kulikuwepo na dalili za Tanzania kuingia kwenye "uncompromised state" kwamba hakuna mwenye sauti ya kukemea na kila mtu alikuwa anafanya yake wakiwemo wageni na kwa kutambua hilo CCM wenyewe hawakuwa na jibu la nini kifanyike.

Hivyo kwa maslahi mapana ya Tanzania ikabidi kuwepo mabadiliko ya haraka yaani "rapid transformation" ambayo yataendana na matarajio ya watanzania.

Hivyo ikaonekana raisi John Magufuli ni perfect candidate kwa utekelezaji wa kazi hiyo na ndicho kilichoamuliwa pale Dodoma October 2015.

Hao wengine wote Lowasa, Sumaye, Membe, Nyalandu na wengine ni sehemu ya DS na wana uhakika wa pensheni.

Deep State kwa sasa inajipa justification ya maamuzi mbalimbali ya CCM na serikali yake khasa baada ya yale tuliyoyashuhudia yakifanywa na Tundu Lissu, Robert Amsterdam na genge lao zima.

Ni kwamba kwa sasa Tundu Lissu ameachwa tu lakini kwa vyombo vya usalama chini ya DS, yeye na Robert Amsterdam na genge zima ni sehemu ya matishio au "threats" kwa usalama wa taifa Tanzania ingawa ni kwa "level" ya kati.

Hivyo Tanzania haiwezi kuchukua hatua zozote ambazo zitaingiza kwenye mtego ambao waendelea kutegwa.

WalterRodney katika kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" amesema wazi kwamba nguvu za kisiasa na uporaji wa rasilimali za Africa ndio sababu kubwa ya bara hilo kurudi nyuma kimaendeleo.

Anaamini kwamba kila mwafika anawajibika kujifunza na kuelewa mfumo wa kibepari na jinsi ya kukabiliana nao.

Walter Rodney ni kama Frantz Fanon na kitabu chake cha "The Wretched of the Earth".

Fanon anazungumzia athari za kisaikolojia ambazo ukoloni ulimpatia mwafrika na bara zima na madhara yake kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Hivyo jukumu la kiongozi na viongozi wa Afrika ni kuamka kifikra na kuachana na tabia ya kutegemea mawazo ya kuturudisha nyuma na kuondoa mazingira ambayo yanalifanya bara la Afrika kuendelea kuwa tegemezi kwa nchi za kibeberu.

Haiwezekani mtu kama seneta Mendes asimame leo aseme kwamba Tanzania haiheshimu mikataba ilosainiwa huko nyuma mikataba ambayo ilikuwa ikiwanufaisha kampuni kama Symbion ambayo yeye mwenyewe Mendes alikuwa ni dalali wao.

Hivyo hitimisho langu ni kwamba watanzania wameamua kuchagua maendeleo baada ya kuona mambo ambayo yamefanywa na CCM na serikali yake kwa miaka mitano ilopita.

Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza kabisa ulijikita kwenye maendeleo ya uchumi wa vitu na watu hivyo madaraja, barabara, reli, umeme hadi vijinini ni mambo ambayo yamewapa imani wapiga kura kutaka CCM itawale tena kwa miaka mingine mitano.

Hivyo miaka mitano ijayo raisi Magufuli atahukumiwa kwa kazi na utendaji wake ambao hauna shaka.
Propaganda za kuzimua uovu! Hakuna mtakaemdanganya dunia ya leo. Simple ni bora mkubali tu mmeiba uchaguzi na hili halikubaliki na kuna price yake. Msituleteee story za alinacha hapa! Hakuna cha deep satate wala mavi ya deep state hapa!
Kilicho wazi ni kwamba mmefanya uharamia mkubwa na kutudhulumu haki zetu za msingi. Na kwa hili halisameheki!
 
Wewe mwenyewe hoja zako zinakinzana.

[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Scenerio 1. Haya ni matokeo ya Rais JPM, amefanikiwa kuvunja nguvu za vyombo vyote vya dola na mihimili yake, sasa kila mtu anajaribu kumfurahisha boss kwa kutekeleza maagizo wanayopewa kama yalivyo.

Scenario 2. Huu ni mpango wa kizalendo wa 'deep state', wenye lengo la kurahisisha mabadiliko ya kikatiba kwa mslahi mapana ya Taifa.

********************

Tuanze na scenario ya pili.

Sasa kwa bunge lililochaguliwa la JMT ambalo ni la chama kimoja na linadhibitiwa kirahisi na mwenyekiti wa CCM na serikali ya Zanzibar chini ya Ndugu Mwinyi pamoja na baraza lake la wawakilishi ambavyo navyo vinadhibitiwa vilivyo na mwenyekiti wa CCM.

[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Kwenye senario hii, JPM ataacha legacy kubwa ya kutuachia katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi, mamlaka yaliyopunguzwa ya Rais, demokrasia ya kweli ya vyama vingi

Kimsingi wananchi hatujui tunapopelekwa.
 
Hongera mkuu,umechambua vizuri sana ingawa yote kwa yote senario ya kwanza ndio mpango mzima wa huyu jamaa ambae kaacha legacy ambayo hata watangulizi wake hawakuwahi kuifanya roho ya ubaguzi iliyokithiri.
 
Hizi habari za deep state ni hadithi za alinacha , ni hadithi za vijiweni, hiyo deep state inafanya kazi kwenye nchi za wenzetu huuko kama UK, USA, israel n.k ndiyo maana umaona kiongozi akivurunda anawekwa kitimoto.

Kwa hapa tz hamna kitu kama hicho eti deep state, Magu kaonyesha kwamba yeye ni mwamba kuliko hao mnaowaita deep state et al.. na anauwezo wa kuwafanya chochote na wakabaki kumsifia na kumwimbia mapambio. Yeye ndiye alpha na omega kwa hapa Tz kwa sasa.

Tuache kuleta propaganda za kusadikika eti deep state. Ingekua hivyo wangeshazuia kupotea kwa 1.5 tr, uchotwaji wa mapesa hazina bila baraka za bunge, kufukuza CAG Kinyume na sheria, kutumia pesa za umma katika white elephant project, na kama kweli kungekua na kitu hicho kiitwacho deep state basi nchi yetu ingekua mbali sana kimaendeleo.
 
JPM kasha vuruga kila utaratibu wa nchi hi haya maneno ya deep state ya mebaki kama" political science theories" kuua kwa upizani kiujinga katika ulimwengu wa kimataifa kwasasa ni 'political suicide' kwa Tz hamna mjumbe wa deep state wakukishauri hivo, huyu JPM akuandaliwa na CCM kabla ya kupewa madaraka, anafanya political blunders nyingi. Sio mfasi wa political philosophy yoyote,.......Hata Urusi licha kua political giant wanaheshimu vyama vya upizani na wanavihitaji viwepo.
Nope. Kila kitu kipo under careful control, take it or frame it! Kinafanyika kwa mipango makini. Unatakiwa uwe mtulivu sana (na pengine uvae uzalendo usio na mashaka) ili uweze kumwelewa vyema huyu Kiongozi mahiri wa Afrika. Sijawahi kamwe kuwa na mashaka na hatua zake madhubuti kwa ajili ya ustawi wetu kama raia na maslahi mapana ya taifa.
 
Mkuu, waweza kuwa na hoja kwa kiwango fulani , lakini mtazamo wangu ni tofauti kidogo.

Scenario ya kwanza.

Raisi ni amiri mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama hivyo hawezi kuamuru tu majeshi hayo yafanye anavyotaka, zipo taratibu za kufuata.

Hiyo ni kwa sababu wapo washauri na washauri elekezi ambao wanamsaidia hata kuelewa hichi ulichoandika.

Sema kwa mtindo wa utawala wake hata vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa sasa vinatekeleza majukumu yao kwa uzuri zaidi kuliko huko nyuma na kila kiongozi wake anawajibika kwani kuna kitu chaitwa KPI ambacho raisi amekiweka.

Scenario ya pili, Deep state.

Hili limeongelewa sana hata kule jukwaa la intelligence kwamba hakuna nchi siyo na deep state.

Kabla ya 2015 Deep state iliona umuhimu wa mabadiliko kwenye ngazi ya juu na hiyo yote ikiwa ni kwa kulinda misingi ya amani na utulivu ambayo tulijengewa na hayati baba wa taifa.

Kulikuwepo na dalili za Tanzania kuingia kwenye "uncompromised state" kwamba hakuna mwenye sauti ya kukemea na kila mtu alikuwa anafanya yake wakiwemo wageni na kwa kutambua hilo CCM wenyewe hawakuwa na jibu la nini kifanyike.

Hivyo kwa maslahi mapana ya Tanzania ikabidi kuwepo mabadiliko ya haraka yaani "rapid transformation" ambayo yataendana na matarajio ya watanzania.

Hivyo ikaonekana raisi John Magufuli ni perfect candidate kwa utekelezaji wa kazi hiyo na ndicho kilichoamuliwa pale Dodoma October 2015.

Hao wengine wote Lowasa, Sumaye, Membe, Nyalandu na wengine ni sehemu ya DS na wana uhakika wa pensheni.

Deep State kwa sasa inajipa justification ya maamuzi mbalimbali ya CCM na serikali yake khasa baada ya yale tuliyoyashuhudia yakifanywa na Tundu Lissu, Robert Amsterdam na genge lao zima.

Ni kwamba kwa sasa Tundu Lissu ameachwa tu lakini kwa vyombo vya usalama chini ya DS, yeye na Robert Amsterdam na genge zima ni sehemu ya matishio au "threats" kwa usalama wa taifa Tanzania ingawa ni kwa "level" ya kati.

Hivyo Tanzania haiwezi kuchukua hatua zozote ambazo zitaingiza kwenye mtego ambao waendelea kutegwa.

WalterRodney katika kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" amesema wazi kwamba nguvu za kisiasa na uporaji wa rasilimali za Africa ndio sababu kubwa ya bara hilo kurudi nyuma kimaendeleo.

Anaamini kwamba kila mwafika anawajibika kujifunza na kuelewa mfumo wa kibepari na jinsi ya kukabiliana nao.

Walter Rodney ni kama Frantz Fanon na kitabu chake cha "The Wretched of the Earth".

Fanon anazungumzia athari za kisaikolojia ambazo ukoloni ulimpatia mwafrika na bara zima na madhara yake kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Hivyo jukumu la kiongozi na viongozi wa Afrika ni kuamka kifikra na kuachana na tabia ya kutegemea mawazo ya kuturudisha nyuma na kuondoa mazingira ambayo yanalifanya bara la Afrika kuendelea kuwa tegemezi kwa nchi za kibeberu.

Haiwezekani mtu kama seneta Mendes asimame leo aseme kwamba Tanzania haiheshimu mikataba ilosainiwa huko nyuma mikataba ambayo ilikuwa ikiwanufaisha kampuni kama Symbion ambayo yeye mwenyewe Mendes alikuwa ni dalali wao.

Hivyo hitimisho langu ni kwamba watanzania wameamua kuchagua maendeleo baada ya kuona mambo ambayo yamefanywa na CCM na serikali yake kwa miaka mitano ilopita.

Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza kabisa ulijikita kwenye maendeleo ya uchumi wa vitu na watu hivyo madaraja, barabara, reli, umeme hadi vijinini ni mambo ambayo yamewapa imani wapiga kura kutaka CCM itawale tena kwa miaka mingine mitano.

Hivyo miaka mitano ijayo raisi Magufuli atahukumiwa kwa kazi na utendaji wake ambao hauna shaka.
Well-said. The only critical way to keep Africans down in terms of sustainable growth & development is to keep their leaders dependant on them---regarding the philosophy of leadership and approach to governance. If the leaders are truly 'initiated,' almost everything is liberated and falls into its proper course.
 
Kwenye senario hii, JPM hatojiongezea muda, bali ataacha legacy kubwa ya kutuachia katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi, mamlaka yaliyopunguzwa ya Rais, demokrasia ya kweli ya vyama vingi na muundo sustainable wa muungano (serikali moja). Pia vyama vya upinzani vitapata nafasi ya kuzaliwa upya.
LOOoo, mkuu, ulikuwa unatiririka vizuri sana, hadi ulipofika hapa ukaingiliwa na jini nadhani!

Inawezekana uliyoweka huko chini ni mazuri, lakini nimekosa nguvu za kuendelea hadi huko kutokana na aya hiyo hapo juu!
 
Nope. Kila kitu kipo under careful control, take it or frame it! Kinafanyika kwa mipango makini. Unatakiwa uwe mtulivu sana (na pengine uvae uzalendo usio na mashaka) ili uweze kumwelewa vyema huyu Kiongozi mahiri wa Afrika. Sijawahi kamwe kuwa na mashaka na hatua zake madhubuti kwa ajili ya ustawi wetu kama raia na maslahi mapana ya taifa.
Kama deep state Tz ingekuepo na kufanya kazi vizuri JPM asinge pita kwenye venting process nakua Raisi kwasababu sio mwana siasa mzuri, utaweka je Raisi asio jua kuongea kingereza vizuri, ateweza je ktuakirisha uko nje bila kujua kingereza vizuri.......
 
Back
Top Bottom