Uchaguzi 2020 Maono yangu juu ya Tanzania ndani ya miaka mitano ijayo

Tusiombe itokee hii. Zanzibar serikali moja haitakiwi. Ikitokea hivyo Zanzibar imekwisha. Mungu aepushe mbali hilo.
 
Magufuli aibe kura kwa kuchagizwa na mabadiliko ya Katiba mpya? No, hiyo sahau! Katiba si inapatikana kwa consensus? Sasa iweje ipatikane kupitia deselection of citizens from policy making mainstream? Scenario hii hapana!
 
Ni kweli, mbele kuna giza nene. Lakini bado siamini jinsi TISS, JWTZ, NEC na waandamizi wengine ndani ya serikali walivyoruhusu mambo haya yatokee, inashangaza. Labda kama scenario 2 ndio mpango uliopo.

Hao ni wachumia tumbo tu hawawezi kuwa wamelenga scenario 2 hapo wametawaliwa na ubinafsi tu wa kulinda matumbo yao. Wengine wanaona hata likitokea lolote wao watakuwa wameshajilimbikizia mali za kutosha. Tuna tatizo kubwa sana lakukosa wazalendo was kweli katika teuzi hakuna vetting ya kutosha ndo tumefikia hapo. Watu wanaotakiwa kushauri wapewa maelekezo tu.
 
Kwa upande wangu naona ujio wa Sheria ngumu zaidi zitakazopitishwa na Bunge hasa Kwenye suala la chama cha mapinduzi kujichimbia zaidi Kwenye madaraka..
(1)...mapungufu yote yaliyojitokeza Kwenye uchaguzi huu yatafanyiwa KAZI Kwa kutungiwa Sheria Kali zaidi
(2).... serikali ya CCM hakuna wanalowaza zaidi ya kubuni mbinu ya kuendelea madarakani hivyo wale wababe wa kutunga Sheria hivi sasa wapo kazini wakidesign namna ya kukandamiza upinzani zaidi
(1)....miaka hii mitano magufuli atakuwa na wakati mwingi wa kuangalia Nani anamwachia kijiti kwahiyo kazi kubwa itakuwa Kwa wateule wake ambao muda mwingi watafanya KAZI Kwa kumlamba miguu magufuli badala ya wananchi

uwe mpinzani au CCM katika miaka hii mitano watanzania watatamani kuhama nchi maana Hali ya utengamano wa nchi utatoweka kabisaaa
 
Hakika umenena vyema kabisa
 
Mimi bado nina imani sana na jpm. Hiyo scenario ya pili nadhani ndio lengo 2020-2025, ingawaje inaweza isitekelezwe kwa kufurahisha upinzani.
Baadhi ya maamuzi yanayofanywa kwa maslahi ya taifa yanaweza yasiwafurahishe wote. Pia upinzani huu wa 1995-2020 ndio umeisha rasmi kwa scenario hiyo. 2020 kwenda mbele utazaliwa upinzani mpya ambao utaaminiwa na dola.
 
Umechambua vizuri mkuu.

Scenario ya pili kama ikitekelezwa vizuri (licha ya kuwa dalili zake ni chache mno) basi uchaguzi wa 2025 CCM wanaweza kushinda kihalali kwani watakua wamegusa matakwa ya nchi.

Issue ni kwamba idadi ya wabunge wa upinzani ktk bunge lililopita haikua kikwazo kupitisha maamuzi yoyote ambayo wangetaka kupitisha hivyo hatuwezi kusema kuwa upinzani ulikua kikwazo bungeni.
 
Kabisa aiseeee tutarajie nchi kuwa kama Somalia ndani ya muda mfupi ujao watu wataanza kuikimbia nchi kwenda nchi jirani kutafuta ajira.
 
Scenario namba one inaendana na ukweli zaidi

Jambo moja niongezee tu hapo,ni gharama sana kuongoza watu wasiokutaka.

Utatumia nguvu nyingi sana za dola kuvunja wale wanaokupinga na katika kutenda hayo mambo mawili yatakumaliza.

La kwanza ni kuvunja haki za watu na sheria na hivyo kutengwa na dunia.Hili litaudhoofisha uchumi wako.

La pili matumizi ya fedha katika vyombo vya dola yatakuwa makubwa kutokana na nguvu inayotumika kutiisha umma usiotaka kutii.

Wale unaowatumia kufanya uharamia,watazidisha ziada ya uharamia wao kwa ajili ya ile principle ya "chukua chako mapema" na "sisi ndio machinery yake hawezi kutufanya kitu".

Corruption itaongezeka sehemu "takatifu" kama kwenye majeshi n.k huku kukiwa hakuna sauti za taasisi pinzani zinazopinga na kukusaidia kunyoosha mambo.Mwisho wake ni internal conflict between wale wale ambao leo wameconspire na wewe kuiitiisha nchi under your absolute rule,kukiwa hakuna adui mwingine wa kumnyooshea kidole na kila mtu akitaka kufaidika na kuonekana ni zaidi among you,mtaanza kugombana na kuvurugana,fedha hiyo kidogo kutokana na uchumi dhoofu nayo itatumika na dola na nyingine kupotelea kwenye corruption za ndani kwa ndani.

Mambo yasiyotegemewa kama ugaidi wa Kusini kule ndio itakuwa chumvi kwenye kidonda.Vijana kama wazanzibar itakuwa rahisi sana kujiunga na haya makundi.

Jamii isiyoridhika na mambo ni unpredictable na inajifunza kutoka juu.So suala la watu kuanza kubaguana kimaslahi katika jamii iliyobanwa na ufukara na isiyokuwa na tumaini kwa uongozi wake ni inevitable.Inatengenezwa jamii ambayo inaweza kuwa ngumu sana kuitiisha.

Haya yote yatauangusha uchumi kabisa na itafikia mahali yule "mbwa" uliyekuwa unamlisha vizuri na anakulinda "usiku" atageuka kuwa hostile pale utakaposhindwa kumlisha.!
Absolute power corrupt absolutely!
 
Hakika Kuna mijitu ya hovyo [ viazi ] kwa Tz yetu
Nakuombea utoke kwa huo upofu ndugu
 
Sikubaliani na mawazo yako kwenye hii scenario namba 2. Kwamba Deep State ilazimishe muungano wa serikali moja! Huoni kwamba huu ni ukatili kwa wazanzibari? Hio deep state ni nani mpaka ilazimishe kunyang'anya watu nchi yao?
Ina maana mnaamini katika kunyang'anya na kulazimisha kupora nchi bila ya ridhaa zao? Hivyo wewe unaona hili ni sawa? Kumbe ni kweli nyinyi watanganyika wengi mnatamani kuizamisha Zanzibar.
 
Wewe na mtoa mada mna mawazo kama yangu. Outcome yote ya huu ubakaji mmeielezea vema na ndo kitachotokea
 
Mkuu, waweza kuwa na hoja kwa kiwango fulani , lakini mtazamo wangu ni tofauti kidogo.

Scenario ya kwanza.

Raisi ni amiri mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama hivyo hawezi kuamuru tu majeshi hayo yafanye anavyotaka, zipo taratibu za kufuata.

Hiyo ni kwa sababu wapo washauri na washauri elekezi ambao wanamsaidia hata kuelewa hichi ulichoandika.

Sema kwa mtindo wa utawala wake hata vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa sasa vinatekeleza majukumu yao kwa uzuri zaidi kuliko huko nyuma na kila kiongozi wake anawajibika kwani kuna kitu chaitwa KPI ambacho raisi amekiweka.

Scenario ya pili, Deep state.

Hili limeongelewa sana hata kule jukwaa la intelligence kwamba hakuna nchi siyo na deep state.

Kabla ya 2015 Deep state iliona umuhimu wa mabadiliko kwenye ngazi ya juu na hiyo yote ikiwa ni kwa kulinda misingi ya amani na utulivu ambayo tulijengewa na hayati baba wa taifa.

Kulikuwepo na dalili za Tanzania kuingia kwenye "uncompromised state" kwamba hakuna mwenye sauti ya kukemea na kila mtu alikuwa anafanya yake wakiwemo wageni na kwa kutambua hilo CCM wenyewe hawakuwa na jibu la nini kifanyike.

Hivyo kwa maslahi mapana ya Tanzania ikabidi kuwepo mabadiliko ya haraka yaani "rapid transformation" ambayo yataendana na matarajio ya watanzania.

Hivyo ikaonekana raisi John Magufuli ni perfect candidate kwa utekelezaji wa kazi hiyo na ndicho kilichoamuliwa pale Dodoma October 2015.

Hao wengine wote Lowasa, Sumaye, Membe, Nyalandu na wengine ni sehemu ya DS na wana uhakika wa pensheni.

Deep State kwa sasa inajipa justification ya maamuzi mbalimbali ya CCM na serikali yake khasa baada ya yale tuliyoyashuhudia yakifanywa na Tundu Lissu, Robert Amsterdam na genge lao zima.

Ni kwamba kwa sasa Tundu Lissu ameachwa tu lakini kwa vyombo vya usalama chini ya DS, yeye na Robert Amsterdam na genge zima ni sehemu ya matishio au "threats" kwa usalama wa taifa Tanzania ingawa ni kwa "level" ya kati.

Hivyo Tanzania haiwezi kuchukua hatua zozote ambazo zitaingiza kwenye mtego ambao waendelea kutegwa.

WalterRodney katika kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" amesema wazi kwamba nguvu za kisiasa na uporaji wa rasilimali za Africa ndio sababu kubwa ya bara hilo kurudi nyuma kimaendeleo.

Anaamini kwamba kila mwafika anawajibika kujifunza na kuelewa mfumo wa kibepari na jinsi ya kukabiliana nao.

Walter Rodney ni kama Frantz Fanon na kitabu chake cha "The Wretched of the Earth".

Fanon anazungumzia athari za kisaikolojia ambazo ukoloni ulimpatia mwafrika na bara zima na madhara yake kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Hivyo jukumu la kiongozi na viongozi wa Afrika ni kuamka kifikra na kuachana na tabia ya kutegemea mawazo ya kuturudisha nyuma na kuondoa mazingira ambayo yanalifanya bara la Afrika kuendelea kuwa tegemezi kwa nchi za kibeberu.

Haiwezekani mtu kama seneta Mendes asimame leo aseme kwamba Tanzania haiheshimu mikataba ilosainiwa huko nyuma mikataba ambayo ilikuwa ikiwanufaisha kampuni kama Symbion ambayo yeye mwenyewe Mendes alikuwa ni dalali wao.

Hivyo hitimisho langu ni kwamba watanzania wameamua kuchagua maendeleo baada ya kuona mambo ambayo yamefanywa na CCM na serikali yake kwa miaka mitano ilopita.

Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza kabisa ulijikita kwenye maendeleo ya uchumi wa vitu na watu hivyo madaraja, barabara, reli, umeme hadi vijinini ni mambo ambayo yamewapa imani wapiga kura kutaka CCM itawale tena kwa miaka mingine mitano.

Hivyo miaka mitano ijayo raisi Magufuli atahukumiwa kwa kazi na utendaji wake ambao hauna shaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…