Maono yangu kutoka Temple Mount: Ipo siku CHADEMA itaongoza Tanzania

Very good saed nakupa big gap mtu wa maono ipo siku itatimia kikubwa afya ili tushuhudie mabadiliko makubwa ya kiutawala nchini tanzania
 
Kipi kingine umeshawahi pata maono kikatokea ili tufanye rejea?

Nauliza hayo kwa kuwa binafsi nipo sensitive sana na manabii na mitume wanaojituma wenyewe.
 
Tanzania ni Nchi huru. Hakuna taifa litaamka na kwenda kuamua mshindi wa uchaguzi wa nchi nyingine.

Tambua kwamba hapo unaambiwa hakuna jiwe litabaki bila kugeuzwa.

Hizi ni hadithi za Yesu na wafuasi wake siyo Tanzania na wananchi wake.

Kama Magu alisema yeye ni jiwe kwelikweli haimaanishi kwamba ni lile jiwe lenyewe ambalo lilikubali kugeuzwa.
 
Are you out of your mind? Rudia kusoma tena
 
CCM inajivunia katiba iliyopo na uvumilivu wa watanzania, kwa mfano kwa sasa kuna mgao wa umeme na maji lakini watanzania wapo kimya.. as if nothing has happened... hii ni nchi rahisi sana kuitawala.
 
Hatutaki kubishana na utabiri wako isije ikawa tunabishana na Mungu .
Mi utabiri wangi ni kwamba Mbowe atahukumiwa kweda jela miongo michache na Rais Samia atamhurumia.
 
Naono tu mchwa waliofukuzwa na Magufuli wanarudi katika Chama.
Wakisharudi katika Chama wanataka kuwaondoa mchwa wanaompenda Magufuli.
 
Dr. Slaa asingeuzwa akabakia Chadema mpaka leo, uchaguzi wa 2025 ungeweza kutoa matokeo ya njonzi yako hii uliyoota.

Lakini kwa mseto wa viongozi wa upinzani waliopo kwa sasa kwa ujumla wao, nitajie jina hata moja tu lifaalo ambalo linaweza kukubalika na waTz walio wengi.

Ujue kweli waTanzania wamechoshwa na Ccm, lakini je ni chama gani ama kiongozi gani mbadala anayeweza kukata kiu cha wana mageuzi nchini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la chama chenu mnalijua wenyeweee. Tungekuwa na chama cha upinzani imara tungejaribu kuwaunga mkono ili watuleteee umeme wa uhakika wa mwalim nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…