Maonyesho ya Ubunifu UDSM yanafikirisha

Maonyesho ya Ubunifu UDSM yanafikirisha

Wiki hi inayoishia nikiwa naelekea Changanyikeni nilibahatika kutembelea yanayoitwa Maonyesho ya Ubunifu pale Mlimani.

Aisee, kwa kweli inabidi vyuo hivi kujipanga upya. Maana dunia inaenda Mbele wao wapo Zama za mawe.

Sanamu la mabati mbona Fundi tu kitaa anatengeneza?

Utaalamu wenu mpaka PhD ndio umefika mwisho?

View attachment 1801671
[emoji23][emoji23][emoji23], Kazi kweli kweli
 
Engineer anapigania kubuni mashine ya kufyatulia tofali
Engineer anamsikiliza motivation Speaker anapomwambia angalia jamii inayokuzunguka kuna tatizo gani kisha ulitatue hiyo ni fursa... ! 😂😂
 
Wiki hi inayoishia nikiwa naelekea Changanyikeni nilibahatika kutembelea yanayoitwa Maonyesho ya Ubunifu pale Mlimani.

Aisee, kwa kweli inabidi vyuo hivi kujipanga upya. Maana dunia inaenda Mbele wao wapo Zama za mawe.

Sanamu la mabati mbona Fundi tu kitaa anatengeneza?

Utaalamu wenu mpaka PhD ndio umefika mwisho?

View attachment 1801671
Hahahaaaa nimechekaaaa
Kweli tuko Zama za mawe
 
Karibuni tufanye sayansi.
odf.png
 
Aisee. Nilistaajabu kuona Profesa katengeneza jiko la kutumia mwanga wa jua kupikia supu. Hivi ile dawa Yao ya kufukiza bado wanayo?
**Halafu mbona Kama hayo maonyesho wanafanya kwa kujificha? Promo hamna kabisa
...Mbona ninakumbuka kuwa miaka kadhaa nyuma kuna mtu aliwahi kuvumbua kitu kama hiki hiki...Jiko linalotumia mwanga wa jua kuchemshia maji na hata mboga???
 
Kalamu1

Babu unajua kwamba unapigia mbuzi gitaa...
Hapa unajaribu kuwaelewasha "matutusa"
Utakesha..........
 
Wazee wakukopy na kupaste..ndio amana nasemaga bila mzugu tungekua bado maporini tuna kula mizizi na kuvaa ngozi..bongo hakuna wasomi ila kuna wakarirji wazuri.

#MaendeleoHayanaChama
Hii inchi watu wengi Wana shule..Ila hawana Elimu ......
 
Hata sasa sijui kama kuna chuo chochote hapa nchini, au taasisi yoyote inayojihusisha na utafiti juu ya ugonjwa huo!

Nilisikitika sana kuwa nawasikia hata ma-profesa wetu mashuhuri, kama wale wa Muhimbili wakijihusisha na upuuzi aliokuwa akiufanya Magufuli juu ya ugonjwa huo.

Itatuchukua muda mwingi sana kurudisha heshima ya elimu yetu kutokana na yaliyotokea kwa muda huo mfupi wa Magufuli.
Maprofesa wamekimbilia kwenye siasa wanaona inalipa kuliko kufanya tafiti, kama darasa la saba wananufaika zaidi kwenye siasa kuliko wao, bora nao wakapambane huko, makosa ya serikali ni kuweka kipaumbele mwenye siasa badala ya taaluma
 
Hiyo sanamu ilikuwa inaeleza jambo katika historia, mlitaka mtu wa history afanye nini? Halafu mlipata ufafanuzi kwa nini hiyo sanamu?

Kuhusu kuamia ndege, kuna kifaa kilishatengenezwa siku nyingi, kinatoa sauti ya mwewe au ya ndege wanaokula ndege wenzao. Ndege wala mazao wakisikia hiyo sauti wanakimbia.

Humu watu wengi hawapo informed. Halafu hawawezi kuchambua na kuelewa mantiki ya kitu.

Innovation ipo katika kila eneo, sio sayansi tu.
 
Mkuu tunafwatilia kwa karibu kila mnachofanya na hatujatoa hukumu kwa maonyesho hayo tuu. Hata kule saba saba hamna jipya.
Kama hatuko informed ni makosa yenu ya kutowasiliana na sisi kutoa hizo taarifa sawasawa.
Unaposema wengi hatuwezi kuchambua umetumia kigezo gani na data ipi? Usituchukulie poa kabisa. Tafiti ziko nyingi hapo hamzisomi mnazunguka na maungo mkisema ni majiko mmebuni. Mmebuni kitu gani wakati hakuna ubunifu unajirudia mara mbili zimekwisha tengenezwa jiko advanced sana za solar mpaka za kutumia maji kama nishati. Hata hilo jiko lenyewe nikija na kande haziiivi. Hebu badilikeni bwana. Pale maji wanashindwa hata kutengeneza kifaa cha kumwagilia maji kusaidia wakulima?
Hapo engineering ni mara ngapi kampuni za nje zinakuja kuwajengea majengo ambayo wao wangekuwa na uwezo wa kuyajenga wenyewe? Wakapata fedha wakaboresha idara zao?
Tunasema kwa machungu maana mengi tunayajua mnafanya vitu chini ya kiwango chenu. Tusipowaambia sisi tuliopita huko nani atasema?
 
Kuhusu swali ulilouliza kwamba mtu wa historia afanye nini? Inaonyesha sanamu hilo ndio ilikuwa mwisho wenu wa kufikiri.
 
Hayo ni mawazo yako. Angeweza kuja na vitu vingi vya kihistoria. Sasa amekuja na hicho mnachokiita sanamu.
 
Mkuu tunafwatilia kwa karibu kila mnachofanya na hatujatoa hukumu kwa maonyesho hayo tuu. Hata kule saba saba hamna jipya.
Kama hatuko informed ni makosa yenu ya kutowasiliana na sisi kutoa hizo taarifa sawasawa.
Unaposema wengi hatuwezi kuchambua umetumia kigezo gani na data ipi? Usituchukulie poa kabisa. Tafiti ziko nyingi hapo hamzisomi mnazunguka na maungo mkisema ni majiko mmebuni. Mmebuni kitu gani wakati hakuna ubunifu unajirudia mara mbili zimekwisha tengenezwa jiko advanced sana za solar mpaka za kutumia maji kama nishati. Hata hilo jiko lenyewe nikija na kande haziiivi. Hebu badilikeni bwana. Pale maji wanashindwa hata kutengeneza kifaa cha kumwagilia maji kusaidia wakulima?
Hapo engineering ni mara ngapi kampuni za nje zinakuja kuwajengea majengo ambayo wao wangekuwa na uwezo wa kuyajenga wenyewe? Wakapata fedha wakaboresha idara zao?
Tunasema kwa machungu maana mengi tunayajua mnafanya vitu chini ya kiwango chenu. Tusipowaambia sisi tuliopita huko nani atasema?
Unafuatilia lakini hauna taarifa. Kuna mashindano yanaitwa Science, Technology, and Innovation kwa kiswahili MAKISATU, ambayo huratibiwa na COSTECH. Kati ya wabunifu bora 10 kitaifa Mwaka huu wa 2021, category ya vyuo vikuu, 5 walitoka UDSM. Wa kwanza katika mashindano hayo yaliyohitimishwa katika viwanja vya Jamhuri Dodoma, alitoka UDSM.
 
Wangetengeneza hata sensor ya kupiga Alam mwizi anapokaribia dirishan,.au ukuta..Mana wez Sasa hv wamekuwa kero
Hizo sensor mbona kuna dogo mmoja wa Arusha ameshazivumbua na zishaanza kutumika kwenye baadhi ya nyumba na shule huko Arusha na alishahojiwa hadi na Millard Ayo! Sasa hivi anasoma chuo South Africa anapiga hela na huku bongo ashawajengea hadi wazazi wake nyumba!
 
Back
Top Bottom