Mkuu Godfather-02
Imenichukuwa muda kiasi kuutafuta mchango wako huu hapa, baada ya kuona jibu ulilopewa na mpuuzi mmoja anayejiita MRUSI, ili na mimi nikupongeze na kuchangia machache juu yake.
Ila katika kuutafuta mchango huu, nikakutana na mwingine uliouweka mwanzo ambao kidogo umenisikitisha.
Kuhusu wazo hili zuri la kuwasaidia wakulima, kusema kweli ni kukosa tu usimamizi mzuri ndani ya nchi yetu, maana hapa ingetakiwa tu kutekeleza. Teknologia tayari ipo kabisa, kinachotakiwa ni kuunda tu hivyo vyombo vya kutosha na kuvisambaza kwa wakulima vifanye kazi.
1. Ni kuweka 'monitors' tu huko shambani, kutambua kuwa ndege wametuwa, hii tayari ipo.
2. Robot lililowekwa huko shambani likishajuwa ndege wametua, linatikisa au kutoa milio kuwafukuza ndege, uwezo huu tayari upo
3. Kinachotakiwa ni 'software' za kuweka tu kwenye hayo maroboti.
4. Internet of things(IoT), tayari itamwezesha mkulima kujua hali shambani kwake ipoje, akitumia 'smartphone'tu yenye uwezo wa kawaida
Sasa, kinachosikitisha kwetu ni huku kujidharau
Kwani kweli hatuwezi kuachana na haya mambo tukafanya mambo yetu kiuhakika zaidi?