Mapadre acheni kuudhalilisha ukatoliki (padre aomba waumini wamchangie milion 90 anunue kluger ya kutembelea

Mapadre acheni kuudhalilisha ukatoliki (padre aomba waumini wamchangie milion 90 anunue kluger ya kutembelea

Zamani mapadre walikuwa wananunuliwa magari na wafadhili wao wa nje.
Miaka ya karibuni kanisa linajitegemea sasa unataka padri apande punda kwenye kuhudumia wanajumuiya na wakristo wa huko vigangoni?
Maisha ya sasa gari sio anasa ni hitaji muhimu kwa mtu mwenye ratiba ya maisha.
Pole mleta mada kwa hali ngumu ya maisha iliyonayo.
Nikukumbushe tu miaka nadhani 2/3 waamini wa jimbo la Kahama walimnunulia askofu wao VXR mpya atembelee na kuwahudumia.
 
Nimeandika kwa masikitiko makubwa sana nikiwa kama muumin kindakindaki mkatoliki

Miezi miwili iliyopita nilijumuika na waumini wenzangu kwenye misa ya asubuh ndani ya kanisa katoliki lililopo maeneo ya saint carol wilayani sengerema jijini Mwanza

Mamia ya waumini tulijumuika kwenye misa hiyo,

Kitu kilichonishangaza kwenye hiyo ibada ni pale padre alipoomba waumini tumchangie pesa kiasi cha milioni 90 kwa ajili ya kununua toyota kluger ya kutembelea

Padre hakuishia hapo bali aliendelea kwa kutoa utaratibu wa namna gani pesa hiyo itapatikana

Alitoa amri kila kigango kimchangie milioni 1 na pesa nyingine alielekeza namna zitakapopatikana infact nilijiskia vibaya sana na kujiuliza hv wakatoliki kweli tumefikia hatua hii?

Leo hii tena tarehe 10 nimeudhulia misa ya asubuh kwenye kanisa lilelile padre aliongea kauli yenye ukakas sana, kwamba baba paroko amemwagiza amchukulie kiasi cha milioni moja ambacho aliwaomba waumin wamchangie akiwa kwenye ibada siku za nyuma zilizopita

Niliposkia kauli hiyo nilitoka ndani ya kanisa na kuondoka zangu

Sasa swali langu linaenda kwa wale viongozi wa juu wa kikatoliki

Kwanini mmetufanya sisi waumini wenu kama major source of income? Au mnataka tusiwe tunakuja kusali?

Haya mambo kwenye ukatoliki yameanza lini mbona mnajidhalilisha

Na hiyo kluger ya milion 90 ni kluger gan au anataka range?

Tena kaongea kabisa kwamba ameongea na wataalam wa magar wakamshaur gar nzur inayofaa kwa mazingira ya kitanzania ni kampuni ya toyota na wakamshaur anunue toyota kluger ambayo wakampatia na bei tsh milion 90 wakatoliki badiliken mnatia aibu
...Kweli, Wanajifhalilisha tu ! [emoji35][emoji35]...

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Walikuwa wanachangia waumini wenzenu wa Ulaya kuja kuhudumia makanisa yenu huku Afrika.
Sasa muhudumie wenyewe parokia zenu.

Tunatoa sadaka kila jpili, tunatoka michango Kibao kila jumapili, tumechangia miradi kama bank ya mkombizi ya kanisa, tumechangia kumbi Kibao za harusi, mashule ta seminary, mahosptili no lakn still hatupumzishwi michango ikiwepo padiri anataka gari jipya.

Kwann wasitoe kweny mishahar yao wajinunulie magari watakayo
 
Huenda wewe ndo umeanza kusikia au kuona Mimi Nina bahasha ya harambee ya kumchangia BabaParoko gari! Nipo kazini nikifika home napiga picha naiweka hapa siogopi mtu Wala nani nikifika nyumbani inapigwa picha inaweka hapa.

Kabla ya harambee WAUMINI walichangishwa Hela na kupewa Gori (kiasi Cha pesa)Kila mtu ambayo ilikuwa 45k. Akaona haitoshi wakasoti watu walio na kazi zao wakatengeneza group wasap wakaweka Gori Tena 100k Kila mtu then Harambe Kwa kuandikiwa barua kabisa na ilifanyika kigangoni.

Ukumbke nyumba tuli mjengea kubwa na ya kisasa kabisa!

Mimi ni Rc lakni Nimeshastuka kitambo naenda mwaka wa7 bila kunusa kanisani uhuni mwingi na utapeli umerudi makanisani.
Sasa viongozi wa kiroho wa namna hiyo ndio wanaudhalilisha ukatoliki

Na hata michango pia imezid kuwa mingi siku hadi siku, yaan imefikia hatua sasa hv ukiwa na 5k unaogopa kwenda kanisani sababu haitoshi hata sadaka
 
Una hakika na hiki ulichoandika hapa?

Tangu miezi miwili iliyopita leo ndio umekumbuka kuanzisha thread sio?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nimeamua kuandika leo hii sababu nimeona kwenye kanisa lilelile limetokea tena la padri kutumwa na baba paroko aje amchukulie milioni moja yake aliyowaomba waumin

Hicho ndicho kilichonikera mpaka niandike

Sababu mara ya kwanza wameomba ml 90 , leo hii hao hao wanadai milion sasa inamaana kwamba mapadri wa kanisa lile ni omba omba
 
Ilikuwa lazima uanzishe uzi kutafuta justification ya irresponsibility yako?
 
Back
Top Bottom