Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...Kweli, Wanajifhalilisha tu ! [emoji35][emoji35]...Nimeandika kwa masikitiko makubwa sana nikiwa kama muumin kindakindaki mkatoliki
Miezi miwili iliyopita nilijumuika na waumini wenzangu kwenye misa ya asubuh ndani ya kanisa katoliki lililopo maeneo ya saint carol wilayani sengerema jijini Mwanza
Mamia ya waumini tulijumuika kwenye misa hiyo,
Kitu kilichonishangaza kwenye hiyo ibada ni pale padre alipoomba waumini tumchangie pesa kiasi cha milioni 90 kwa ajili ya kununua toyota kluger ya kutembelea
Padre hakuishia hapo bali aliendelea kwa kutoa utaratibu wa namna gani pesa hiyo itapatikana
Alitoa amri kila kigango kimchangie milioni 1 na pesa nyingine alielekeza namna zitakapopatikana infact nilijiskia vibaya sana na kujiuliza hv wakatoliki kweli tumefikia hatua hii?
Leo hii tena tarehe 10 nimeudhulia misa ya asubuh kwenye kanisa lilelile padre aliongea kauli yenye ukakas sana, kwamba baba paroko amemwagiza amchukulie kiasi cha milioni moja ambacho aliwaomba waumin wamchangie akiwa kwenye ibada siku za nyuma zilizopita
Niliposkia kauli hiyo nilitoka ndani ya kanisa na kuondoka zangu
Sasa swali langu linaenda kwa wale viongozi wa juu wa kikatoliki
Kwanini mmetufanya sisi waumini wenu kama major source of income? Au mnataka tusiwe tunakuja kusali?
Haya mambo kwenye ukatoliki yameanza lini mbona mnajidhalilisha
Na hiyo kluger ya milion 90 ni kluger gan au anataka range?
Tena kaongea kabisa kwamba ameongea na wataalam wa magar wakamshaur gar nzur inayofaa kwa mazingira ya kitanzania ni kampuni ya toyota na wakamshaur anunue toyota kluger ambayo wakampatia na bei tsh milion 90 wakatoliki badiliken mnatia aibu
...Yesu akiendesha Punda au Farasi ?? SI alikuwa anachapa Lapa akieneza Dini ??Hutaki Padre aendeshe Mkoko mzuri? Waache waumini wamchangie walichonacho Mkuu
Toa Ndugu Toa Ulichonacho [emoji445].
KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Huyo mposa anayejiita nabii sijawahi mwamini na sitokuja mwaminiHamia kwa Mwamposa
Walikuwa wanachangia waumini wenzenu wa Ulaya kuja kuhudumia makanisa yenu huku Afrika.
Sasa muhudumie wenyewe parokia zenu.
Sasa viongozi wa kiroho wa namna hiyo ndio wanaudhalilisha ukatolikiHuenda wewe ndo umeanza kusikia au kuona Mimi Nina bahasha ya harambee ya kumchangia BabaParoko gari! Nipo kazini nikifika home napiga picha naiweka hapa siogopi mtu Wala nani nikifika nyumbani inapigwa picha inaweka hapa.
Kabla ya harambee WAUMINI walichangishwa Hela na kupewa Gori (kiasi Cha pesa)Kila mtu ambayo ilikuwa 45k. Akaona haitoshi wakasoti watu walio na kazi zao wakatengeneza group wasap wakaweka Gori Tena 100k Kila mtu then Harambe Kwa kuandikiwa barua kabisa na ilifanyika kigangoni.
Ukumbke nyumba tuli mjengea kubwa na ya kisasa kabisa!
Mimi ni Rc lakni Nimeshastuka kitambo naenda mwaka wa7 bila kunusa kanisani uhuni mwingi na utapeli umerudi makanisani.
Nimeamua kuandika leo hii sababu nimeona kwenye kanisa lilelile limetokea tena la padri kutumwa na baba paroko aje amchukulie milioni moja yake aliyowaomba wauminUna hakika na hiki ulichoandika hapa?
Tangu miezi miwili iliyopita leo ndio umekumbuka kuanzisha thread sio?!
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app