Hawalipwi mafao yoyote yale ya uzeeni! Ukishapokea Sakramenti ya Upadre, unakuwa umefunga ndoa na kanisa! Utatakiwa kuchunga kondoo wa Bwana maisha yako yote!
Ukizeeka kwa kiwango cha kushindwa kuendesha misa, utaenda kuishi kwenye nyumba maalum kwa ajili ya mapadre wazee. Huko mtapewa huduma zote muhimu. Na ukiumwa, Kanisa litakutibu mwanzo mwisho.
Mapadre hawalipwi mishahara! Isipokuwa tu posho ambayo hulipwa kila mwaka mara moja. Wakati nilipokuwa Mseminari, miaka mingi iliyopita, posho yao ilikuwa ni tsh. Milioni 1.5 kwa mwaka! Bila shaka kwa sasa itakuwa ni zaidi ya hapo.
Mapadre wa zamani walikuwa na wafadhili wao huko Roma - Italy na pia Austria (MIVA), ambao waliwatumia magari ya kutembelea na fedha kwa ajili ya kuanzishia miradi mbalimbali!
Ila kwenye miaka ya katikati kwa 90 na 2000, hawa wafadhili walipungua kwa kiwango kikubwa, na hivyo kufanya baadhi ya maisha ya mapadre kuwa magumu kwa kiasi chake.
NB: maisha ya USEJA ni magumu kwa Mapadri wengi! Maana wanakula vyakula vyenye mafuta, wanga na sukari nyingi! Sasa kinachotokea baada ya hapo, wanakijua wenyewe! Baadhi wanayamudu. Ila wengi yanawashinda.
Naamini ipo siku wataruhusiwa kuoa kama sisi Walei wao.