Mapadri wakizeeka wanapewa mafao ya kujikimu?

Mi swali langu ni hivi kamanda! Mapadri na masista baada ya kustaafu kwao huwa wanaowa/wanaolewa? Au maisha yao yote wanakua single!
mkuu masista na mapadri hawaoi wao wametoa sadaka kitu kitam zaidi wanachokipenda kwa mungu sababu ya kutooa sio kwamba wamezuiwa na mungu hapana sema kazi yao ile unatakiwa ukafanyekazi popote duniani yani kuna kuhama hama sana sasa wangekua na familia ingekua usumbufu imagine miaka ile ya 1900 wanaambiwa waje africa huku namtumbo huko sasa ukiwa na familia inakua mtihani ila kwa maisha ya sasa papa alikua anafikiria kuwaruhusu waoe manake kesi za kula kondoo zimekua nyingi mi nimeishi nao nawafahamu vizuri
 
Mi nijuavyo kwa ufahamu wangu mapadre wa Rc wengi wao huhudumiwa hadi mwisho wa maisha yao,na hakuna watu wanaoishi maisha ufahari kama mapadre,Maisha yao ni raha mustarehe
Maisha ya kutokuwa na watoto,ni maisha ya upweke.
 
Hiyo miradi haipo kila sehemu/Parokia! Wapo Mapadre wengi tu wanaishi aina hiyo ya maisha. Na sikatai hicho ulichokisema.

Na usisahau pia hao Mapadre nao ni binadamu kama sisi. Hivyo wana tabia za ubinafsi, kupigana zewnge/majungu, ukuda, nk.
Sawa makanisa kwani yanajitegemea au miradi iliyopo sehemu inafahamika na shirika taasisi
Lakini mapadre ni wasomi wazuri lazima wawe na mipango mizuri ya maendeleo zaidi ya kukaa na kuongoza misa tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
mkuu kwenye miradi yao hao wasomi wanatumika jamaa wako fiti kwenye kada zote kuna walim madaktari manesi yani kila professional wanazo hadi wengine wanajeshi refer padri wa kanisa la udsm
 
Sawaa Kuna padri mmoja was balangdalali uko kateshi Ni mmbulu Ni tajir haswa aliniambia Ana shamba la miti alifanyia tadhimini akapata milioni Mia nane .na pia alitunga nguruwe Mia mbili akauzaa in short Ana pesa yake nzuri tu cyo za kanisa
 
Sentenso yako ya mwisho ni mbovu!
 
Na masista nao maisha yao yanakuwaje nao wanapofikia umri wa kuzeeka nao wanalipwa nssf ama pssf
Kwanza Masista wao nadhani hufanya mikataba na kanisa kwa hm mda fulani tu na mda ukiisha huwa wanaongeza au wanaachana usista, ila nawao wanapata huduma kama zilezile za mapadre.
 
sikuhizi wanakua nao kwa siri mi nnamjua padri mmoja ana watoto wawili wakubwa tu mtaani
Hahahah ila wanalelewa kimya kimya πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa sijajua kwenye wosia huwa wanatajwa kama watoto wa marehemu au wanakausha?
 
Mkuu unasema "Ipo siku wataruhusiwa kuoa"

Swali langu ni kwamba,

Kwani nani kawakataza kuoa? Je ni sheria ya Mungu au ni binadamu tu ndiye aliyewawekea huo utaratibu?

Nauliza tu kiroho safi ili nijue.
 
Hua wanagewa kiinua mgongo cha alfu 65, redio ya bluetooth na flash na biblia.
 
Mi swali langu ni hivi kamanda! Mapadri na masista baada ya kustaafu kwao huwa wanaowa/wanaolewa? Au maisha yao yote wanakua single!
Kwanza kanisa katoliki mapadre wake hawastafu, ndoa yao na kanisa katoliki ni ya milele, katika kuachana na upadre kuna kuasi au kufukuzwa.
Ila kuhusu masista ninavojua mimi wao mikataba yao ni ya mda, mda ukiisha kama hataki kuendelea na usista, basi ana uhuru wa kuolewa!
 
Sawaa Kuna padri mmoja was balangdalali uko kateshi Ni mmbulu Ni tajir haswa aliniambia Ana shamba la miti alifanyia tadhimini akapata milioni Mia nane .na pia alitunga nguruwe Mia mbili akauzaa in short Ana pesa yake nzuri tu cyo za kanisa
Padre haruhusiwi kuwa na pesa au utajiri wake mwenyewe . Kila alichonacho ni mali ya kanisa
 
Padre haruhusiwi kuwa na pesa au utajiri wake mwenyewe . Kila alichonacho ni mali ya kanisa
Hpana zile Ni Mali zake nadhani yule Musa CYO mrefu atutema upadari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…