NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Mkuu kama tunalinda eneo la maziwa makuu una maanisha nchi zinazopakana na ziwa victoria Sasa pale Rwanda na sisi ule mgogoro wa paka na jk ulikuwa personal!!!?au ni nchi kama NCHI!!?Wafahamu kitu kikiishatengenezwa kama pale Congo DRC basi huwa shida kukirekebisha.
Congo DRC "instability" ni kitu hakiwezi kuondolewa leo au kesho.
Congo DRC ina serikali "kioo" au kiinimacho na kisha kuna serikali zingine kivuli kama mbili au tatu hivi.
Kisha kuna warlords na vikundi mbalimbali vya uasi na wamo pia "arms dealers".
Hawa arms dealers wengi ni "unlisenced" yaani hawana leseni na hawatambuliki na wanaweza kukupatia silaha yoyote ile uoitaka hata latest. kutoka Ukraine.
Usistuke nikikuambia nchi yetu inalinda eneo la maziwa makuu na tunaona na tunafahamu kila kinoendelea kule Congo, ila nasi twafaidika kwa namna kubwa.
Hii pengine ni moja ya sababu nasi twahitaji kiongozi ambae si mgumu sana ili mambo yaendelee.
Ndo maana CCM haiwezi kutoka madarakani kwani kuna wadau wengi wa ndani na nje ya nchi wamejikita humo.
Wakisikia kuna "outsider" wanahamaki na kuingia uoga mkuu.