Mapara A Jazz yawezekana wakawa cheap zaidi kulinganisha na wasanii wengine maarufu kutoka South Africa?

Mapara A Jazz yawezekana wakawa cheap zaidi kulinganisha na wasanii wengine maarufu kutoka South Africa?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Wakali wa hit Amapiano ya John vuli gate (Mapara A Jazz) kwa mtazamo wa kiutafiti yawezekana wakawa ndio kundi cheap na rahisi kupatikana compared na makundi yenye mfanano na wao kutoka bondeni kwa Madiba.

Thamani ya vitu au watu upimwa kwa Sifa mbalimbali ila kubwa ni upekee na upatikanaji wake lakini ikitokea kitu kikawa na ubora pamoja na upekee afu kikawa ni rahisi kupatikana basi pasipo na shaka watu uanza kukichukulia poa kwa maana thamani yake inakuwa ya chini refer mwanamke akiwa mzuri afu kila mwanaume anayemtaka anampata ndivyo anavyozidi kuchukuliwa poa lakini mwanamke akiwa wa kawaida lakini upatikanaji wake ukawa ni mgumu thamani yake inakuwa juu.

Hawa ndugu zetu Mapara A Jazz Bongo imekuwa kama kwao ndani ya kipindi kifupi cha mwaka 2021 washafanya kazi zaidi ya nne na wasanii wa bongoflava kwa observation ya kawaida kabisa utagundua kuwa upatikanaji wao ni simple na hata vigezo na masharti yao yako rafiki kiasi cha kumpa kila msanii fursa ya kufanya nao kazi.

Wasanii waliofanya nao kazi bongo na majina ya kazi zenyewe.
1. Iyo - Diamond Platnumz
2. Ayaya - Rj the Dj ft Lavalava
3. Chawa - Rayvanny ft whozu
4. Na bado - fas Masauti

Ni mtazamo wangu tu.

From northern part of Tanzania.

images (1).jpeg
 
Niliwahi kuwasikiliza kwenye interview moja kwenye kutuo Fulani Cha redio wanasema wamekuja dar kwasababu south Kuna lockdown na hamna show na hawana kitu Cha kuwaingizia kipato Zaid ya mziki. Lkn haimanish kwamba wako cheap inategemea unawalinganisha na nani
 
mkuu hapa nadhani umeshindwa kuunganisha dot, ni hivi kwa asilimia kubwa na nyingi ni kuwa msanii flani akija bongo akifanya kazi na mtu wa kundi flani tegemea kuna watu weng wa kundi hilo watafanya nae kazi ikiwa ni kama fursa kwao. pia lockdown kwao inawanyanyasa sana na inapelekea maisha kuwa na ugumu flani so wanakuwa rahisi kwao kutoka kutafuta tonge nje ya kwao na hii si kuwa ndo kuwa cheap
 
Back
Top Bottom