Mapato ya Mjusi Wetu

Mapato ya Mjusi Wetu

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Posts
16,681
Reaction score
8,241
"TUNATAKA MAPATO YA MJUSI WA TANZANIA AMBAYE YUKO UJERUMANI" - YouTube

1612379154478.png

''WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo itakayopambania maslahi ya Mjusi huyo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu. MAPAMBANO haya yanaungwa mkono na wabunge mbalimbali kutoka katika majimbo ya Tanzania Bara na upande wa Pili wa Zanzibar kwa maslahi mapana ya Taifa. Kwa upande wa Serikali kupitia kwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi amewathibitishia wabunge hawa kuwa serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kuwa taifa linaanza kunufaika kupitia mabaki ya mjusi huyo.''​

Upumbavu na ujinga mtupu kupigania mapato ya mali yako inayohifadhiwa na mtu ambaye sio mali yake.

Kinachotakiwa ni kupambana na kupata Mjusi wetu, arudishwe nyumbani tu. Hapo hakuna mjadala. Kwani inashindikana mabaki ya huyo mjusi kuwekwa katika jumba la makumbusho ya taifa na huko tuweze kupata mapato 100% kutokana na utalii??!;,

Tangu hayo mabaki yachukuliwe na hao Wajerumani miaka 100 iliyopita ni mapato kiasi gani wamepata??, huu ni wakati wetu na sisi tuchukue mjusi wetu kwa ajili ya mapato na kwa ajili ya historia ya nchi yetu na urithi kwa vizazi vyetu.
 
Kama unafikiri kuchukua huyo mjusi ni sawa na kudai deni shauri yako.
 
Kama unafikiri kuchukua huyo mjusi ni sawa na kudai deni shauri yako.

Kudai deni hakuna maana sana kuliko kudai mali inayosababisha hilo deni, kumbuka kwamba hilo deni mnalodai ni sehemu ndogo ya mapato yaliyopatikana kutokana na mapato ya utalii kwa huyo mjusi, sasa ni kwa muda gani utakuwa ukidai hayo madeni ya huyo mjusi kwa kubembeleza??!!, Mjusi ni mali yako na sehemu ya mapato yake unayaomba kwa kubembeleza isitoshe wanaweza wasikupe!!!---- hiyo yote ni ishara kwamba huyo mjusi sio mali yako au humuhitaji sasa kwanini udai pesa kwa kitu usichokihitaji kitu usichojua umuhimu wake kwako??!!, ndiyo maana ninasema kumdai mjusi ni bora sana kuliko kudai chenji (vijisenti) vya huyo mjusi kitu ambacho unaweza kupima uwezo wetu wa kufikiri ulivyokuwa mdogo tunajali pesa kuliko kujali kitu kinachozalisha hizo pesa, tunajali samaki wa kula siku moja badala ya kujali nyavu zinazovua hao samaki kila siku!!.

Akili kubwa ni hii; Tunataka mjusi wetu tumuweke katika National museum na watalii waje kumuona huku kwetu na tuweze kupata pesa, isitoshe sisi na vizazi vyetu tuweze kumuona huyo mjusi kwa macho yetu, huo ni urithi wa taifa letu, hatuna haja ya kuwasujudia Wajerumani waliopora mali zetu.

Warudishe mjusi wetu, hilo ndilo la kupigania sio kupigania vijisenti kwani huo ni ulofa wa akili.
 
Let us be serious kidogo tu. Hebu twende kwenye cost za kumtunza kabla hatujapa kipato.
Ili aendelee kuwa wetu Ni lazima tukubalu kuingia gharama. Naamini tuko tayari

Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!, and you be serious too!!, kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, the time laid burried in the ground surpasses the time since it was unearthed, if at all any preservative treatment is required to keep it last longer, part of the money (tourism fees) collected would be used to serve the purpose the same way Germans do today.
 
Tumeacha kukomaa na hela za Tanzanite,gas,gold,diamond sasa tumeamua kukomaa na hela za mijusi.

Safi sana
 
Tumeacha kukomaa na hela za Tanzanite,gas,gold,diamond sasa tumeamua kukomaa na hela za mijusi.

Safi sana
Tupe mapato basi ya Tanzanite, gas, gold na diamond? Maana soko lake ni open kila mtu anaweza kufanya na twambie nani anatudhulumu vipi na kwa njia gani?
 
Si na sisi tukafanye utafiti tunaweza pata ndugu zake na huyo mjusi.
Lindi ina hazina nyingi sana bado kugunduliwa,
Kwa sasa mninga umeisha tabora unapatikana lindi.
Mbao adimu adimu zinapatikana lindi,
Samaki wakubwa kama gari ndogo ya hiace wanapatikana lindi.
 
Akili kubwa ni hii; Tunataka mjusi wetu tumuweke katika National museum na watalii waje kumuona huku kwetu na tuweze kupata pesa,...
Jamani sijui akili gani? Hao wanasiasa wanaamini kwamba dinosauri wa Berlin inaleta faida? Na wewe unataka mifupa iwekwe hapa ili kuleta pesa ????

Samahani lakini hiyo si mawazo ya mtu mzima. Makumbusho hugharamia pesa, si kuleta faida. Pale Berlin serikali inaingiza pesa mara kwa mara kulipa gharama za makumbusho yake.
Unafikiri makumbusho hapa Dar es Salaam yanaleta faida ya kifedha??? Kiasi gani? Ni kinyume: mapato ya kiingilio ni msaada kupunguza gharama. si chanzo cha faida!

Hasa ukichukua mifupa ile ambayo ni urithi wa Dunia. Unapaswa kuthibiti mwanga na kiwango cha unyevu hewani ili isiharibike. Unahitaji kutunza jengo, mvua isiingie ndani. Unahitaji kuwekeza taa bora, AC, walinzi.... Maana mifupa unayoona kwa kiasi kikibwa ilikuwa vipande-vipande. Timu ya wataalamu ilifanya kazi zaidi ya miaka 10 kuiunganisha. Kiunzi cha Berlin kimeunganishwa kutoka mifupa ya wanyama kadhaa, na sehemu ya mifupa inayoonyehswa si mifupa, ni mifano ya jasi (gypsum). Kiunzi chote kilijengwa upya mara kadhaa, safari ya mwisho 2007 kwa gharama za milioni euro kwa sababu watafiti walitambua kwamba mifupa kadhaa za original bado zilikuwa kwenye ghala (maana wakati ule walibeba tani 250 visukuku!; vingine bado viko kwenye ghala maana gharama za kuvitambua na kuunganisha vyote hadi sasa ! zilishindikana). Pia namna ya kuunganisha vipande vyote imewahi kudhoofika mara kadhaa na kulikuwa na hatari ya kiunzi kuporomoka.

Basi sidhani Wajerumani watakataa kuleta kiunzi Tanzania - kama Tanzania ina nafasi ya kuiwekea. Makumbusho ya Dar hayafai. Lazima kujenga nyumba mpya. n a alazima kupanga makisio kwa gharama za kundesha nyumba mpya maana mapatao hayataingiza gharama zake.

Je unaweza kutaja makumbusho duniani yanayoleta faida ya pesa (faida ya utamaduni, ya elimu ni kitu kingine..)????
 
Upumbavu na ujinga mtupu kupigania mapato ya mali yako inayohifadhiwa na mtu ambaye sio mali yake.

Kinachotakiwa ni kupambana na kupata Mjusi wetu, arudishwe nyumbani tu. Hapo hakuna mjadala. Kwani inashindikana mabaki ya huyo mjusi kuwekwa katika jumba la makumbusho ya taifa na huko tuweze kupata mapato 100% kutokana na utalii??!;,

Tangu hayo mabaki yachukuliwe na hao Wajerumani miaka 100 iliyopita ni mapato kiasi gani wamepata??, huu ni wakati wetu na sisi tuchukue mjusi wetu kwa ajili ya mapato na kwa ajili ya historia ya nchi yetu na urithi kwa vizazi vyetu.
Thanks man for the nice facts.
 
Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!, and you be serious too!!, kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, the time laid burried in the ground surpasses the time since it was unearthed, if at all any preservative treatment is required to keep it last longer, part of the money (tourism fees) collected would be used to serve the purpose the same way Germans do today.
Ngoja niwemkalimani Kidogo😁😁

Ndugu Yetu Mokaze amesema hivi "Inabidi tuwe makini kidogo, kwa sababu hayo mabaki yalikuwa chini ya ardhi karibia miaka elfu iliyopita na yalijitunza yenyewe kupitia njia za asili bila msaada wa mwanadamu.
Kama kutakuwa kuna uhitaji wa utunzaji kwa ajili ya kudumu zaidi basi mapato yanayopatikana kwenye utalii yanatakiwa kutumika kwa ajili ya kumtunza. Kama Wajerumani wanavyofanya sasa hivi."

I have done this bcoz of your nice contribution about this topic Mokaze
 
hapo kuhusu matengenezo ya mwisho ya kiunzi cha Tendaguru pale Berlin. Mnaamini bado hii inaleta faida ya fedha badala ya gharama kubwa?

World's largest dinosaur gets makeover in Berlin​

BERLIN (Reuters Life!) - The world’s largest dinosaur skeleton is busy being fixed, buffed and pampered for the summer opening of an exhibition at Berlin’s natural history museum.
Museum employees work with the model of the skeleton of Brachiosaurus brancai, the largest mounted dinosaur in the world, in Berlin March 23, 2007. REUTERS/Hannibal Hanschke
A team of Canadian specialists are reconstructing the 12.5 meter high (41 feet), 23 meter long Brachiosaurus after the giant herbivore was dismantled three years ago while the museum building was refurbished.
Since then, it has undergone a total makeover, with numerous sections of the skeleton recast in carbon fiber -- a material experts working on the project said was about 100 times lighter than the original fossils.
“All the legs are real, the shoulder and the entire tail is original fossil material” explained Kristian Remes, the scientist in charge of the reconstruction.
“But the slightly smoother parts, like some of the spinal vertebrae are reconstructed. Using modern technology, the dinosaur models are more accurate than ever as well as more elegant”.
The bones of the Brachiosaurus, considered one of the largest dinosaurs to have ever walked the earth, were found in the early 1900s in Tendaguru, a former German colony, in what is now Tanzania.
New techniques being used at the Berlin museum fit metal armatures around the bones, holding them like fingers rather than having to drill through them.
That allows the full weight of 50 ton structure to be propped up by the metal supports, easing the burden on the fossils themselves. Under the new method, individual bones can be removed and studied without dismantling the whole structure.
“Engineering is paramount. The team also has some excellent blacksmiths, artists and carpenters,” said Mike Thom, looking over at a man wearing biker sunglasses and a lycra skull cap, while shaving the dinosaur’s leg with a sander.
Thom said it was the quest to accurately reconstruct the dinosaur, some 150 million years after it existed, which made the challenge so interesting.
By studying fossilized dinosaur tracks, for example, experts now know that the Brachiosaurus’s legs were much closer together than previously thought.
Thanks to the lighter carbon-fiber parts, the legs on the Brachiosaurus skeleton can be closed up without making the structure unstable.

Chanzo World's largest dinosaur gets makeover in Berlin
 
Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!, and you be serious too!!, kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, the time laid burried in the ground surpasses the time since it was unearthed, if at all any preservative treatment is required to keep it last longer, part of the money (tourism fees) collected would be used to serve the purpose the same way Germans do today.
Ndiyo kaka, kutunza mifupa ni kazi kubwa!! Kumbuka mifupa hiyo ilikaa chini ya ardhi kwa miaka milioni (si thousands!) ilikingwa na athira ya hali ya hewa inayoweza kusaga hata mwamba mgumu kuwa mchanga. Haikupaswa kubeba mzigo wowote, na kwa sababu hiyo wamebadilisha sasa sehemu ya kiunz kuwa plastiki ili vipandi vya kiasili visiwe na uzito mkubwa mno - uliokuwa udhaifu wa kiunzi kilichosimamishwa awali.

Halafu ndoto yako ya pesa ni ajabu kweli. Si vile kwamba sehemu ndogo ya kiingilio inalipa utunzwaji na mengine ni faida. Pesa inayopatikana kutoka kwa watalii inasaidia gharama ya utunzaji, ambazo zinahitaji kuongezwa kutoka hela ya umma yaani kutoka mapato ya serikali.
Kote duniani gharama za kuendesha makumbusho ni kubwa kuliko mapato ya kiingilio. Ukiona tofauti, lete mfano tafadhali.
 
Bora abaki huko huko angekua hapa wajinga wangemshukuru mwendazake kwa kusema ndie aliyemleta wakati wa uhai wake
 
Je unaweza kutaja makumbusho duniani yanayoleta faida ya pesa (faida ya utamaduni, ya elimu ni kitu kingine..)????

Usiniulize mimi hilo swali bali muulize mleta mada kwani yeye ndiye anadai kwamba mifupa ya huyo mjusi inaingiza pesa huko ilipo kutoka kwa Watalii wanaoenda kutembelea.

Vyovyote iwavyo, kama hiyo mifupa inaingiza kipato sio lazima ihifadhiwe katika Museum, inaweza kuhifadhiwa popote panapofaa ili isiharibike.

Kama hiyo mifupa ni urithi wa dunia ni vyema lakini la muhimu zaidi hiyo mifupa ni urithi wa Tanzania, ni urithi wako, Wangu na urithi wa kizazi kinachokuja cha Watz, kama unaweza kumuacha mwanao alelewe na jirani (huku akimpatisha faida) na wewe ukaona ni fahari juu ya jambo hilo basi inabidi ukachunguzwe at the top of your ass.

Mzungu hakumbatii kitu kisichokuwa na faida cha kushangaza zaidi kitu hicho sio mali yake!!!----watalii wanapouliza: hii mifupa imefukuliwa nchi gani??, majibu huwa yapi??.
 
Ngoja niwemkalimani Kidogo😁😁

Ndugu Yetu Mokaze amesema hivi "Inabidi tuwe makini kidogo, kwa sababu hayo mabaki yalikuwa chini ya ardhi karibia miaka elfu iliyopita na yalijitunza yenyewe kupitia njia za asili bila msaada wa mwanadamu.
Kama kutakuwa kuna uhitaji wa utunzaji kwa ajili ya kudumu zaidi basi mapato yanayopatikana kwenye utalii yanatakiwa kutumika kwa ajili ya kumtunza. Kama Wajerumani wanavyofanya sasa hivi."

I have done this bcoz of your nice contribution about this topic Mokaze

🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Ndiyo kaka, kutunza mifupa ni kazi kubwa!! Kumbuka mifupa hiyo ilikaa chini ya ardhi kwa miaka milioni (si thousands!) ilikingwa na athira ya hali ya hewa inayoweza kusaga hata mwamba mgumu kuwa mchanga. Haikupaswa kubeba mzigo wowote, na kwa sababu hiyo wamebadilisha sasa sehemu ya kiunz kuwa plastiki ili vipandi vya kiasili visiwe na uzito mkubwa mno - uliokuwa udhaifu wa kiunzi kilichosimamishwa awali.

Halafu ndoto yako ya pesa ni ajabu kweli. Si vile kwamba sehemu ndogo ya kiingilio inalipa utunzwaji na mengine ni faida. Pesa inayopatikana kutoka kwa watalii inasaidia gharama ya utunzaji, ambazo zinahitaji kuongezwa kutoka hela ya umma yaani kutoka mapato ya serikali.
Kote duniani gharama za kuendesha makumbusho ni kubwa kuliko mapato ya kiingilio. Ukiona tofauti, lete mfano tafadhali.

Nakwambia hivi: MIFUPA HIYO NI MALI NA URITHI KWA VIZAZI VYETU, TUNAO WAJIBU WA KULINDA NA KUHIFADHI MALI ZETU ZA ASILI SISI WENYEWE, INAKUAJE MALI YA Tz IHIFADHIWE UJERUMANI???--- mbona (kichwa) fuvu la shujaa Mkwawa mlienda kulichukua kutoka huko???--- hamuoni aibu mbele za uso wa dunia??!!
 
kaka sijui unapinga nini? Nilijibu hoja lako "Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!.. kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, .. if at all any preservative treatment is required to keep it.. part of the money (tourism fees) collected would be used".
Hapa nasema 1) Ndiyo kutunza mifupa ya kale ni kazi kubwa na ghali, 2) tusiwaze maonyesho yake yataleta faida ya kifedha kutokana na kiingilio maana gharama za kutunza ni kubwa kuliko kila kila kiingilio..

Kwa hiyo anayetaka kuirudisha mifupa aseme jinsi atakavyolipa gharama (Kwanza kujenga ukumbi, pamoja na tekinolojia ya AC, usalama na taa, pili kufunza wataalamu wa fani husika, tatu kugharamia uendeshaji endelevu wa makumbusho mapya.)

Nigeria wanapanga sasa kuchukua hizo sanamu ndogo za bronzi zilizoibiwa na Waingereza mjini Benin. Kwa kazi hiyo wametenga mamilioni kujenga makumbusho mapya. Wakiamua kutumia milioni kutoka pesa ya mafuta yao, sawa, (hata kama bado watu wengi sana pale wako maskini na bila huduma - chanzo cha BokoHaram). Na Ujerumani waliamua kuwapa bronzi kutoka Benini zilizonunuliwa na makumbusho ya Ujerumani.
Kwa hiyo sidhani Wajerumani watagoma kurudisha mifupa ya dinosauri. Ila ukiangalia maelezo ya ile kamati ya bunge (video), hawasemi wanataka mifupa, wanasema wanataka asilimia ya mapato.
1619852700140.png

Ambayo naona ni ajabu kidogo ukitaka sehemu ya mapato ya biashara inayoleta hasara. Hao wa pale kama ni wajanja wangejibu je mnataka 50% za hasara ya maonyesho?
Hawatasema, lakini je ingekuwa busara kurudisha mifupa hapa TZ sasa, wakati hakuna mahali pa kuwekea, hakuna wataalamu wanaoweza kuiunganisha na kusimamisha na hakuna pesa ya kuendesha?

Mifupa hii itendewe kama mwendokasi?
 
Back
Top Bottom