Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,241
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
''WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo itakayopambania maslahi ya Mjusi huyo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu. MAPAMBANO haya yanaungwa mkono na wabunge mbalimbali kutoka katika majimbo ya Tanzania Bara na upande wa Pili wa Zanzibar kwa maslahi mapana ya Taifa. Kwa upande wa Serikali kupitia kwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi amewathibitishia wabunge hawa kuwa serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kuwa taifa linaanza kunufaika kupitia mabaki ya mjusi huyo.''
Kama unafikiri kuchukua huyo mjusi ni sawa na kudai deni shauri yako.Upumbavu na ujinga mtupu kupigania mapato ya mali yako inayohifadhiwa na mtu ambaye sio mali yake.
Kinachotakiwa ni kupambana na kupata Mjusi wetu, arudishwe nyumbani tu. Hapo hakuna mjadala. Kwani inashindikana mabaki ya huyo mjusi kuwekwa katika jumba la makumbusho ya taifa na huko tuweze kupata mapato 100% kutokana na utalii??!;,
Tangu hayo mabaki yachukuliwe na hao Wajerumani miaka 100 iliyopita ni mapato kiasi gani wamepata??, huu ni wakati wetu na sisi tuchukue mjusi wetu kwa ajili ya mapato na kwa ajili ya historia ya nchi yetu na urithi kwa vizazi vyetu.
Kama unafikiri kuchukua huyo mjusi ni sawa na kudai deni shauri yako.
Let us be serious kidogo tu. Hebu twende kwenye cost za kumtunza kabla hatujapa kipato.
Ili aendelee kuwa wetu Ni lazima tukubalu kuingia gharama. Naamini tuko tayari
Tupe mapato basi ya Tanzanite, gas, gold na diamond? Maana soko lake ni open kila mtu anaweza kufanya na twambie nani anatudhulumu vipi na kwa njia gani?Tumeacha kukomaa na hela za Tanzanite,gas,gold,diamond sasa tumeamua kukomaa na hela za mijusi.
Safi sana
Jamani sijui akili gani? Hao wanasiasa wanaamini kwamba dinosauri wa Berlin inaleta faida? Na wewe unataka mifupa iwekwe hapa ili kuleta pesa ????Akili kubwa ni hii; Tunataka mjusi wetu tumuweke katika National museum na watalii waje kumuona huku kwetu na tuweze kupata pesa,...
Thanks man for the nice facts.Upumbavu na ujinga mtupu kupigania mapato ya mali yako inayohifadhiwa na mtu ambaye sio mali yake.
Kinachotakiwa ni kupambana na kupata Mjusi wetu, arudishwe nyumbani tu. Hapo hakuna mjadala. Kwani inashindikana mabaki ya huyo mjusi kuwekwa katika jumba la makumbusho ya taifa na huko tuweze kupata mapato 100% kutokana na utalii??!;,
Tangu hayo mabaki yachukuliwe na hao Wajerumani miaka 100 iliyopita ni mapato kiasi gani wamepata??, huu ni wakati wetu na sisi tuchukue mjusi wetu kwa ajili ya mapato na kwa ajili ya historia ya nchi yetu na urithi kwa vizazi vyetu.
Ngoja niwemkalimani Kidogo😁😁Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!, and you be serious too!!, kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, the time laid burried in the ground surpasses the time since it was unearthed, if at all any preservative treatment is required to keep it last longer, part of the money (tourism fees) collected would be used to serve the purpose the same way Germans do today.
Ndiyo kaka, kutunza mifupa ni kazi kubwa!! Kumbuka mifupa hiyo ilikaa chini ya ardhi kwa miaka milioni (si thousands!) ilikingwa na athira ya hali ya hewa inayoweza kusaga hata mwamba mgumu kuwa mchanga. Haikupaswa kubeba mzigo wowote, na kwa sababu hiyo wamebadilisha sasa sehemu ya kiunz kuwa plastiki ili vipandi vya kiasili visiwe na uzito mkubwa mno - uliokuwa udhaifu wa kiunzi kilichosimamishwa awali.Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!, and you be serious too!!, kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, the time laid burried in the ground surpasses the time since it was unearthed, if at all any preservative treatment is required to keep it last longer, part of the money (tourism fees) collected would be used to serve the purpose the same way Germans do today.
Je unaweza kutaja makumbusho duniani yanayoleta faida ya pesa (faida ya utamaduni, ya elimu ni kitu kingine..)????
Ngoja niwemkalimani Kidogo😁😁
Ndugu Yetu Mokaze amesema hivi "Inabidi tuwe makini kidogo, kwa sababu hayo mabaki yalikuwa chini ya ardhi karibia miaka elfu iliyopita na yalijitunza yenyewe kupitia njia za asili bila msaada wa mwanadamu.
Kama kutakuwa kuna uhitaji wa utunzaji kwa ajili ya kudumu zaidi basi mapato yanayopatikana kwenye utalii yanatakiwa kutumika kwa ajili ya kumtunza. Kama Wajerumani wanavyofanya sasa hivi."
I have done this bcoz of your nice contribution about this topic Mokaze
Ndiyo kaka, kutunza mifupa ni kazi kubwa!! Kumbuka mifupa hiyo ilikaa chini ya ardhi kwa miaka milioni (si thousands!) ilikingwa na athira ya hali ya hewa inayoweza kusaga hata mwamba mgumu kuwa mchanga. Haikupaswa kubeba mzigo wowote, na kwa sababu hiyo wamebadilisha sasa sehemu ya kiunz kuwa plastiki ili vipandi vya kiasili visiwe na uzito mkubwa mno - uliokuwa udhaifu wa kiunzi kilichosimamishwa awali.
Halafu ndoto yako ya pesa ni ajabu kweli. Si vile kwamba sehemu ndogo ya kiingilio inalipa utunzwaji na mengine ni faida. Pesa inayopatikana kutoka kwa watalii inasaidia gharama ya utunzaji, ambazo zinahitaji kuongezwa kutoka hela ya umma yaani kutoka mapato ya serikali.
Kote duniani gharama za kuendesha makumbusho ni kubwa kuliko mapato ya kiingilio. Ukiona tofauti, lete mfano tafadhali.
kaka sijui unapinga nini? Nilijibu hoja lako "Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!.. kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, .. if at all any preservative treatment is required to keep it.. part of the money (tourism fees) collected would be used".Nakwambia hivi: MIFUPA HIYO NI MALI NA URITHI KWA VIZAZI VYETU, TUNAO WAJIBU WA KULINDA NA KUHIFADHI MALI ZETU ZA ASILI SISI WENYEWE, INAKUAJE MALI YA Tz IHIFADHIWE UJERUMANI???--- mbona (kichwa) fuvu la shujaa Mkwawa mlienda kulichukua kutoka huko???--- hamuoni aibu mbele za uso wa dunia??!!