One love again
Member
- May 30, 2025
- 47
- 71
Tunaomba mamlaka husika na JamiiForums kutusaidia kufuatilia suala hili. Kwa takribani miaka mitatu sasa, Mwenyekiti na Mtendaji wa Mwime, Manispaa ya Kahama, hawajawahi kuwasilisha taarifa za mapato yanayotokana na mgodi uliopo katika eneo letu.
Wananchi tunaeleza kuwa kila duara linalofika kijijini huwa linatoa mfuko wa maendeleo wa kijiji, lakini mifuko hiyo imekuwa ikichukuliwa bila wananchi kuelezwa matumizi yake. Kutokana na hali hiyo, kijiji cha Mwime kinaendelea kukosa maendeleo muhimu kama soko, barabara bora na madarasa ya kutosha.
Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini mapato hayo yamekuwa yakitumika vipi na wahusika wahojiwe kuhusu fedha za mfuko wa kijiji ambazo hazijawahi kutolewa taarifa zake kwa wananchi.