Mapendekezo: Baraza la Mawaziri

Shida yako ipo wapi?
Uchambuzi wangu kwa sehemu kubwa umelenga elimu ya mtu na uzoefu wake kwenye jambo husika hasa katika Mafanikio.

Udaktari wa Gwajima ndo mana akapendekezwa Wizara ya Afya. Ummy kapendekezwa Tamisemi Kwa sababu Kupitia uzoefu wake na uanasheria wake anaonekana anafaa hapo. Una lingine?
 
Alipiga nini hapo MCL? Tupe ushahidi? Kesi Ilipelekwa wapi na iliamliwaje?
 
Kwa huo uwezo wake wa kushawishi tu Serikali kufanya malipo kupitia bank aliyokuwa anaiongoza inaonesha ni mtu creative atayeweza kutumia mbinu sahihi kuhakikisha anatengeneza tija na faida. That is how business is!

Bank nyingi sana zimeanzishwa lakini hakuna bank iliyoweza ku compete na hao NMB na NBC kama ilivyoweza ku compete CRBD chini ya Kimei. He is a Mogul kwenye sekta ya fedha na Uchumi. Period
 
Wamelivurugaje? Tupe sababu
Makamba na Nape wamelifundisha taifa kuwa wizi ni jambo jema kufanya ili kupata matokeo (goli la mkono).
Mwigulu... ukiacha dharau na hate-speech kuna unyama anaofanya kwenye tozo (Tuendelee kusubiri Singida BigStars ishuke daraja uwaziri ukiisha?)
 
Hivi January Makamba hanaga proffession?
Maana kwingine kote naona umewataja kwa sifa ikiwemo taaluma, Ila kwa huyu mwamba naona Kama umepata kigugumizi[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]

[emoji3]
 
Hujui kitu! Kwa hiyo uchambuzi wako unasema Waziri alichosomea ndiyo akifanyie kazi?? Nani aliyekuambia Waziri ni mtendaji kwenye Wizara husika?? Ningekuona wa manaa sana,kama ungesema Katibu Mkuu awe na Elimu ya kile anachokifanyia kazi! Mfano Katibu Mkuu Afya awe Daktari,Katibu Mkuu Ujenzi awe Mhandisi,Katibu Mkuu Maji awe Mhandisi,Katibu Mkuu Sheria,awe Mwanasheria, Katibu Mkuu fedha awe CPA flani! Katibu Mkuu Madini awe Geologist,Katibu Mkuu Nishati mmoja Mhandisi wa mafuta,na mwingine awe Mhandisi wa Umeme!
 
Tanzania hakujawahi kuwa na mapinduzi makubwa ya uchumi
 
Makatibu Wakuu mostly wana fani ya Taasisi wanazoziongoza. Kusema Waziri asiwe na fani inayohusu Taasisi anayoiongoza au asiwe na uzoefu wa Mafanikio katika jambo fulani inawezekana ndo imetufanya hadi leo Tupo hapa tulipo. Kila siku kupeana lawama kumbe Tatizo hatuna watu sahihi katika nafasi sahihi.

Nimekupa mfano wa Amir Jamal aliyejenga viwanda vingi zaidi na kuanzisha makampuni na mashirika mbalimbali katika kipindi cha Uchumi wa kijamaa only Kwa sababu alikuwa na elimu ya mambo ya Fedha na Uchumi pamoja na uzoefu katika mambo ya biashara.

Ukijua kuwa Baraza la Mawaziri ndo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwenye nchi huwezi kupuuzia hoja kuwa Waziri lazima awe na kitu kama Elimu na uzoefu katika jambo analoliongoza

Kuchagua watu sahihi katika nafasi za Uwaziri kutapeleka kubadilika hadi kwenye aina ya wabunge tunaochagua na kuwapeleka bungeni
 
Alipiga nini hapo MCL? Tupe ushahidi? Kesi Ilipelekwa wapi na iliamliwaje?
Walioiba Tanzania hii wote wako mahakamani?? Juzi Eng Kakonko katia timu na gari la JW huoni kama ni watu wanaojiamini??

Unajua kashifa ya January Makamba kipindi akiwa Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini??

Unajua kina nani walibeba pesa za Tegeta Escrow pale Stanbic kwenye mifuko ya sandarusi?? Unajua nani alikua Waziri wa fedha wa kipindi hicho?? Kipi kilimkuta?? Jifunze!

Unajua kipindi kile Mizengo Pinda akiwa PM alisema yuko tayari kusurubiwa bungeni,lakini hayuko tayari kusema nani mmlimi wa Kagoda Agriculture??? Mifano ni mingi! Jifunze kwanza!
 
Amiri Jamal aliweza kufanya kwenye viwanda na Fedha during the glory days of Tanzania economy Awamu ya Kwanza
Tanzania hakujawahi kuwa na mapinduzi makubwa ya uchumi
 
Nimekwambia tupe ushahidi dhidi ya wizi ya bashe acha maneno maneno
 
Makamba na Nape wamelifundisha taifa kuwa wizi ni jambo jema kufanya ili kupata matokeo (goli la mkono).
Mwigulu... ukiacha dharau na hate-speech kuna unyama anaofanya kwenye tozo (Tuendelee kusubiri Singida BigStars ishuke daraja uwaziri ukiisha?)
Aliiba nini kwenye bao la mkono?
 
Kuna Waziri anayeweza kupinga suala,ambalo Rais atalisema kwenye Baraza la Mawaziri hata kama ni ujinga?? Rejea uuzwaji wa nyumba za serikali kipindi cha Mkapa, Magufuli alisimamia zoezi akiwa Waziri wa Ujenzi,lakini hadi anafariki,hii kitu ilikua inamtafuna kweli kweli,na kama ingekua kwenye democratic countries, Magufuli asingekua Rais wa Tanzania kwa hiyo scandal
 
Tatizo la ncho hii sio aina ya Mawaziri, Hata yesu angeshukankuja kuwa Waziri matatizo yatakuwa pale pale
 
Kwa utalii ni safi sana.anahitajika mtu mwenye exposure na ubunifu kuliko mtu ambae ni hard wired protocol. Ingawa hamis alijarib kuleta ladha tofauf kwaa.kupeleka wale wasaniikupanda mlima haikua sahih wale sio influencers.sasa nan yule mzee wa kulia misiban akapande mlima ili ani motivate mim kweli?? Kwanza hata sijui hata anacho act na sio mpenz wa bongo muv kabisaa.
Utalii unahitaj creativeness kwerikweri.hiv mpaka leo suala la beach Agency sijui limefia kweny makbrasha? Hatu ja utileze beach kabisaaa kabisaa.nchi ndogo ndogo tu ambazo hazina vivutio vingi mfano sycheles ni beach tu zinawatoa.idad ya wagen ni kubwa compared na sehem nyingine.hakuna raia hasa utalii wa ndan asiyependa beach na masuala ya maji maji kama zile water packs.utalii unahitaj maono sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…