Mapendekezo: Baraza la Mawaziri

Mapendekezo: Baraza la Mawaziri

Kama tupo serious na kumpata Waziri wa Fedha imara na tunatapa mabadiliko Wizara hiyo apewe Hussein Bashe-binafsi yangu ndio huwa namuona huwa yupo serious.

Bashe yupo serious na Kazi zake vibaya sana sina uhakika na utaalamu wake wa masuala ya fedha, msikivu na anaingilika
 
Amani iwe nanyi wana bodi.

Hongereni na mapumziko ya mwisho wa wiki.
Leo napenda kutoa uchambuzi wangu kuhusu Baraza la Mawaziri ambalo ninatamani Rais wa Awamu ya 6 aanze nalo kama Baraza lake la kwanza la Mawaziri ambalo linatekeleza Bajeti yake ambayo imetengenezwa yeye akiwa Rais.

Hii ni kwa sababu Rais Samia kwa kipindi chote tangu awe Rais amekuwa alihudumu na Baraza ambalo kiuhalisia ni la mtangulizi wake ambalo alilifanyia mabadiliko madogo tu.

Kwenye Baraza hili uchambuzi wangu utajikita hasa kwenye Wizara huku nikiwataja watu ninaotamani washike wizara hizo na kwa sababu gani?

Kabla ya kuanza uchambuzi wangu naomba nianze kwa kumtaja mtu ambaye inasemwa ndo waziri bora zaidi kuwahi kuhudumu kwenye baraza la Mawaziri la Tanganyika na baadae Tanzania na kwa nini huyu mtu anatajwa kuwa Waziri bora zaidi

Mtu huyu ni Marehemu Amir Jamal ambaye alikuwa waziri wa fedha kuanzia mwaka 1965 na baadae alikuja kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975 na akarudi tena kuwa Waziri wa Fedha kuanzia 1975 mpaka 1977

Ikumbukwe huyu ndo Waziri aliyeongoza Wizara nyeti ambazo zilileta mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa Tanzania katika kipindi chake. Viwanda vingi vilivyojengwa kipindi cha Mwl Nyerere vilijengwa huyu mtu akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha. Kikubwa zaidi aliongoza sera hizi na zikafanikiwa kipindi Tanzania ikiwa nchi ya kijamaa. Unaweza kumuita The mastermind of Tanzania economy

Kwa nini Amir Jamal?
View attachment 2336473

Ikumbukwe Amir Jamal alikuwa na degree ya Masuala ya Fedha na Uchumi kutoka chuo cha Calcuta nchini India. Aliporudi Tanzania ambapo ndo alipozaliwa na kupata elimu ya awali alijihusisha na biashara ikiwemo kusimamia biashara za wazazi wake zilizokuwepo Mkoani Morogoro. Uzoefu huo katika kusimamia biashara za wazazi wake kwa mafanikio ndiko kulikomfanya kuwa Waziri bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania akiongoza Wizara za Fedha pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara

Hivyo uchambuzi wangu wa nani awe Waziri wa Sekta ipi utajikita katika eneo la elimu na uzoefu wa mtu husika kwenye eneo hilo

Mapendekezo yangu
1. Wizara ya Fedha, Charles Kimei na Daniel Sirro
kwa Charles Kimei kila mtu anamjua kama mchumi mahiri aliyetolewa Benki kuu ya Tanzania na kupelekwa kuanzisha Benki ya Wakulima CRDB. Tofauti na matumaini ya wengi mchumi huyu aliweza kuongoza CRDB na kuifanya kutoka kuwa benki ya kawaida kabisa na kuwa benki bora zaidi Tanzania na mpaka kufungua Matawi nje ya nchi. Kwa elimu yake ya PhD ya uchumi na uzoefu wake katika kuongoza Taasisi kwa mafanikio makubwa hana budi kuongoza Taasisi nyeti ya Fedha.

2. Wizara ya Viwanda na Biashara, Shabiby naTarimba Abass
Hawa ni wafanyabiashara wenye uzoefu mkubwa kwenye masuala ya Biashara. Wana biashara zinazofahamika na hata ulipaji wao kodi hautilii mashaka. Wana akili ya utafutaji na uzoefu kwenye utafutaji. Mapendekezo yangu wapewe Wizara ya Viwanda na Biashara

3. Wizara ya Kilimo: Wabaki Bashe na Mavunde. Hii ni kwa sababu wameonyesha wana mawazo chanya na uwezo. Bashe kwa uzoefu wake wa kusimamia biashara hasa kampuni za Rostam ameonyesha ameweza kusimamia kilimo kiwe cha Kibiashara.

4. Wizara ya Afya. Mama Gwajima na Ndugulile watafaa. Uzoefu wao kwenye masuala ya Afya ni muhimu sana. Sekta hii inahitaji sana mjuzi wa sekta. Ummy Mwalimu sio kwamba hafai kuwa Waziri ila Tamisemi itamfaa akisaidiana na Jerry Silaa ambaye nae ameonekana kuwa na uzoefu kutokana na kuwa Diwani na Meya kwa kipindi fulani

5. Wizara ya Katiba na Sheria. Hapa Ndumbaro anaweza kuendelea kutokana na uzoefu wake wa Sheria ila anahitaji Naibu Mwanasheria mwenye uzoefu pia wa masuala ya Sheria. Ridhiwani Kikwete na Abdullah Mwinyi au Joseph Thadayo mbunge wa Mwanga wanaweza kumsaidia kwa sababu kama Wanasheria waliofanya kazi kwenye Law firms kubwa zinazofahamika Tanzania wanaweza kuwa msaada mzuri kwa Waziri wao. Sekta ya Sheria ni sekta nyeti hivyo lazima iwe na waziri na naibu wanasheria

6. Wizara ya Maliasili na Utalii. Nape Mnauye na Toufik Salim Turky wanafaa kuongoza Wizara hii. Nape hana uzoefu kwenye sekta ya Utalii ila ameonesha ana passion na masuala ya utalii kupitia habari. Turkish ni mfanyabiashara ambaye kwa sasa anaongoza biashara za baba yake Zanzibar ikiwemo zile zinazohusiana na masuala ya watalii kama hoteli. Naamini kwa pamoja wataweza kuipeleka sekta hii juu

7. Wizara ya Madini. Sospeter Muhongo na Deo Mwanyika watafaa sana kwenye hii Wizara. Kwa uzoefu wa Muhongo kwenye Madini na uzoefu wa Deo mwanyika ambaye alifikia hadi cheo cha Makamu wa Rais wa Barrik kampuni kubwa inayomiliki migodi mikubwa zaidi Tanzania hakuna namna zaidi ya kuwatumia hawa watu kwenye sekta hii

8. Wizara ya Nishati. January Makamba ameonesha anaweza, nimevutiwa sana na ubunifu wake wa kusisitiza nishati mbadala hasa ya Gesi ambayo kwa hali inavyokwenda hasa mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu mkubwa wa misitu nasisitiza aendelee kuwepo kwenye wizara hii. Kwa Naibu aendelee Byabato

9. Ofisi ya Waziri Mkuu. Waendelee Simbachawene na mwenzake. Wametosha

10. Teknolojia na Habari. Pindi Chana na Zaytun Swai. Pindi Chana ni Mwanasheria ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya Sheria. Uzoefu wake unahitajika sana kwenye kusimamia kanuni na taratibu kwenye sekta ya habari na mawasiliano. kwa zaytun swai huyu ni msomi mahiri kwenye suala la teknolojia aliyesoma shule za vipaji maalum na kuhitimu vizuri degree ya computer science. anafaa kuwa hapa.

11. Makamu wa Rais- Muungano, Mwigulu Nchemba. kwa uzoefu wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama ni dhahiri anazijua vizuri siasa za bara na visiwani. Ni vizuri akawa wizara hii akipewa Naibu yeyote kutoka upande wa Zanzibar

12. Ardhi. Kunambi na Mtemvu. kwa kunambi huyu akiwa Mkurugenzi wa Jiji Dodoma tuliona alivyosimamia vizuri Dodoma kupangwa. Mtemvu pia kupitia michango yake bungeni anaonekana kama mbunge mwenye uelewa mkubwa sana juu ya mipango miji. Ni vizuri wakapewa wizara ya Ardhi ili kwa mara ya kwanza Tanzania tushuhudie mipango miji mizuri na kuondokana na ujenzi holela.

13. Ujenzi na Uchukuzi. Waendelee waliopo. Wameonesha Wanaweza. Pia mambo ya nje ya Ulinzi hazihitaji mabadiliko

14. Maji. Waendelee waliopo kwa kuwa wameonesha wanaweza

Naomba kuwasilisha!
12. Napinga. MH Jaffery Chege wa Rorya anafaa kuwa Waziri wa Ardhi
 
Mkuu,
Sina haja ya kusoma kitabu chochote ili kuelewa ni nani atakuwa rais baada ya uchaguzi mkuu wa 2025!

Sikatai kwamba kuna wawili watatu wanaweza kujotokeza ndani ya CCM na kutaka kuchukuwa fomu za urais. Lakini watakuwa ni wale "choka mbaya". Hata tulikuwa hatujui kama bado wapo hai. Dhumuni lao na wao waonekane.

Lakini hakuna hata mmoja kwenye ili Baraza la Mawaziri au ambao amewatema. Hakadhubutu kuchuana na Samia.
Hata usishangae wagombea kupitia upinzani wakagwaya!
Nakuhakikishia. Samia ni Rais wa JMT 2025-2030. Tutarudi hapa kukumbushana.
 
Duh! Kwamba umependa kupitiliza.

Anyway hata akija mwingine we BADILI GIA angani maana chawa habagui windo.
Mkuu,
Sio kupenda kupitiliza. Jijenge tabia ya kutojidanganya mwenyewe hata kama upendi itakavyokuwa kwenye uchaguzi mkuu 2025. Ni muhimu kwa afya yako ya akili labda kama unafanya siasa kwenye ili.

Again I want to reiterate my question; Ni nani ndani ya CCM au upinzani anaweza kuwa kumwondoa Samia 2025?
 
Akikujibu nitagg
 
Mkuu Lord Denning.

Kwenye wizara ya utalii sikubaliani na wewe.
Wengi waliowahi kuchaguliwa kuiongoza hii wizara hawana uwezo. Ni Lazaro Nyalandu ndio niliona alikuwa anajitaidi kidogo.
Kwa bahati mbaya, wengi wanaogombea ubunge na kushinda. Uwezo wao unaishia kwenye kuwashawishi wabongo lakini nje ya Tanzania wanakuwa domo zege.

Sasa mtu anachaguliwa kuwa Waziri wa Utalii. Yeye kikomo cha uwezo wake kipo kwenye kuchagua bongo muvi au fleva kuwa mabalozi wa Utalii. Sio Jambo baya lakini hiyo ni kuitangaza Tanzania ndani ya Tanzania!

Kwa mtazamo wangu, kuitendea haki hii wizara inabidi rais atumie haki yake kikatiba kumpa mtu ubunge wa viti maalumu na kumpa hii wizara!

Inatakiwa mtu anayeweza kujieleza kwenye TV za uko mbeleni na sio uwezo wake unaishia kumkabidhi Diamond bendera ya Tanzania pale Clouds!

Lakini nao viongozi wa Afrika hawapendi kuona Waziri wake yupo BBC hardtalk au Geographic channels anajielezea. Ni anaona kama anamfunika. Wapo more comfortable na madomo zege nje ya Tanzania. Na sio mtu mwenye uwezo wa kufanya Royal tour part 2!
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana bro,mwenzako kaja na mawazo ww umempinga tuuu bila kutoa mapendekezo yoyote, really?Come on
Mleta mada anawapenda wajinga wa sampuli yako, amekuja na mada amejichanganya haina locus standi, amekosa consistence kwenye maelezo yake, bado wewe unaona amekuja na mawazo?

Nisome nilivyoendelea kumjibu comments zilizofuata uone alivyojichanganya, hajui anasimama wapi; elimu au "mipango".

Mawazo yake ni ya hovyo sana, kwangu hii thread ilitakiwa kufutwa kabisa, akajipange upya kuja na mawazo mengine yaliyonyooka ndio yasomwe halafu itolewe option B kama ikihitajika.
 
Uharibifu wa mazingira unajulikana ndiyo ila nani aliwahi kuchukua hatua kama hizi huko nyuma?

Mtu akifanya vizuri apongezwe na akikosea akosolewe
Hata sioni cha maana ulichonijibu, unaruka ruka tu, uchambuzi wako fake.
 
Hivi January Makamba hanaga proffession?
Maana kwingine kote naona umewataja kwa sifa ikiwemo taaluma, Ila kwa huyu mwamba naona Kama umepata kigugumizi😊😊😊😊😊😊
Huyu katumwa na makamba
 
Mkuu Lord Denning.

Kwenye wizara ya utalii sikubaliani na wewe.
Wengi waliowahi kuchaguliwa kuiongoza hii wizara hawana uwezo. Ni Lazaro Nyalandu ndio niliona alikuwa anajitaidi kidogo.
Kwa bahati mbaya, wengi wanaogombea ubunge na kushinda. Uwezo wao unaishia kwenye kuwashawishi wabongo lakini nje ya Tanzania wanakuwa domo zege.

Sasa mtu anachaguliwa kuwa Waziri wa Utalii. Yeye kikomo cha uwezo wake kipo kwenye kuchagua bongo muvi au fleva kuwa mabalozi wa Utalii. Sio Jambo baya lakini hiyo ni kuitangaza Tanzania ndani ya Tanzania!

Kwa mtazamo wangu, kuitendea haki hii wizara inabidi rais atumie haki yake kikatiba kumpa mtu ubunge wa viti maalumu na kumpa hii wizara!

Inatakiwa mtu anayeweza kujieleza kwenye TV za uko mbeleni na sio uwezo wake unaishia kumkabidhi Diamond bendera ya Tanzania pale Clouds!

Lakini nao viongozi wa Afrika hawapendi kuona Waziri wake yupo BBC hardtalk au Geographic channels anajielezea. Ni anaona kama anamfunika. Wapo more comfortable na madomo zege nje ya Tanzania. Na sio mtu mwenye uwezo wa kufanya Royal tour part 2!
Umesema vyema. Nakubaliana na wewe
 
Mleta mada anawapenda wajinga wa sampuli yako, amekuja na mada amejichanganya haina locus standi, amekosa consistence kwenye maelezo yake, bado wewe unaona amekuja na mawazo?

Nisome nilivyoendelea kumjibu comments zilizofuata uone alivyojichanganya, hajui anasimama wapi; elimu au "mipango".

Mawazo yake ni ya hovyo sana, kwangu hii thread ilitakiwa kufutwa kabisa, akajipange upya kuja na mawazo mengine yaliyonyooka ndio yasomwe halafu itolewe option B kama ikihitajika.
Huna hoja zaidi ya kujaa chuki. Hakuna lolote la maana unaloongea zaidi ya kuonesha chuki tu kwa watu usiowapenda. kama unapinga jambo pinga kwa hoja nzito na sema kwa nini unapinga kwa hoja
 
Huwezi kujiongeza? Aliyekusudiwa ni Abdullah Mwinyi ambaye ni mwanasheria. Hussein Mwinyi ni Daktari by professional
Bado unapuyanga tu!

Ummy Mwalimu ni Mwanasheria by professional,lakini ni Waziri wa Afya! Doroth Gwajima ni Daktari by professional lakini ni Waziri wa maendeleo ya jamii,Makamba kasoma mambo ya conflicts,lakini ni Waziri wa Nishati, Dotto Biteko ni Mwalimu by professional ni Waziri wa Madini! Punguza njaa utaandika na yasiyoandikika! Mtu ni Rais aje kua Naibu Waziri kweli?? Nina njaa kama wewe,lakini njaa yako imenizidi
 
Kama Kimei hafai basi CRDB ingekuwa benki mufilisi sasa
We jamaa reasoning capacity yako ni zero kabisa!

CRDB kwa taarifa yako,ilikua moto sababu ya pesa za serikali nyingi zilikua zinapitia pale! Hadi mishahara ya watu wa serikali ilikua inapita pale,Baada ya Magu kupiga chini CRDB,Kimei akaachia ngazi faster,maana alijua kuna anguko lake linakuja! Sasa hivi NMB kamuacha CRDB mbali sana kwa kila kitu! Punguza njaa!
 
Amani iwe nanyi wana bodi.

Hongereni na mapumziko ya mwisho wa wiki.
Leo napenda kutoa uchambuzi wangu kuhusu Baraza la Mawaziri ambalo ninatamani Rais wa Awamu ya 6 aanze nalo kama Baraza lake la kwanza la Mawaziri ambalo linatekeleza Bajeti yake ambayo imetengenezwa yeye akiwa Rais.

Hii ni kwa sababu Rais Samia kwa kipindi chote tangu awe Rais amekuwa alihudumu na Baraza ambalo kiuhalisia ni la mtangulizi wake ambalo alilifanyia mabadiliko madogo tu.

Kwenye Baraza hili uchambuzi wangu utajikita hasa kwenye Wizara huku nikiwataja watu ninaotamani washike wizara hizo na kwa sababu gani?

Kabla ya kuanza uchambuzi wangu naomba nianze kwa kumtaja mtu ambaye inasemwa ndo waziri bora zaidi kuwahi kuhudumu kwenye baraza la Mawaziri la Tanganyika na baadae Tanzania na kwa nini huyu mtu anatajwa kuwa Waziri bora zaidi

Mtu huyu ni Marehemu Amir Jamal ambaye alikuwa waziri wa fedha kuanzia mwaka 1965 na baadae alikuja kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975 na akarudi tena kuwa Waziri wa Fedha kuanzia 1975 mpaka 1977

Ikumbukwe huyu ndo Waziri aliyeongoza Wizara nyeti ambazo zilileta mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa Tanzania katika kipindi chake. Viwanda vingi vilivyojengwa kipindi cha Mwl Nyerere vilijengwa huyu mtu akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha. Kikubwa zaidi aliongoza sera hizi na zikafanikiwa kipindi Tanzania ikiwa nchi ya kijamaa. Unaweza kumuita The mastermind of Tanzania economy

Kwa nini Amir Jamal?
View attachment 2336473

Ikumbukwe Amir Jamal alikuwa na degree ya Masuala ya Fedha na Uchumi kutoka chuo cha Calcuta nchini India. Aliporudi Tanzania ambapo ndo alipozaliwa na kupata elimu ya awali alijihusisha na biashara ikiwemo kusimamia biashara za wazazi wake zilizokuwepo Mkoani Morogoro. Uzoefu huo katika kusimamia biashara za wazazi wake kwa mafanikio ndiko kulikomfanya kuwa Waziri bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania akiongoza Wizara za Fedha pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara

Hivyo uchambuzi wangu wa nani awe Waziri wa Sekta ipi utajikita katika eneo la elimu na uzoefu wa mtu husika kwenye eneo hilo

Mapendekezo yangu
1. Wizara ya Fedha, Charles Kimei na Daniel Sirro
kwa Charles Kimei kila mtu anamjua kama mchumi mahiri aliyetolewa Benki kuu ya Tanzania na kupelekwa kuanzisha Benki ya Wakulima CRDB. Tofauti na matumaini ya wengi mchumi huyu aliweza kuongoza CRDB na kuifanya kutoka kuwa benki ya kawaida kabisa na kuwa benki bora zaidi Tanzania na mpaka kufungua Matawi nje ya nchi. Kwa elimu yake ya PhD ya uchumi na uzoefu wake katika kuongoza Taasisi kwa mafanikio makubwa hana budi kuongoza Taasisi nyeti ya Fedha.

2. Wizara ya Viwanda na Biashara, Shabiby naTarimba Abass
Hawa ni wafanyabiashara wenye uzoefu mkubwa kwenye masuala ya Biashara. Wana biashara zinazofahamika na hata ulipaji wao kodi hautilii mashaka. Wana akili ya utafutaji na uzoefu kwenye utafutaji. Mapendekezo yangu wapewe Wizara ya Viwanda na Biashara

3. Wizara ya Kilimo: Wabaki Bashe na Mavunde. Hii ni kwa sababu wameonyesha wana mawazo chanya na uwezo. Bashe kwa uzoefu wake wa kusimamia biashara hasa kampuni za Rostam ameonyesha ameweza kusimamia kilimo kiwe cha Kibiashara.

4. Wizara ya Afya. Mama Gwajima na Ndugulile watafaa. Uzoefu wao kwenye masuala ya Afya ni muhimu sana. Sekta hii inahitaji sana mjuzi wa sekta. Ummy Mwalimu sio kwamba hafai kuwa Waziri ila Tamisemi itamfaa akisaidiana na Jerry Silaa ambaye nae ameonekana kuwa na uzoefu kutokana na kuwa Diwani na Meya kwa kipindi fulani

5. Wizara ya Katiba na Sheria. Hapa Ndumbaro anaweza kuendelea kutokana na uzoefu wake wa Sheria ila anahitaji Naibu Mwanasheria mwenye uzoefu pia wa masuala ya Sheria. Ridhiwani Kikwete na Abdullah Mwinyi au Joseph Thadayo mbunge wa Mwanga wanaweza kumsaidia kwa sababu kama Wanasheria waliofanya kazi kwenye Law firms kubwa zinazofahamika Tanzania wanaweza kuwa msaada mzuri kwa Waziri wao. Sekta ya Sheria ni sekta nyeti hivyo lazima iwe na waziri na naibu wanasheria

6. Wizara ya Maliasili na Utalii. Nape Mnauye na Toufik Salim Turky wanafaa kuongoza Wizara hii. Nape hana uzoefu kwenye sekta ya Utalii ila ameonesha ana passion na masuala ya utalii kupitia habari. Turkish ni mfanyabiashara ambaye kwa sasa anaongoza biashara za baba yake Zanzibar ikiwemo zile zinazohusiana na masuala ya watalii kama hoteli. Naamini kwa pamoja wataweza kuipeleka sekta hii juu

7. Wizara ya Madini. Sospeter Muhongo na Deo Mwanyika watafaa sana kwenye hii Wizara. Kwa uzoefu wa Muhongo kwenye Madini na uzoefu wa Deo mwanyika ambaye alifikia hadi cheo cha Makamu wa Rais wa Barrik kampuni kubwa inayomiliki migodi mikubwa zaidi Tanzania hakuna namna zaidi ya kuwatumia hawa watu kwenye sekta hii

8. Wizara ya Nishati. January Makamba ameonesha anaweza, nimevutiwa sana na ubunifu wake wa kusisitiza nishati mbadala hasa ya Gesi ambayo kwa hali inavyokwenda hasa mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu mkubwa wa misitu nasisitiza aendelee kuwepo kwenye wizara hii. Kwa Naibu aendelee Byabato

9. Ofisi ya Waziri Mkuu. Waendelee Simbachawene na mwenzake. Wametosha

10. Teknolojia na Habari. Pindi Chana na Zaytun Swai. Pindi Chana ni Mwanasheria ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya Sheria. Uzoefu wake unahitajika sana kwenye kusimamia kanuni na taratibu kwenye sekta ya habari na mawasiliano. kwa zaytun swai huyu ni msomi mahiri kwenye suala la teknolojia aliyesoma shule za vipaji maalum na kuhitimu vizuri degree ya computer science. anafaa kuwa hapa.

11. Makamu wa Rais- Muungano, Mwigulu Nchemba. kwa uzoefu wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama ni dhahiri anazijua vizuri siasa za bara na visiwani. Ni vizuri akawa wizara hii akipewa Naibu yeyote kutoka upande wa Zanzibar

12. Ardhi. Kunambi na Mtemvu. kwa kunambi huyu akiwa Mkurugenzi wa Jiji Dodoma tuliona alivyosimamia vizuri Dodoma kupangwa. Mtemvu pia kupitia michango yake bungeni anaonekana kama mbunge mwenye uelewa mkubwa sana juu ya mipango miji. Ni vizuri wakapewa wizara ya Ardhi ili kwa mara ya kwanza Tanzania tushuhudie mipango miji mizuri na kuondokana na ujenzi holela.

13. Ujenzi na Uchukuzi. Waendelee waliopo. Wameonesha Wanaweza. Pia mambo ya nje ya Ulinzi hazihitaji mabadiliko

14. Maji. Waendelee waliopo kwa kuwa wameonesha wanaweza

15. Michezo. Mchengerwa na Gekul wamepamudu. Si vibaya wakaendelea. ila pakihitaji mabadiliko Hamis Mwinjuma akiwekwa kumsaidia mchengerwa hasa kwenye kuboresha Sanaa sio vibaya sana

16. Utumishi na Utawala Bora. Jessica kapamudu. sio vibaya akiendelea na Ndejembi ambaye pia anaonekana yuko composed na ana uelewa mzuri wa mambo.

17. Elimu wakiendelea waliopo sio mbaya wana uzoefu na exposure nzuri.

18. Mifugo na uvuvi hapa pasta kichwa. So far sioni mwenye exposure anayeweza kugeuza sekta ya uvuvi kuwa ya kisasa zaidi. Tunahitaji sana mtaalam au mzoefu kwenye masuala ya biashara na uwekezaji ili anyone na kuibadilisha hii sekta. Akitoka nje ya wabunge hawa itapendeza zaidi

Naomba kuwasilisha!
Una haki ya kutoa mawazo yako, ila ulipomtaja Gwajima, nimetilia shaka uchambuzi na uwezo wako.
 
Kama tupo serious na kumpata Waziri wa Fedha imara na tunatapa mabadiliko Wizara hiyo apewe Hussein Bashe-binafsi yangu ndio huwa namuona huwa yupo serious.
Bashe humujui kwa undani! Nimefanya nae kazi MCL! Bashe ni hatari,ni mpigaji mzuri sana! Hizo ni bla bla tu! Nikijana wa Rostam yule! Wizara ya fedha kwa Bashe hapana,atakula hadi basi! Bashe anadunda sababu ya nguvu ya Rostam tu,bila Rostam Bashe angekua huko mavumbini!

Mwaka 2010, kipindi cha Jakaya,kina Jakaya na Makamba Senior,waliwahi sema Bashe sio mtanzania,Masha akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alimuokoa!
 
Back
Top Bottom