Mapendekezo: Baraza la Mawaziri

Mapendekezo: Baraza la Mawaziri

Kuna Waziri anayeweza kupinga suala,ambalo Rais atalisema kwenye Baraza la Mawaziri hata kama ni ujinga?? Rejea uuzwaji wa nyumba za serikali kipindi cha Mkapa, Magufuli alisimamia zoezi akiwa Waziri wa Ujenzi,lakini hadi anafariki,hii kitu ilikua inamtafuna kweli kweli,na kama ingekua kwenye democratic countries, Magufuli asingekua Rais wa Tanzania kwa hiyo scandal
Naamini yupo huyo Waziri na inawezekana. Labda utupe uzoefu wako kama umewai kuingia kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri.

Usisahau kutupa ushahidi wa wizi wa Bashe maana Bado tunausubiri!
 
Sahihi kabisa! Utalii is all about creativeness na exposure!
Kwa utalii ni safi sana.anahitajika mtu mwenye exposure kuliko yule hard wired protocol. Inangawa hamis alijarib kuleta ladha tofauf ola.kupeleka wale kupanda mlima haikua sahih wale sio influencers.sasa nan yule mzee wa kulia misiban akapande mlima ili ani motivate mim kweli?? Kwanza hata sijui hata anacho act na sio mpenz wa bongo muv kabisaa.
Utalii unahitaj creativeness kwerikweri.hiv mpaka leo suala la beach Agency sijui limefia kweny makbrasha? Hatu ja utileze beach kabisaaa kabisaa.nchi ndogo ndogo tu ambazo hazina vivutio vingi mfano sycheles ni beach tu zinawatoa.idad ya wagen ni kubwa compared na sehem nyingine.hakuna raia hasa utalii wa ndan asiyependa beach na masuala ya maji maji kama zile water packs.utalii unahitaj maono sana
 
Aliiba nini kwenye bao la mkono?
Waliiba kura! Wakati wao wakiruhusiwa na "clone tallying center ya matokeo ya NEC", ofisi za UKAWA zilivamiwa na vitendea kazi kchukuliwa.
Wizi ni wizi lakini wizi wa kura za maamuzi ya wananchi ni laana!
 
Weka ushahidi! Usilete maneno ya mtaani
 
Amani iwe nanyi wana bodi.

Hongereni na mapumziko ya mwisho wa wiki.
Leo napenda kutoa uchambuzi wangu kuhusu Baraza la Mawaziri ambalo ninatamani Rais wa Awamu ya 6 aanze nalo kama Baraza lake la kwanza la Mawaziri ambalo linatekeleza Bajeti yake ambayo imetengenezwa yeye akiwa Rais.

Hii ni kwa sababu Rais Samia kwa kipindi chote tangu awe Rais amekuwa alihudumu na Baraza ambalo kiuhalisia ni la mtangulizi wake ambalo alilifanyia mabadiliko madogo tu.

Kwenye Baraza hili uchambuzi wangu utajikita hasa kwenye Wizara huku nikiwataja watu ninaotamani washike wizara hizo na kwa sababu gani?

Kabla ya kuanza uchambuzi wangu naomba nianze kwa kumtaja mtu ambaye inasemwa ndo waziri bora zaidi kuwahi kuhudumu kwenye baraza la Mawaziri la Tanganyika na baadae Tanzania na kwa nini huyu mtu anatajwa kuwa Waziri bora zaidi

Mtu huyu ni Marehemu Amir Jamal ambaye alikuwa waziri wa fedha kuanzia mwaka 1965 na baadae alikuja kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975 na akarudi tena kuwa Waziri wa Fedha kuanzia 1975 mpaka 1977

Ikumbukwe huyu ndo Waziri aliyeongoza Wizara nyeti ambazo zilileta mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa Tanzania katika kipindi chake. Viwanda vingi vilivyojengwa kipindi cha Mwl Nyerere vilijengwa huyu mtu akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha. Kikubwa zaidi aliongoza sera hizi na zikafanikiwa kipindi Tanzania ikiwa nchi ya kijamaa. Unaweza kumuita The mastermind of Tanzania economy

Kwa nini Amir Jamal?
View attachment 2336473

Ikumbukwe Amir Jamal alikuwa na degree ya Masuala ya Fedha na Uchumi kutoka chuo cha Calcuta nchini India. Aliporudi Tanzania ambapo ndo alipozaliwa na kupata elimu ya awali alijihusisha na biashara ikiwemo kusimamia biashara za wazazi wake zilizokuwepo Mkoani Morogoro. Uzoefu huo katika kusimamia biashara za wazazi wake kwa mafanikio ndiko kulikomfanya kuwa Waziri bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania akiongoza Wizara za Fedha pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara

Hivyo uchambuzi wangu wa nani awe Waziri wa Sekta ipi utajikita katika eneo la elimu na uzoefu wa mtu husika kwenye eneo hilo

Mapendekezo yangu
1. Wizara ya Fedha, Charles Kimei na Daniel Sirro
kwa Charles Kimei kila mtu anamjua kama mchumi mahiri aliyetolewa Benki kuu ya Tanzania na kupelekwa kuanzisha Benki ya Wakulima CRDB. Tofauti na matumaini ya wengi mchumi huyu aliweza kuongoza CRDB na kuifanya kutoka kuwa benki ya kawaida kabisa na kuwa benki bora zaidi Tanzania na mpaka kufungua Matawi nje ya nchi. Kwa elimu yake ya PhD ya uchumi na uzoefu wake katika kuongoza Taasisi kwa mafanikio makubwa hana budi kuongoza Taasisi nyeti ya Fedha.

2. Wizara ya Viwanda na Biashara, Shabiby naTarimba Abass
Hawa ni wafanyabiashara wenye uzoefu mkubwa kwenye masuala ya Biashara. Wana biashara zinazofahamika na hata ulipaji wao kodi hautilii mashaka. Wana akili ya utafutaji na uzoefu kwenye utafutaji. Mapendekezo yangu wapewe Wizara ya Viwanda na Biashara

3. Wizara ya Kilimo: Wabaki Bashe na Mavunde. Hii ni kwa sababu wameonyesha wana mawazo chanya na uwezo. Bashe kwa uzoefu wake wa kusimamia biashara hasa kampuni za Rostam ameonyesha ameweza kusimamia kilimo kiwe cha Kibiashara.

4. Wizara ya Afya. Mama Gwajima na Ndugulile watafaa. Uzoefu wao kwenye masuala ya Afya ni muhimu sana. Sekta hii inahitaji sana mjuzi wa sekta. Ummy Mwalimu sio kwamba hafai kuwa Waziri ila Tamisemi itamfaa akisaidiana na Jerry Silaa ambaye nae ameonekana kuwa na uzoefu kutokana na kuwa Diwani na Meya kwa kipindi fulani

5. Wizara ya Katiba na Sheria. Hapa Ndumbaro anaweza kuendelea kutokana na uzoefu wake wa Sheria ila anahitaji Naibu Mwanasheria mwenye uzoefu pia wa masuala ya Sheria. Ridhiwani Kikwete na Abdullah Mwinyi au Joseph Thadayo mbunge wa Mwanga wanaweza kumsaidia kwa sababu kama Wanasheria waliofanya kazi kwenye Law firms kubwa zinazofahamika Tanzania wanaweza kuwa msaada mzuri kwa Waziri wao. Sekta ya Sheria ni sekta nyeti hivyo lazima iwe na waziri na naibu wanasheria

6. Wizara ya Maliasili na Utalii. Nape Mnauye na Toufik Salim Turky wanafaa kuongoza Wizara hii. Nape hana uzoefu kwenye sekta ya Utalii ila ameonesha ana passion na masuala ya utalii kupitia habari. Turkish ni mfanyabiashara ambaye kwa sasa anaongoza biashara za baba yake Zanzibar ikiwemo zile zinazohusiana na masuala ya watalii kama hoteli. Naamini kwa pamoja wataweza kuipeleka sekta hii juu

7. Wizara ya Madini. Sospeter Muhongo na Deo Mwanyika watafaa sana kwenye hii Wizara. Kwa uzoefu wa Muhongo kwenye Madini na uzoefu wa Deo mwanyika ambaye alifikia hadi cheo cha Makamu wa Rais wa Barrik kampuni kubwa inayomiliki migodi mikubwa zaidi Tanzania hakuna namna zaidi ya kuwatumia hawa watu kwenye sekta hii

8. Wizara ya Nishati. January Makamba ameonesha anaweza, nimevutiwa sana na ubunifu wake wa kusisitiza nishati mbadala hasa ya Gesi ambayo kwa hali inavyokwenda hasa mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu mkubwa wa misitu nasisitiza aendelee kuwepo kwenye wizara hii. Kwa Naibu aendelee Byabato

9. Ofisi ya Waziri Mkuu. Waendelee Simbachawene na mwenzake. Wametosha

10. Teknolojia na Habari. Pindi Chana na Zaytun Swai. Pindi Chana ni Mwanasheria ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya Sheria. Uzoefu wake unahitajika sana kwenye kusimamia kanuni na taratibu kwenye sekta ya habari na mawasiliano. kwa zaytun swai huyu ni msomi mahiri kwenye suala la teknolojia aliyesoma shule za vipaji maalum na kuhitimu vizuri degree ya computer science. anafaa kuwa hapa.

11. Makamu wa Rais- Muungano, Mwigulu Nchemba. kwa uzoefu wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama ni dhahiri anazijua vizuri siasa za bara na visiwani. Ni vizuri akawa wizara hii akipewa Naibu yeyote kutoka upande wa Zanzibar

12. Ardhi. Kunambi na Mtemvu. kwa kunambi huyu akiwa Mkurugenzi wa Jiji Dodoma tuliona alivyosimamia vizuri Dodoma kupangwa. Mtemvu pia kupitia michango yake bungeni anaonekana kama mbunge mwenye uelewa mkubwa sana juu ya mipango miji. Ni vizuri wakapewa wizara ya Ardhi ili kwa mara ya kwanza Tanzania tushuhudie mipango miji mizuri na kuondokana na ujenzi holela.

13. Ujenzi na Uchukuzi. Waendelee waliopo. Wameonesha Wanaweza. Pia mambo ya nje ya Ulinzi hazihitaji mabadiliko

14. Maji. Waendelee waliopo kwa kuwa wameonesha wanaweza

15. Michezo. Mchengerwa na Gekul wamepamudu. Si vibaya wakaendelea. ila pakihitaji mabadiliko Hamis Mwinjuma akiwekwa kumsaidia mchengerwa hasa kwenye kuboresha Sanaa sio vibaya sana

16. Utumishi na Utawala Bora. Jessica kapamudu. sio vibaya akiendelea na Ndejembi ambaye pia anaonekana yuko composed na ana uelewa mzuri wa mambo.

17. Elimu wakiendelea waliopo sio mbaya wana uzoefu na exposure nzuri.

18. Mifugo na uvuvi hapa pasta kichwa. So far sioni mwenye exposure anayeweza kugeuza sekta ya uvuvi kuwa ya kisasa zaidi. Tunahitaji sana mtaalam au mzoefu kwenye masuala ya biashara na uwekezaji ili anyone na kuibadilisha hii sekta. Akitoka nje ya wabunge hawa itapendeza zaidi

Naomba kuwasilisha!
Hii ncni wajinga hawataisha na siku wakiisha itakuwa mwishonwa Dunia, Kwa katiba hii unategemea Waziri afanyeje? Kwa hio mnakaaa vijiwe vya kahawa mnadanganyana tatizo ni mawaziri? Kwamba tatizo ni January Makamba au Mwiguru? kwani misiseme tatizo ni katiba? Hao wakina Makamba si kuna mtu wana report kwake? Yeye kama anawataka wewe una shida gani?
 
Wewe u KIPOFU unayedhani unaona.

KIMEI na baadhi ulowataja ktk upofu wako wataingia soon kuinusuru kuzama Kwa JAHAZI.
Kwenye hihii katiba ya sasa? Au mnazungumzia nini? Ficheni ujinga wenu basi
 
Hii ncni wajinga hawataisha na siku wakiisha itakuwa mwishonwa Dunia, Kwa katiba hii unategemea Waziri afanyeje? Kwa hio mnakaaa vijiwe vya kahawa mnadanganyana tatizo ni mawaziri? Kwamba tatizo ni January Makamba au Mwiguru? kwani misiseme tatizo ni katiba? Hao wakina Makamba si kuna mtu wana report kwake? Yeye kama anawataka wewe una shida gani?
Kwa iyo wewe huoni shida kwenye wasimamizi wa sera na watu wanaotoa maamuzi ya mwisho kupitia chombo kinachoitwa baraza la mawaziri?

Basi shida kubwa unayo wewe!
 
Hivi January Makamba hanaga proffession?
Maana kwingine kote naona umewataja kwa sifa ikiwemo taaluma, Ila kwa huyu mwamba naona Kama umepata kigugumizi[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
Kwa katina hii hata ungeweka waziri wa aina hani haisaidii chochote kile, mtaendelea kudanganyana kwamba changamoto za nchi hii ni Mawaziri
 
Amani iwe nanyi wana bodi.

Hongereni na mapumziko ya mwisho wa wiki.
Leo napenda kutoa uchambuzi wangu kuhusu Baraza la Mawaziri ambalo ninatamani Rais wa Awamu ya 6 aanze nalo kama Baraza lake la kwanza la Mawaziri ambalo linatekeleza Bajeti yake ambayo imetengenezwa yeye akiwa Rais.

Hii ni kwa sababu Rais Samia kwa kipindi chote tangu awe Rais amekuwa alihudumu na Baraza ambalo kiuhalisia ni la mtangulizi wake ambalo alilifanyia mabadiliko madogo tu.

Kwenye Baraza hili uchambuzi wangu utajikita hasa kwenye Wizara huku nikiwataja watu ninaotamani washike wizara hizo na kwa sababu gani?

Kabla ya kuanza uchambuzi wangu naomba nianze kwa kumtaja mtu ambaye inasemwa ndo waziri bora zaidi kuwahi kuhudumu kwenye baraza la Mawaziri la Tanganyika na baadae Tanzania na kwa nini huyu mtu anatajwa kuwa Waziri bora zaidi

Mtu huyu ni Marehemu Amir Jamal ambaye alikuwa waziri wa fedha kuanzia mwaka 1965 na baadae alikuja kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975 na akarudi tena kuwa Waziri wa Fedha kuanzia 1975 mpaka 1977

Ikumbukwe huyu ndo Waziri aliyeongoza Wizara nyeti ambazo zilileta mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa Tanzania katika kipindi chake. Viwanda vingi vilivyojengwa kipindi cha Mwl Nyerere vilijengwa huyu mtu akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha. Kikubwa zaidi aliongoza sera hizi na zikafanikiwa kipindi Tanzania ikiwa nchi ya kijamaa. Unaweza kumuita The mastermind of Tanzania economy

Kwa nini Amir Jamal?
View attachment 2336473

Ikumbukwe Amir Jamal alikuwa na degree ya Masuala ya Fedha na Uchumi kutoka chuo cha Calcuta nchini India. Aliporudi Tanzania ambapo ndo alipozaliwa na kupata elimu ya awali alijihusisha na biashara ikiwemo kusimamia biashara za wazazi wake zilizokuwepo Mkoani Morogoro. Uzoefu huo katika kusimamia biashara za wazazi wake kwa mafanikio ndiko kulikomfanya kuwa Waziri bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania akiongoza Wizara za Fedha pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara

Hivyo uchambuzi wangu wa nani awe Waziri wa Sekta ipi utajikita katika eneo la elimu na uzoefu wa mtu husika kwenye eneo hilo

Mapendekezo yangu
1. Wizara ya Fedha, Charles Kimei na Daniel Sirro
kwa Charles Kimei kila mtu anamjua kama mchumi mahiri aliyetolewa Benki kuu ya Tanzania na kupelekwa kuanzisha Benki ya Wakulima CRDB. Tofauti na matumaini ya wengi mchumi huyu aliweza kuongoza CRDB na kuifanya kutoka kuwa benki ya kawaida kabisa na kuwa benki bora zaidi Tanzania na mpaka kufungua Matawi nje ya nchi. Kwa elimu yake ya PhD ya uchumi na uzoefu wake katika kuongoza Taasisi kwa mafanikio makubwa hana budi kuongoza Taasisi nyeti ya Fedha.

2. Wizara ya Viwanda na Biashara, Shabiby naTarimba Abass
Hawa ni wafanyabiashara wenye uzoefu mkubwa kwenye masuala ya Biashara. Wana biashara zinazofahamika na hata ulipaji wao kodi hautilii mashaka. Wana akili ya utafutaji na uzoefu kwenye utafutaji. Mapendekezo yangu wapewe Wizara ya Viwanda na Biashara

3. Wizara ya Kilimo: Wabaki Bashe na Mavunde. Hii ni kwa sababu wameonyesha wana mawazo chanya na uwezo. Bashe kwa uzoefu wake wa kusimamia biashara hasa kampuni za Rostam ameonyesha ameweza kusimamia kilimo kiwe cha Kibiashara.

4. Wizara ya Afya. Mama Gwajima na Ndugulile watafaa. Uzoefu wao kwenye masuala ya Afya ni muhimu sana. Sekta hii inahitaji sana mjuzi wa sekta. Ummy Mwalimu sio kwamba hafai kuwa Waziri ila Tamisemi itamfaa akisaidiana na Jerry Silaa ambaye nae ameonekana kuwa na uzoefu kutokana na kuwa Diwani na Meya kwa kipindi fulani

5. Wizara ya Katiba na Sheria. Hapa Ndumbaro anaweza kuendelea kutokana na uzoefu wake wa Sheria ila anahitaji Naibu Mwanasheria mwenye uzoefu pia wa masuala ya Sheria. Ridhiwani Kikwete na Abdullah Mwinyi au Joseph Thadayo mbunge wa Mwanga wanaweza kumsaidia kwa sababu kama Wanasheria waliofanya kazi kwenye Law firms kubwa zinazofahamika Tanzania wanaweza kuwa msaada mzuri kwa Waziri wao. Sekta ya Sheria ni sekta nyeti hivyo lazima iwe na waziri na naibu wanasheria

6. Wizara ya Maliasili na Utalii. Nape Mnauye na Toufik Salim Turky wanafaa kuongoza Wizara hii. Nape hana uzoefu kwenye sekta ya Utalii ila ameonesha ana passion na masuala ya utalii kupitia habari. Turkish ni mfanyabiashara ambaye kwa sasa anaongoza biashara za baba yake Zanzibar ikiwemo zile zinazohusiana na masuala ya watalii kama hoteli. Naamini kwa pamoja wataweza kuipeleka sekta hii juu

7. Wizara ya Madini. Sospeter Muhongo na Deo Mwanyika watafaa sana kwenye hii Wizara. Kwa uzoefu wa Muhongo kwenye Madini na uzoefu wa Deo mwanyika ambaye alifikia hadi cheo cha Makamu wa Rais wa Barrik kampuni kubwa inayomiliki migodi mikubwa zaidi Tanzania hakuna namna zaidi ya kuwatumia hawa watu kwenye sekta hii

8. Wizara ya Nishati. January Makamba ameonesha anaweza, nimevutiwa sana na ubunifu wake wa kusisitiza nishati mbadala hasa ya Gesi ambayo kwa hali inavyokwenda hasa mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu mkubwa wa misitu nasisitiza aendelee kuwepo kwenye wizara hii. Kwa Naibu aendelee Byabato

9. Ofisi ya Waziri Mkuu. Waendelee Simbachawene na mwenzake. Wametosha

10. Teknolojia na Habari. Pindi Chana na Zaytun Swai. Pindi Chana ni Mwanasheria ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya Sheria. Uzoefu wake unahitajika sana kwenye kusimamia kanuni na taratibu kwenye sekta ya habari na mawasiliano. kwa zaytun swai huyu ni msomi mahiri kwenye suala la teknolojia aliyesoma shule za vipaji maalum na kuhitimu vizuri degree ya computer science. anafaa kuwa hapa.

11. Makamu wa Rais- Muungano, Mwigulu Nchemba. kwa uzoefu wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama ni dhahiri anazijua vizuri siasa za bara na visiwani. Ni vizuri akawa wizara hii akipewa Naibu yeyote kutoka upande wa Zanzibar

12. Ardhi. Kunambi na Mtemvu. kwa kunambi huyu akiwa Mkurugenzi wa Jiji Dodoma tuliona alivyosimamia vizuri Dodoma kupangwa. Mtemvu pia kupitia michango yake bungeni anaonekana kama mbunge mwenye uelewa mkubwa sana juu ya mipango miji. Ni vizuri wakapewa wizara ya Ardhi ili kwa mara ya kwanza Tanzania tushuhudie mipango miji mizuri na kuondokana na ujenzi holela.

13. Ujenzi na Uchukuzi. Waendelee waliopo. Wameonesha Wanaweza. Pia mambo ya nje ya Ulinzi hazihitaji mabadiliko

14. Maji. Waendelee waliopo kwa kuwa wameonesha wanaweza

15. Michezo. Mchengerwa na Gekul wamepamudu. Si vibaya wakaendelea. ila pakihitaji mabadiliko Hamis Mwinjuma akiwekwa kumsaidia mchengerwa hasa kwenye kuboresha Sanaa sio vibaya sana

16. Utumishi na Utawala Bora. Jessica kapamudu. sio vibaya akiendelea na Ndejembi ambaye pia anaonekana yuko composed na ana uelewa mzuri wa mambo.

17. Elimu wakiendelea waliopo sio mbaya wana uzoefu na exposure nzuri.

18. Mifugo na uvuvi hapa pasta kichwa. So far sioni mwenye exposure anayeweza kugeuza sekta ya uvuvi kuwa ya kisasa zaidi. Tunahitaji sana mtaalam au mzoefu kwenye masuala ya biashara na uwekezaji ili anyone na kuibadilisha hii sekta. Akitoka nje ya wabunge hawa itapendeza zaidi

Naomba kuwasilisha!
Stupidity thread
 
Kama Kimei hafai basi CRDB ingekuwa benki mufilisi sasa
Crdb na kuendesha nchi viko sawa? Nyie hizi akili za kipimbi mnazitoa wapi? Hii ncho ina vilaza sana eti, Kwa akili zako unaona mtu anaye manage vyema kampuni basi anaweza simamia Serikali?/ kwa katiba ipi? Acheni ujinga komaeni mpate katiba mpya,
 
Elewa jambo, uhuru wa kiutendaji aliokuwa nao Kimei akiwa CRDB hauna uhusiano na utendaji wa Kimei atakapokuwa waziri, kwenye uwaziri Kimei wa CRDB atakuwa mwingine.

Usishangae mkianza kumlaumu kwamba hajui wakati tatizo sio lake, tatizo ni mazoea yaliyojengwa kwa watawala kuwa ndio wenye last say, hata kama akiwa na maono hafifu.
Hii nchi hata Mungu akaja kuwa Waziri still bado matatizo yatakuwa pale pale,
 
Apewe tuone. Hayo mengine ni ramli tu
Nyie wajinga sikilizeni Mataifa mengine Waziri anaenda kusimamia Sera za nchi na si mawazo yake, hakuna nchi ambauo waziri eti anaenda ku implement mawazo yake pale, nyie komaeni mpate katiba mpya, hizi ngonjera hazisaidii kitu
 
Unasemaje ramli wakati tumeshaona mifano mingi tu, siku hizi elimu ya waziri haina uhusiano na wizara atakayopewa, na hata kama ikiwa na uhusiano huo, bado hatakuwa huru kuitumia elimu yake 100% kwenye utendaji wake mpaka ajue mtazamo wa bosi wake kwenye jambo husika.
Hii nchi shisa sio Mawaziri, kuna wajinha wanazami Mwihuru ndio Tatizo, kwani Mwiguru kafanya mapinduzi nankuwa Waziri wa pesa?
 
Nakupa mfano
Kuna kongamano la Madini. Wamealikwa mawaziri kutoka maeneo mbalimbali wanazungumzia changamoto kwenye kupata teknolojia sahihi kwenye masuala ya miamba. Tunapeleka waziri asiye hata na idea yq miamba kwenye kongamano au majadiliano hayo tutapata kitu?

Au watu wanajadili changamoto za kisheria kwenye masuala ya uwekezaji unampeleka mtu asiyejua hata abc za company law au masuala ya kusafirisha watuhumia mtu hajui hata sheria za kusafirisha watuhumiwa zikoje hapo unategemea kupata nini?
Maraisi waanavyo enda kwenye kongamano la uchumi huwa ni wachumi? Hivi kwa akili yako unaamini shida ya hii nchi ni mawaziri? Huyo bosi wao mbona humsemi? Awamu iliopita Mkuu wa nchi si alikuwa ndio Waziri wa kila wizara unasemaje hapo?
 
Kikwete ndio kakutuma uje kupost huu upuuzi?

Serikali hii inatakiwa ipitishe katiba mpya ile ya warioba halafu ijiuzulu mara moja uchaguzi uitishwe ili nchi ipate viongozi halali.
Huyu ni mjinga, na wajinga wenzake humu watamuina kayoa hoja za maana
 
Crdb na kuendesha nchi viko sawa? Nyie hizi akili za kipimbi mnazitoa wapi? Hii ncho ina vilaza sana eti, Kwa akili zako unaona mtu anaye manage vyema kampuni basi anaweza simamia Serikali?/ kwa katiba ipi? Acheni ujinga komaeni mpate katiba mpya,
Sasa ulitaka awe na uzoefu wa kuendesha nchi? Una akili wewe?
 
Back
Top Bottom