KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Zamani zilikuwa ni department chini ya wizara ya fedha, Kuna tofauti kubwa kati ya department (idara) na authority (mamlaka)Zamani ilikuwa hivyo.
Ila matakwa ya wahisani kwa nchi zetu za kiafrica ndio ikaundwa TRA, kenya ikaundwa KRA, zambia ikaundwa ZRA na nchi zinginezo.
TRA imeundwa miaka ya 1996 hivi.
Zamani zilikuwa ni department chini ya wizara ya fedha, Kuna tofauti kubwa kati ya department (idara) na authority (mamlaka)
Kukiwa na mamlaka ya mapato ya nje ,mamlaka hii ihusike na masuala yote ya kikodi ya bidhaa au huduma zinazotoka( import) na zinazokwenda (export) nje. Kukiwa na udhibiti mzuri wa Kodi kutoka nje inawezekana kabisa tatizo la kuhadimika Kwa Dola litakuwa historiaUna wazo zuri lakini swali la kujiuliza tuna uza kipi nje wakati hadi toothpick tunaagiza kutoka nje ndugu ....... eb nipe mawazo
kirefu Cha TRS tafadhali
Hakutakuwa na kuongeza Kodi bali kuwa na udhibiti mzuri na mkubwa wa Kodi zitokanazo na export na import.Mapato yanatokana na kodi, ukisema uweke kodi kubwa kwenye kupeleka bidhaa nje, unakuwa unaua wajasiriamali wako.
Kwa mazingira hayo, kuanzisha hiyo idara inaweza ikashindwa kujiendesha; lasivyo waweke kodi kubwa itakayoua viwanda n.k
Taasisi ili isiwe mzigo kwa serikali, inatakiwa iweze kujiendesha; kwa mazingira hayo, huoni kama unaongeza tatizo?Hakutakuwa na kuongeza Kodi bali kuwa na udhibiti mzuri na mkubwa wa Kodi zitokanazo na export na import.
Ninapozungumzia Mapato ya nje namaanisha mapato yatokanayo na import na export ,na hapa yanaingia mambo yote ya bandari na mipaka Sasa nambie ukusanyaji wa Kodi bandarini na mipakani mamlaka itajiendesha Kwa hasara? Mind you bandari inachangia 37 % ya bajeti Kwa mwaka. Usifanye mchezo kabisa na mapato ya nje kama yatasimiwa vizuri basi itachangia hata 67 ya bajeti na Hilo ni jukumu la TRATaasisi ili isiwe mzigo kwa serikali, inatakiwa iweze kujiendesha; kwa mazingira hayo, huoni kama unaongeza tatizo?
Tumeona mabadiliko yalifanywa katika wizara au mamlaka ya kupunguza ukubwa wa taasisi au wizara ili kuleta tija na ufanisi.
Tumeona wizara iliyokuwa nishati ya nishati na madini ikigawanywa katika wizara ya nishati na wizara ya madini, iliyokuwa wizara ya ujenzi na uchukuzi ikigawanywa katika wizara ya uchukuzi na wizara ya ujenzi na kwa upande wa mamlaka iliyokuwa mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu na majini ikigawanywa kama LATRA(Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini ) na TASAC( ikihusika na udhibiti wa majini).
Ninapendekeza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) igawanywe na kuwa Mamlaka ya mapato ya ndani na mamlaka ya mapato ya nje for better performance.