Mapendekezo: For better performance, TRA igawanywe zipatikane mamlaka mbili, Mamlaka ya mapato ya ndani na mamlaka ya mapato ya nje

Mapendekezo: For better performance, TRA igawanywe zipatikane mamlaka mbili, Mamlaka ya mapato ya ndani na mamlaka ya mapato ya nje

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Tumeona mabadiliko yalifanywa katika wizara au mamlaka ya kupunguza ukubwa wa taasisi au wizara ili kuleta tija na ufanisi.

Tumeona wizara iliyokuwa nishati ya nishati na madini ikigawanywa katika wizara ya nishati na wizara ya madini, iliyokuwa wizara ya ujenzi na uchukuzi ikigawanywa katika wizara ya uchukuzi na wizara ya ujenzi na kwa upande wa mamlaka iliyokuwa mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu na majini ikigawanywa kama LATRA(Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini ) na TASAC( ikihusika na udhibiti wa majini).

Ninapendekeza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) igawanywe na kuwa Mamlaka ya mapato ya ndani na mamlaka ya mapato ya nje for better performance.
 
Zamani ilikuwa hivyo.

Ila matakwa ya wahisani kwa nchi zetu za kiafrica ndio ikaundwa TRA, kenya ikaundwa KRA, zambia ikaundwa ZRA na nchi zinginezo.

TRA imeundwa miaka ya 1996 hivi.
 
... kwa kipi mnachouza nje hadi kuwe na mamlaka ya mapato ya nje? Mmeua viwanda, mmeua kilimo, mmeua ufugaji, hayo mapato yatokanayo na export yako wapi? CCM ni janga!
 
Zamani ilikuwa hivyo.

Ila matakwa ya wahisani kwa nchi zetu za kiafrica ndio ikaundwa TRA, kenya ikaundwa KRA, zambia ikaundwa ZRA na nchi zinginezo.

TRA imeundwa miaka ya 1996 hivi.
Zamani zilikuwa ni department chini ya wizara ya fedha, Kuna tofauti kubwa kati ya department (idara) na authority (mamlaka)
 
Una wazo zuri lakini swali la kujiuliza tuna uza kipi nje wakati hadi toothpick tunaagiza kutoka nje ndugu ....... eb nipe mawazo
 
Zamani zilikuwa ni department chini ya wizara ya fedha, Kuna tofauti kubwa kati ya department (idara) na authority (mamlaka)

Hizi mambo tunafanya kwa kufata matakwa ya wahisani wetu.

Nchi zote zinazotuzunguka.. wanatumia mamlaka ya kodi moja.. mfano ZRA, URA, KRA etc
 
Mapato yanatokana na kodi, ukisema uweke kodi kubwa kwenye kupeleka bidhaa nje, unakuwa unaua wajasiriamali wako.
Kwa mazingira hayo, kuanzisha hiyo idara inaweza ikashindwa kujiendesha; lasivyo waweke kodi kubwa itakayoua viwanda n.k​
 
Si ndio tunaongeza miutitiri ya vitengo tunavyo omba usiku kucha viunganishwe, mtu utajiwe bill ulipe wao ndo watajua wanagwanaje
 
Una wazo zuri lakini swali la kujiuliza tuna uza kipi nje wakati hadi toothpick tunaagiza kutoka nje ndugu ....... eb nipe mawazo
Kukiwa na mamlaka ya mapato ya nje ,mamlaka hii ihusike na masuala yote ya kikodi ya bidhaa au huduma zinazotoka( import) na zinazokwenda (export) nje. Kukiwa na udhibiti mzuri wa Kodi kutoka nje inawezekana kabisa tatizo la kuhadimika Kwa Dola litakuwa historia
 
Mapato yanatokana na kodi, ukisema uweke kodi kubwa kwenye kupeleka bidhaa nje, unakuwa unaua wajasiriamali wako.
Kwa mazingira hayo, kuanzisha hiyo idara inaweza ikashindwa kujiendesha; lasivyo waweke kodi kubwa itakayoua viwanda n.k​
Hakutakuwa na kuongeza Kodi bali kuwa na udhibiti mzuri na mkubwa wa Kodi zitokanazo na export na import.
 
Hakutakuwa na kuongeza Kodi bali kuwa na udhibiti mzuri na mkubwa wa Kodi zitokanazo na export na import.
Taasisi ili isiwe mzigo kwa serikali, inatakiwa iweze kujiendesha; kwa mazingira hayo, huoni kama unaongeza tatizo?
 
Taasisi ili isiwe mzigo kwa serikali, inatakiwa iweze kujiendesha; kwa mazingira hayo, huoni kama unaongeza tatizo?
Ninapozungumzia Mapato ya nje namaanisha mapato yatokanayo na import na export ,na hapa yanaingia mambo yote ya bandari na mipaka Sasa nambie ukusanyaji wa Kodi bandarini na mipakani mamlaka itajiendesha Kwa hasara? Mind you bandari inachangia 37 % ya bajeti Kwa mwaka. Usifanye mchezo kabisa na mapato ya nje kama yatasimiwa vizuri basi itachangia hata 67 ya bajeti na Hilo ni jukumu la TRA
 
Tumeona mabadiliko yalifanywa katika wizara au mamlaka ya kupunguza ukubwa wa taasisi au wizara ili kuleta tija na ufanisi.

Tumeona wizara iliyokuwa nishati ya nishati na madini ikigawanywa katika wizara ya nishati na wizara ya madini, iliyokuwa wizara ya ujenzi na uchukuzi ikigawanywa katika wizara ya uchukuzi na wizara ya ujenzi na kwa upande wa mamlaka iliyokuwa mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu na majini ikigawanywa kama LATRA(Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini ) na TASAC( ikihusika na udhibiti wa majini).

Ninapendekeza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) igawanywe na kuwa Mamlaka ya mapato ya ndani na mamlaka ya mapato ya nje for better performance.

Mtoa mada naona umekuja na wazo linalotakiwa kuangaliwa vizuri ila labda tuchambue hoja hii kwanza

1: Labda tusaidie kuona kwa mfumo uliopo sasa unashida gani ili tupime na kujadili kwa upana. Kwa ufahamu wangu Mamlaka zinazosimamia Kodi ni moja na ukiangalia hata wenzetu waliotuzunguka sheria wana Mamlaka moja.

2: Pili ikumbuskwe kuna sheria mbalimbali zinazofanya nchi kama Tanzania kupata unafuu wa bidhaa zake kuvuka nchi nyingine , hivo ukiwa na Mamlaka mbili kunaweza changia mgongano au ucheleweshaji wa katika hili.

3: Pia garama kuendesha taasisi mbili itakuwa ni kubwa sana na ukiangalia kanchi ketu bado uchumi siyo imara hivo ni kuongeza mzigo kwa wananchi au walipakodi. Maana kutahitajika viongozi mbalimbali kama kamishna mkuu n.k.

4: Mpaka sasa naamini TRA watakuwa wameshajenga mifumo sasa wakijitenga na kuwa taasisi mbili kutakuwa na changamoto ya kuanza upya kujenga mfumo wa kila taasisi na ikaletea baadhi ya taarifa kupotea wadau wa ICT wanaweza nisaidia hili.

5: Pia chukulia mzigo umetoka labda bandarini badala ya kwenda transit unakwamba mtaani umeshaanza uzwa je hapo huoni kutakuwa na kutunishiana misuli kati ya TRA Customs na TRA Domestic? maana kila mmoja atakuwa anataka kodi yake.
 
Back
Top Bottom