Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Nianze kwa kuhoji; Hivi mmegundua kwanini ktk maeneo ya taasisi za Umma kuna katazo "HURUHUSIWI KUPIGA PICHA".
Na mnaweza kujiuliza kuna uhusiano gani, wateule wanapokula kiapo cha uamijifu husema "Sitotoa nje siri za Serikali."
Serikali ni sisi wananchi kwa kuwa tumeiweka madarakani.
Bila shaka siri za serikali ni ule uovu unaofanywa na watendaji kutokana na urasimu uliopo.
Urasimu ni hali au tabia ya maafisa wasimamizi wa taasisi kubwa za umma kutunga sera za utawala na kuzisimamia bila kujali madhara kwa upande wa walaji na hivyo hupelekea mateso, manyanyaso, kukosa haki za msingi au kucheleweshewa.
kazi kubwa ya serikali ni mbili. Kuyalinda au kuyadhibiti na kukandamiza makundi ya jamii.
Fikiria kundi la wagonjwa wa saratani, anaohitaji kuendelea kutapa tiba, lakini hospitali ya umma imeweka taratibu (urasimu) unamzuia mgonjwa kutoendelea kupata tiba wakati mgonjwa huyo hana uwezo.
Mfano ni huyu bibi yuko kizuizini Muhimbili; huyu kamaliza tiba na madaktari wamempa ruhusa arudi nyumbani akajiangalizie kabla ya kuendelea na tiba. Lakini idara ya ustawi wa jamii imemzuia hadi alipe deni analodaiwa.
Somo la kwanza tunalopata ni kuwa madaktari na wauguzi hawahusiki ktk uovu huu, na niwapongeze madaktari na wauguzi. Wanajitahidi kutimiza wajibu wao katika mazingira magumu kabisa.
Changamoto ya Muhimbili ni maafisa wa ustawi wa jamii.
Picha hii nimepiga kwa siri kwa idhini ya mgonjwa akitaka msaada kwa wenye mamlaka ili aruhusiwe kurudi nyumbani. Anahuzuni kubwa, anahisi yupo kwenye mateso kwa kuwa hata uhakika wa kupata chakula hana. Kwa kuwa ndugu wanaomuuguza ni wanashindwa kuja kila siku kutokana na ukata, dada zake ni wawili ambao nao ni watu wazima kama yeye ambao wenyewe hawakumbuki mwaka waliozaliwa. Lkn ukiwaangalia wana miaka zaidi ya 70.
Urasimu umesababisha Muhimbi kutotoa chaluka cha bure kwa wagonjwa. Au kama kipo kinatolewa kwa misingi ya ubaguzi.
Bibi huyu anategemea uji asubuhi katoka kwa taasisi ya kidini ya JAI wanaojitolea kutoa msaada wa uji na usafi kwa wenye uhitaji. Au apite msamaria amwachie pesa aagizie.
Juzi tar 13 ilikuwa ni zaidi ya siku 25 toka aruhusiwe lkn kabaki ktk zuio mpaka alipe deni lake.
Bila ya shaka hii ni moja ya Siri ambazo wenye mamlaka hawapendi umma ufahamishwe. Ingawa wangeacha huru umma ufahamu pengine ingepatikana suluhisho. Badala yake huthibiti wakimini kuficha tatizo ni moja ya njia ya kuondoa tatizo.
Changamoto hii ni kubwa ambapo mtu mmoja pekee hawezi tatua.
Kwa mujibu wa maafisa wa ustawi wa jamii ni kuwa hili ni agizo katika juu wanalazimisha muhimbili ijitegemee kujiendesha kama ambavyo hospitali za binafsi zinavyoweza kujiendesha.
Napendekeza iundwe tume kufatilia urasimu uliopo Muhimbili unaopelekea wagonjwa kukosa haki zao kwa mujibu wa taaluma ya kidaktari.
Haki hizo ni pamoja na upendo, utu, huruma, uadilifu na ihsani.
Binafsi nina mgonjwa mwenye dalili za saratani lakini anakosa haki yake ya kuendelea na matibabu kwa kuwa anadeni. Na yeye hana uwezo.
Kwa haraka kama ningeulizwa suluhisho la muda mrefu la changamoto hii, ninhependekeza kuifuta wizara nzima ya ustawi wa jamii. Kwani kwa uchunguzi mdogo nilioufanya niegundua kuwa Muhimbili inahitaji 5bila kwa mwaka ili iweze kutoa tiba bure kwa wenye saratani muhimbili, na inahijati 100bil kwa ajili ya kitabu bure wagonjwa wote wanaofika muhimbili. Bajeti hii ni ndogo sana ukilingamisha na bajeti ya wizara ya ustawi wa jamii ambayo kimsingi ni mzigo kwetu sisi wananchi.
Nimeamua kulifikisha hili kwa Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili ili nijivue dhima kwa niliyoyashuhudilia Muhimbili na ikishindikana nitamwandika barua ya wazi kwa mamlaka iliyomteua ili kujivua dhima hii.
Wito kwa jamii tujadili kwa nia ya kushinikiza mwenye nchi asiwaangalie wanasiasa na uchaguzi pekee na kuwasahau walio na sauti.
Kwa watakaohitaji kumpa masada unaweza kutumia namba hii na utaongea na dada wa mgonjwa Khadija Abdallah Kadondola 0719639246