Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mkuu upo sahihi kabisaaa.Waambie wapinzani wenzio kuwa bibi huyu ikimuuliza juu ya katiba mpya haelewi chcht.
Bibi huyu angewaelewa iwapo mngepigania maslahi ya wananchi.
Na kupigania mnapaswa kuanza leo. Binafsi ukiitisha maandamano ya kupigania kupewa matibabu bure kwa wagonjwa wenye magonjwa dume kama vile saratani, figo nitashiriki. Lkn sitoshiriki kwa kupigania katiba mpya
Ukiitisha maandamano ya kutetea wamachinga kujengewa maeneo rafiki kwa biashara zao nitashiriki lkn sitoshiriki kwa kupigania tume huru.
Lengo la msingi ni bibi yetu huyo na wananchi aina hiyo kuanza kupata haki zao za kimsingi za kuhudumiwa kama ambavyo matarajio yao yalivyo.
Pia naamini kuwa hatua ya kuweka uzi ni kusimama upande wao naamini lengo halikuwa kuamsha hisia za kisiasa kwenye hili jambo.
Mimi nilisoma maoni yote juu yangu nikaona kila kitu kimeandikwa hadi sehemu ya mawazo niliyotaka kusema. Lakini nikakumbuka ilani ya chama changu CCM imeelekeza jambo muhimu la utoaji wa afya na hususani wazee kuzingatiwa kwenye huduma na ule mfumo wa bima ya afya kwa wote vimesawiri hilo.
Hili jambo linashawishi ushawishi ndani ya tafakuri kuwa, utekelezaji wa ilani ya CCM ni jambo ambalo kamwe haliwezekani kwani hali hiyo hapo hospitali ni matokeo ya uvurundwaji wa kusimamia huduma za afya. Hapo Ustawi wa Jamii wanasubiri tamko la Waziri au Rais waweze kumpa bibi yetu na wwtu wemgine ambao wamewaweka vizuizini kwenye hospitali zetu.
Nimeweka maoni yangu huru kuwa huu ukatili dhidi ya binadamu unafanyika bila hata kustuka ni kwa ssbabu CCM ipo bize kukopa na kugawana hiyo mikopo badala ya kuipeleka kufanyakazi iliyokusudiwa.
Hivi unamzuia mama mzee hospitali na hamumpi chakula. Hauoni kama hao ni wauaji?
My opinion based on such