Sidhani kama kuna mahala katika mada nimesema aanzishe vya kwake.
Bali nimesema aubadilishe mkoa, auendeleze na aufanye kuwa ni mkoa wenye tija zaidi kiuchumi.
Zamani alikuwepo mzee marehemu Lawrence Gama, huyu mzee alikuwa na maono sana kama kiongozi na kila mkoa alokwenda alihakikisha unabadilika.
Mkoa wa Kilimanjaro uliwahi kuongozwa na mzee Gama na akaunyanyua kwa kiasi chake pia hata mkoa wa Ruvuma alikwenda pale na kufanya machache tu mkoa ukawa moja ya "The Big Four".
Unafahamu kwamba miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa ni mikoa iloitwa "the big four"? Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa?
Mikoa hii ilikuwa yailisha nchi lakini leo hii twapewa mchele wenye virutubisho kutoka nje ili tule tuvimbiwe.
Wamkumbuka au umewahi kumsikia marehemu mzee Gama?