Mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu nini kibadilike katika Mfumo wa Elimu ya Tanzania kupitia Twitterspace ya Jamiiforums

Mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu nini kibadilike katika Mfumo wa Elimu ya Tanzania kupitia Twitterspace ya Jamiiforums


Wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakilalamikia mfumo wa sasa wa Elimu ya Tanzania.

Jamiiforums kama mdau mmoja wapo wa elimu na mabadiliko inatoa fursa kwa Wanachama wake na umma kwa ujumla kutoa maoni yao juu ya nini hasa kibadilike katika mfumo wa elimu uliopo.

Ili kupata nafasi hii tafadhali jiunge nasi katika Mjadala wa TwitterSpace ya JamiiForums utakaofanyika tarehe 16 Februari, 2023 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 02:00 Usiku.

Pia, unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala.

Karibuni.
Watambue degree za sector mbalimbali kuliko kukomaa na degree za education na Mambo ni yale yale.

Kwa mfano bachelor of information technology akiwa na diploma atambulike. Ni mwl mzuri wa ICT

Bachelor of history. Atakuwa na hata certificate of education bachelor yake itambulike. Ni mwalimu mzuri wa history

Ni mpuuzi pekee ataona degree hiyo tofauti Haina mchango kwenye umahiri wa mwalimu
 
Na watoto wa viongozi wote lazima wasome shule za kata za serikali. Kiongozi akichaguliwa/kuteuliwa basi kabla ya kuapishwa watoto kwanza wakalipoti Kata sekondari/primary.
Vinginevyo uteuzi wake unatenguliwa abaki akisomesha huko anakokujua yeye.
Huu ni ujinga
 
Kwa sasa wanafunzi ni wengi sana kuliko uwezo wa hao walimu
Siyo lazima walimu hata kuwapeleka workshop kwa fundi maiko.kila alhamisi inatosha. Vipi hiyo inaitaji mwalimu, na kipindi cha test inatungwa huko watoto wanafa ya paper.4
 
Tatizo la Tanzania ni
Serikali
Wazazi

Wazazi hawaoni maana ya elimu, hivyo hawaweki mkazo kwenye elimu ya watoto wao.

Serikali

Walimu wengi 99% hawakutaka kuwa walimu, matokeo hayakwenda vizuri wakaona waende ualimu.
Wengine walisoma ualimu sababu serikali ilikuwa ikilipa kila kitu, hivyo wakaona waende huko ili wasome.

Miundombinu mibovu, shule hazina maktaba, maabara

Hakuna vitabu vyakutosha kila mwanafunzi.
 
Muda wa kukaa shuleni upunguzwe. Mtu hadi amalize chuo kikuu ana miaka 23/24 au 24 huyu alipaswa awe ameshajitegemea lakini anakuwa bado tegemezi.

Ikiwezekana miaka 19/20 kamili mtu awe ameshamalizana kabisa na mambo ya shule.

Mtu akimaliza masomo yake akiwa na umri mdogo inakuwa ni rahisi kufanya masahihisho kama alikosea uchaguzi wa alichokisomea. miaka 20-23 ni rahisi kurudi kutafuta ujuzi mpya, tofauti na akiwa na umri mkubwa ataishia kukata tamaa.
 
Asante! Tatizo la elimu yetu ni mtaala. Kwa kifupi tu: warudishe mtaala wa zamani miaka ya 1990. Mtaala huu ulikuwa mzuri sana na sisi tulioupitia tunaona matunda yake. Pia kiingereza kifundishwe kuanzia darasa la kwanza.
Mzee wangu aliniambia hii na akasema yule jamaa wa physics with chemistry alipewa pesa na mabeberu akahalibu kilakitu
 
Elimu ya ujuzi mbona ipo veta, mbona veta hampeleki watoto wenu wala hatuoni foleni ya watoto wakiandikishwa veta? Mnalilia elimu ya ujuzi wakati ipo veta na hamthubutu peleka watoto uko. Watanzania wanafki sana.
Wazazi wengi ni washamba ukiongelea degree au diploma akili zina waruka
 
1.kuwe na uwiano sawa wa walimu katika kila 2.miundombinu bora na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.3 maslahi ya watumishi yaboreshwe.4 mwisho kila kiongoz atimize wajibu wake
 
Mapendekezo yangu yatabase upande wa mabadiliko ya masomo na lugha ya kufundisha kama ifuatavyo

1. Kuwe na somo la computer/tehama (ICT) ambalo litafundishwa kwa kina kwa vitendo zaidi kuanzia darasa la 3 Hadi chuo kikuu kwa wanafunzi wote

Hii itasaidia kuendana na maisha ya sasa (digital word) pamoja na kusolve tatizo la ajira, kutokana na somo Hilo tutazalisha programmers wengi, mafundi wengi, maIT technicians weng nakadhalika, hawa wote hawatohitaji kusubir ajira badala yake kila mmoja atashika chake na kujiajiri

2. Sambamba na fani nyingine zitakazokuwepo, somo la ujasiriamali (entrepreneurship) lifundishwe kwa kina na kwa vitendo katika lever zote za elimu kuanzia darasa la 3 Hadi chuo kikuu kwa wanafunzi wote

Hii itasaidia ule ujuzi mwanafunzi alioupata ajue anautumia vipi ili umuwezeshe kuishi regardless changamoto mbali mbali atazokutana nazo

3. Masomo yawe kwa lugha ya kiingereza kwa lever zote za elimu, yawe ya kiingereza si kwa maana vitabu na notes darasani viandikwe kwa kiingereza kama ilivo sasa katika shule zetu za sekondari bali wanafunzi na waalimu wakiishi kiingereza
 
Shule isifundishe masomo ya sayansi kama hamna vifaa vinavyohitajika vya maabara wwalau kwa 90%. Sayansi isifanywe nadharia, sayansi ni vifaa, sayansi ñi vitendo

Hasa hasa shule za sekondari ama la tutaendela kuwaferesha watoto wakati sie ndotunaowaferisha na ni hasara kwa Taifa kupotez muda wao na pesa
 

Wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakilalamikia mfumo wa sasa wa Elimu ya Tanzania.

Jamiiforums kama mdau mmoja wapo wa elimu na mabadiliko inatoa fursa kwa Wanachama wake na umma kwa ujumla kutoa maoni yao juu ya nini hasa kibadilike katika mfumo wa elimu uliopo.

Ili kupata nafasi hii tafadhali jiunge nasi katika Mjadala wa TwitterSpace ya JamiiForums utakaofanyika tarehe 16 Februari, 2023 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 02:00 Usiku.

Pia, unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala.

Karibuni.
waongeze masomo ya ujuzi ili wanafunzi wanapomaliza wanakuwa na ujuzi wowote
 
Back
Top Bottom