Mimi binafsi nafanya hayo yote, napika, nafua, nasafisha nyumba etc pia sioi Mwanamke aje kufanya hayo kama ndio PRIMARY TASK hapana. Ila kwa nature na ASILI hayo yanatakiwa kufanywa na MWANAMKE. ndio kaumbiwa kufanya hayo.
Mwanaume ana offer vitu vingi
1_ Ulinzi
2_Ushauri uliosahihi (Mara nyingi, huwezi fananisha na ushauri wa Mwanamke)
3_MKATE Mezani
4_Ujenzi wa familia Bora. (Angalia malezi ya Single Mama ndio utanielewa).
Wanaune wanatembea na housegirl kutokana na MAMA mwenye nyumba kutokuwa makini na NDOA yake.
1_ Chakula apike housegirl
2_Nguo anyooshe yeye
3_Maji aniwekee bafuni
4_Chakula anipakulie
5_Nikirudi Mizigo yeye ndio anapokea
6_Kodi ya Meza namuachia yeye
7_Kitanda na usafi wa chumbani anasafisha yeye..
Sasa hapo MKE ni yupi? Anafanya kazi gani? Housegirl anafanya majukumu ya MKE ndio maana hicho kipande kidogo cha SEX anaamua kukimalizia kukifanya mwenyewe.
Si kweli.. Sex inamtesa yule asihejitambua ni nani? Na kama sex ikikuendesha hutoweza kufanya maamuzi magumu kama Mwanaume.
pia tusidanganyanye kwamba hakuna njia ya kujinufaisha nafsi.. si kweli.
Kama watu wanafungwa JELA Miaka 40 na hawafi.. na huko jela hakuna MWANAMKE na bado wanaishi duniani hakuna cha kunitisha hata mkiambizana mbanie hizo K.
Kijana hayo majukumu siyo nature ya mwanamke hayo ni gender assigned roles tu ambazo ziligawanywa enzi za mababu zetu, majukumu pekee ambayo ni nature kwa mwanamke ni yale ya kimaumbile, kama kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha et al
Na hayo ndio majukumu pekee ambayo mwanaume hawezi kuyafanya, ukiniambia hayo majukumu mengine ya kazi za ndani nayo ni nature ya mwanamke, basi tuseme pia na jukumu la kutafuta pesa ni nature ya mwanaume hivyo mwanamke halimuhusu
Sawa kama mwanaume anaoffer hayo yote basi na mwanamke naye anaoffer hayo niliyoyaorodhesha awali, kufanya kazi za ndani, kuzaa, kulea, majukumu ambayo mwanaume hawezi au hataki kuyafanya kabisa
Sasa mkuu kama unataka mwanamke afanye hayo majukumu yote ambayo unaona housegirl hatakiwi kufanya, kwanini unataka na jukumu la kutafuta hela na kulipa bills nalo akusaidie, wewe jukumu lako na umuhimu wako kwa mwanamke unakuwa ni upi sasa
Ukiniambia watu wanafungwa jela na hawafanyi sex nakataa, kwa sababu nina uhakika yanayoendelea huko magerezani unayajua fika wala sina haja ya kuyaandika hapa, na wanaume wengine ambao hawana access na sex huwa wanaishia kujichua kitu ambacho hawapendi na hufanya basi tu
Kama kweli sex ingekuwa haina umuhimu kwa wanaume basi wengi wasingekuwa wanalalamika endapo wakikosa na wengine wasingekuwa wanahonga pesa, mali, nyumba na magari kisa hiyo hiyo sex tu
Mimi ninachoshangaa ni kwanini wanaume wengi wanataka wanawake wawasaidie majukumu yao ila wao hawataki kusaidia majukumu ya wanawake, yani mwanamke afanye majukumu yake yote peke yake halafu bado atafute na pesa, wakati huo eti mwanaume akitafuta pesa tu
Yani eti mwanamke ambaye ni msaidizi ndio afanye majukumu mengi zaidi kuliko mwanaume ambaye ni kiongozi, kuna msemo wazungu wanasema "with great power comes great responsibility", ila cha ajabu wanaume wa kiafrika wanataka hiyo power tu ila hiyo responsibility hawataki
Na kwa mantiki hiyo basi maana yake ni kwamba mwanaume ndio mbinafsi zaidi kuliko mwanamke tofauti na ilivyozoeleka kwamba eti mwanamke ndio mbinafsi