Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Kuna namna kama nakuelewa hiviiiiii. Ila twende taratibu sasa.
Huyo mwanaume kuna namna hajapatiwa attention vizuri.
Unaona sasa! Mwanaume unafanyiwa kazi za ndani unapewa na pesa juu bado unataka attention ni attention gani hiyo unataka rafiki?
 
Yes mimi nina uwezo wa kuhudumia familia na nimeshuhudia familia nyingi ambazo wanawake ndiyo wanahudumia familia ilihali wanaume wapo wapo tu! Hivi hizi personal attacks bado hamjaziachaga tu jamani?
Nataka nikuone ni prove..... Maana sipendi kuongea nadharia na mtu ile hali tunaweza kuonyeshana ushahidi wazi wazi.
 
Sasa si jukumu lako boss? Au la nani?
Na yeye jukumu lake ni lipi?kama mwanamke anaishi kwake, anafanya kazi na anaingiza kipato chake kizuri, ajihudumie akikwama nipo kwa ajili yake tuta sort out, nami pia nikikwama natarajia same treatment kutoka kwake, 2 way traffic...ila siyo vizinga visivyokuwa na akili. Siyo kiaa kitobo basi unifanye nihudumie mtu 'mbinafsi'

Kama ni mke wa ndoa hilo ni jukumu langu kuhakikisha natimiza wajibu, ila sitarajii kwamba kipato chake afanye mambo yake ya siri, na majukumu madogo madogo lazima atafanya (kwa mwanamke anayejielewa) baba una deal na mambo mazito
 
Jifunze kuachilia, jifunze kusamehe. Mwisho wa siku uchungu unakuumiza wewe zaidi kuliko hata hao uliowabeba moyoni kwa chuki kubwa. Wakati wewe unaiharibu familia yako kwa nguvu zote kisa uchungu; hao kina Jack waliokuumiza maybe ndoa zao zinawaendea vizuri tu na walishakusahau kabisa. Upe moyo wako amani; uchungu utaondoa utu wako na kukufanya uwe mnyama; and there is no reward for that. Usiharibu maisha yako kwa sababu ya mtu aliyekuumiza.
Sawa dear......
 
Hayo maandiko unayoongelea hapa hayahusiani na mada hii na hali halisi. Hapa tunaangalia Logic hizo story za maandiko waachie akina Gwajima.
Oohh basi tufanye hivi hata kwenye suala la mwanaume kumtawala mwanamke tusiende kwenye maandiko tuyaweke pembeni kabisa halafu nikuulize hili swali! Kama mwanaume na mwanamke wote wanahudumiana na wote wanachangia bills pasu kwa pasu au pengine mwanamke ndiyo anatoa zaidi hapo utasema huyo mwanaume ni kichwa cha familia na kama jibu ni ndiyo je ni kwa misingi ipi?

Kumbuka tumetoka kwenye maandiko tumewaachia kina gwajima! Sasa tunatumia logic na tunaangalia hali halisi!
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Nataka nikuone ni prove..... Maana sipendi kuongea nadharia na mtu ile hali tunaweza kuonyeshana ushahidi wazi wazi.
Nimeshakuambia wapo pia wanawake wengine wengi tu wanaohudumia familia ilihali wanaume wapo! Mbona unajitoa ufahamu rafiki?
 
Na yeye jukumu lake ni lipi?kama mwanamke anaishi kwake, anafanya kazi na anaingiza kipato chake kizuri, ajihudumie akikwama nipo kwa ajili yake tuta sort out, nami pia nikikwama natarajia same treatment kutoka kwake, 2 way traffic...ila siyo vizinga visivyokuwa na akili. Siyo kiaa kitobo basi unifanye nihudumie mtu 'mbinafsi'

Kama ni mke wa ndoa hilo ni jukumu langu kuhakikisha natimiza wajibu, ila sitarajii kwamba kipato chake afanye mambo yake ya siri, na majukumu madogo madogo lazima atafanya (kwa mwanamke anayejielewa) baba una deal na mambo mazito
Kwenu huyo ndiye mwanamke anayejielewa! Basi sawa kaka!
 
Mimi hujihudumia mwenyewe staki back up ili mtu ani control so najiweza na wewe mwanaume usitegemee kuni control na vtu vyako maana staki, pia wanaume wengi sikuhizi wanapenda kupewa kuliko kutoa vya bure loh
 
Hela ya mwanamke ni ya kuogopwa sana, unaweza mpa mwanamke wako 100k then baadae kdgo mkapata changamoto mfano luku ikaisha ukamuomba akupe elfu 5 kwenye hela uliyompa ili utatue hiyo changamoto(mfukoni huna kitu una nauli ya kuendea kwenye mishe zako tu). Atakupa lakini ndani itamuuma sana nasema ivi kwa experience mkuu hela ya Ke ni chungu mno ndio maana hata wengi zawadi zao kwa wanaume wao ni vitu vidogo dogo tu [emoji23][emoji23] tusoksi twa buku.
Kwa sababu hatujaumbwa kutoa Bali kupokea tu.
 
Mimi hujihudumia mwenyewe staki back up ili mtu ani control so najiweza na wewe mwanaume usitegemee kuni control na vtu vyako maana staki, pia wanaume wengi sikuhizi wanapenda kupewa kuliko kutoa vya bure loh
Control ya mwanaume inatakiwa kuwa pale pale, uwe nacho usiwe nacho ukiwa na mimi ujue mimi mwanaume ndio kichwa, kisha unafuatia wewe mwanamke wangu wa ubavauni, hao wanaotegemea wanawake ni 'mafala', ila haiondoi utu mwenzako akikwama basi usimsaidie kwa sababu siyo jukumu lako...hapo mapenzi yako wapi sasa ubinafsi na uchoyo wa wanawake unafanya mahusiano yanakuwa magumu sana kwa wanaume
 
Dah, sasa kwani hii mada mbona mnataka kuivuruga, iko wazi! Hakuna mtu aliesema anataka kulelewa ila tunazungumzia kupigana tuff kama sehemu ya mapenzi yenu. Kama vile ambavyo mwanamke anaweza chukuliwa akiwa form 4 akasomeshwa hadi kufikia chuo kikuu basi ndio same ambavyo mke akipata kazi anaweza msaidia mume mambo yanyomuelemea. Hapo kuna kulelewa? Acheni kubaka mada.
umeona msemo niliokuwekea juu bro
 
Back
Top Bottom