Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Huyu Karma atakua anamsoma Sana yule jamaa insta anajiita Idd makengo ....yule jamaa anateka akili za wanawake kibaya anawapoteza badala ya awasaidie .! Ni mjinga Sana yule jamaa ana story za kutunga Sana na si za uhalisia bonzo kabisa

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Na mwijaku. Kwenye page za hawa jamaa mwanamke ni malaika ambaye hakosei, hasaliti, anaumizwa hisia haumizi, ananyanyaswa.......

Kitu wasichojua ni kuwa katika biashara yoyote jambo muhimu ni kumtengenezea mteja wako story itakayomvutia....
 
Control ya mwanaume inatakiwa kuwa pale pale, uwe nacho usiwe nacho ukiwa na mimi ujue mimi mwanaume ndio kichwa, kisha unafuatia wewe mwanamke wangu wa ubavauni, hao wanaotegemea wanawake ni 'mafala', ila haiondoi utu mwenzako akikwama basi usimsaidie kwa sababu siyo jukumu lako...hapo mapenzi yako wapi sasa ubinafsi na uchoyo wa wanawake unafanya mahusiano yanakuwa magumu sana kwa wanaume
Kutoa msaada huwa natoa Sana kwa watu wengi sio mpenzi tu hata wenye uhitaji kwa kidogo nilicho jaliwa, concern yangu sipendi mtu kunipangia maisha kisa mwanaume, kila mtu abaki kwenye lane yake kwa kweli
 
Group conformity and African culture ni mojawapo ya sababu kubwa za Watu weusi kuendelea kuwa Maskini, Wakati weusi mnaitana majina yakukatishana tamaa km Mario, Goal keeper na kuogopa ke'' wenye hela. Wazungu wao wanaamini ''kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna Mwanamke'', wanajali, kulinda mke na mnyama kwa hali ya juu! ndiyo siri walio nayo!

Mwanaume Oa tu hata km amekuzidi kipato ukinyanyasika ni fursa adimu kwako, ichukulie kama changamoto, kichocheo cha kukutoa kwenye Umaskini, tumia hela zake kujinufaisha ili mwisho wa siku uwe hela kumzidi yeye!! na uendelee kumheshimu na kumpenda zaidi kwa kukunyanysa. uwe makini tu asikuue!

Hata ukikwepa ujue unaweza oa mwanamke Goal keeper, House girl maskini lkn na bado akatajirika kukupita kwa kutumia hela zako hizo!! kwakujiunga na vikoba tu akafika mbali sasa je utamuacha?

Mleta Mada kumbuka tuna Ma boss wanawake maofisini kwetu huko, Waalimu, wafanyakazi wenzetu ke'' tunaolingana kipato lkn wanazo, Jeshini huko ndo usiseme ki-mdada kinalingana na mdogo wako lkn unakapigia saluti na kanakutuma. utasikia ''weee kopro kuja hapa!!!

Umesahau JKT wakati ukiwa Kuruta? unaonaje vile vidada vikopro vilivyokuwa vinawaendesha, una ndevu na Degree yako ya mlimani!!! huko kooote ni wewe ujifunze ! sidhani kwa mtu aliyepita huku ataogopa kuitwa Mario!!! lkn wengine hatuwalaumu sababu hawajui.

Matajiri wengi ni wake zao ndo kisababishi, akimwaacha tu kwa dharau bila chochote na kuoa mke mwingine, lazima utajiri uporomoke! na wengine kuwa maskini kabisaa kama ''Yego store''. Matajiri hutafuta wanawake/ume wenye harufu ya utajiri. waoane na watoto wao!
 
mkuu hili suala linatokana na nature ya uumbaji ndo maana mara nyingi ke akiwa provider madharau hutokea na inakua ngumu kumcontrol
Akikudharau manake wewe umeshindwa kumpita. piga kimya na dhamiria ushindi moyoni !!! na ushindani uko mahali popote utakapo kwenda Duniani, Drsani, michezoni, Kazini,nk, hata uwe Rais, ma-rais wenzako wenye nazo watakudharau huko kwenye vikao vyenu!

Hata kunako familia yenu ukishindwa kupata pesa wadogo zako watakudharau, Baba yako akifa huambiwi, utajua while's too late, sasa wewe, muache udharauliwe mazima, Usilalamee sasa?? hapa ni wewe kukaza Buti bin kukomaa uwe mbunifu ufike pale unapoona uko juu kifedha! walalamishi humu sidhani km drsni walikuwa kwenye kumi bora.
 
Sawa baki ulivyo. Kama haukujifunza kwenu then dunia itakufunza kwa namna yake....uzuri ni kwamba nature haibishiwi. Hapa unabishana na mimi unanichosha tu akili but kuna ukweli na utabishana nao vizuri....
Wala sina la kujifunza hapo nimeshajifunza mengi kupitia mahusiano ya watu hivyo siwezi kusubiri hadi yanikute mimi ndiyo nijifunze! Kwangu mahusiano nilishayapiga stop hata kabla sijaanza kupitia ambayo watu wengi wanayapitia hivyo hakuna kinachoweza kunibadilisha msimamo wala mtazamo wangu!
 
”Demu wa shida na raha na misoto sana, huyo demu hanifai... changamoto hana!”

~Nikki II.
 
Ukianza kujitegemea na kuanza maisha utaelewa hizo nadharia mnazojifunza huko Facebook na Instagram haziapply kwenye maisha.......
Woii mbona umeng'ang'ania kujitegemea? Kwa taarifa yako mimi hapa nilipo ninajitegemea na wala sijaanza jana wala juzi!

Na katika umri huu nilio nao tayari nimeshashuhudia utopolo mwingi kwenye mahusiano ya watu kiasi kwamba kwangu mapenzi nayaona kama ujinga tu! I know a couple or two that inspire me to stay single!
 
Anahisi maisha yanafanyika kwenye wonderland? Af hawa wa hivi unakuta chuo alikuwaga mke wa mtu ila humu anatukazia
Teh teh siyo mimi my friend! Na wala siwezi kukulazimisha uamini hilo ila ukweli utabaki pale pale tu!
 
Tukitoa maandiko logic ya mwanaume inamwambia kulala na kuzaa na mwanamke yoyote anaevutiwa nae.....

So,unataka tutumie logic ya kiume au?!
Kwani mwanamke ni kipi kinachomzuia kufanya hivyo? By the way kwani hiyo siyo logic mnayoitumia sasa hivi au mnataka kusema sasa hivi ninyi mko na mwanamke mmoja mmoja tu?
 
Wewe sasa unaishi vipi ndio napenda kujua.... Mbona una preach ambacho haupractice?!
Kwahiyo mfano mimi nikikuambia naishi kwa wazazi ndiyo itabadilisha ukweli wa ninachokisema? Mimi siko kama wewe bro huwa sisubiri eti kitu hadi kinikute ndiyo nikiamini mmi siyo tomaso huwa naanza kujifunza kupitia makosa ya watu wengine!
 
Hii sio lengo la mada, unapotosha mada kwa makusudi! Turudie kwenye lengo.
Mnachofanya ni kuukimbia ukweli! Na hiki ndicho nilichojifunza tangu najiunga JF tunapojadili mada kama hizi huwa mnataka kusikia yale ambayo yatawafurahisha masikio yenu tu hamtaki kuambiwa ukweli kwa sababu mnajua ukweli ni mchungu na unauma!
 
Mbona makofi hampokei [emoji23][emoji23][emoji23] mnajifanya kukimbilia kwa joyce Kiria.
Kila mtu kaumbiwa kupokea inategemea na wakati gani
Duuh! N wapi paliposema mwanaume naye kaumbwa kupokea?
 
Huyu Karma atakua anamsoma Sana yule jamaa insta anajiita Idd makengo ....yule jamaa anateka akili za wanawake kibaya anawapoteza badala ya awasaidie .! Ni mjinga Sana yule jamaa ana story za kutunga Sana na si za uhalisia bonzo kabisa

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Kwa taarifa yako sifuatiliagi hizo hadithi zenu za huko instagram sijui facebook maana hao nao ni wale wale tu! Mimi najifunza kutokana na mahusiano ya watu wanaonizunguka ambayo nayashuhudia kwa macho yangu siyo hayo ya kwenye maandishi!
 
Wenzake walipokuwa shule walisema "education is better than money" na walikuwa na hoja nzito kabisa kutetea hiyo ajenda yao, sasa akawaulize bado wana maoni yale yale?!
Na hapo ndio mnapokosea! Kulazimisha mitazamo ya jamii kuwa uhalisia!
 
Back
Top Bottom