Mapenzi ni upuuzi

Mapenzi ni upuuzi

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,971
Reaction score
4,085
Nimegundua kwa mara ya pili mapenzi ni upumbavu na upuuzi tu, yalishanikuta mara ya kwanza nikapuuzia na hii mara ya pili nathibitisha ni upuuzi tu!

Baada ya siku kadhaa kuwakejeleli watu hapa JF waliokuwa wakilialia kipuuzi kuhusu mapenzi na mimi yamenikuta aisee!

Unampenda mtu na kumjali na kumfanya mtu muhimu halafu anakuja kukugeuka kipuuzi! Muhimu ni kwamba nilishajiwekea kutomuamini 100% mwanamke na hii imesaidia kidogo. Ila nimeumia sana.

Kuna mwanamke nilipanga kumuoa na tulipanga naye mambo mengi tu, tulipanga mwakani nifanye kweli kumuoa ila kumbe kuna mwenzangu sasa kapeleka posa na mwanamke kakubali kuolewa!

Sasa najiuliza kule kumjali kote na kujifanya kunionesha ananipenda kupitiliza yale yote yalikua maigizo? Mpaka muda huu nashindwa kumtafakari huyu binti maana kanipotezea muda aisee.

Leo nasema kamwe sioi, sioi, sioi kamwe! Naanza kulipa kisasi sasa, nitawadanganya, kuwachezea na kuwapotezea na ninyi muda ili kulipa hiki kisasi. Nasema kataa ndoa, kataa ndoa!
 
Hahaaa, 100% humwamini, ..... Huezi kumjali/kumthamini mtu ka humwamini ata kwa asilimia 5-20. Pole, it's weekend nyunyizia moyo
 
Sas mbona unatukatisha tamaa na sisi tunaopenda huku. Unatak kusema mambo yatabadilika hata kwa jinsi anavyo apa kiasi hik "your my one and only" [emoji849][emoji2]
 
Hahaaa, 100% humwamini, ..... Huezi kumjali/kumthamini mtu ka humwamini ata kwa asilimia 5-20. Pole, it's weekend nyunyizia moyo
Me simuamini mwanamke 100% japo nampenda na huwa na tahadhar ila huyu nilipanga kumuoa kwahy kumjali ni kawaida tu
 
Sas mbona unatukatisha tamaa na sisi tunaopenda huku. Unatak kusema mambo yatabadilika hata kwa jinsi anavyo apa kiasi hik "your my one and only" [emoji849][emoji2]
Kataa ndoa ndugu, utakuja kulia lia na uzi hapa JF
 
Ona huyu eti nme jiwekea 100% kuto muamini mwanamke afu una lia lia hapa ..uoi nini sasa? una leta umwamba uku machozi yana kutoka
 
Ona huyu eti nme jiwekea 100% kuto muamini mwanamke afu una lia lia hapa ..uoi nini sasa? una leta umwamba uku machozi yana kutoka
Una uhakika.
 
Back
Top Bottom