Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 54
- 140
Na THABIT MADAI, ZANZIBAR.
‘ZANZIBAR ni njema atakaye na aje’, Msemo huu ni maarufu sana visiwani haapa, na kwamba umetokana na ukarimu wa watu wake tangu asili na asili.
Bila ya shaka hakuna asiejua kuwa watu wa Zanzibar walikuwa wakiishi kwa msingi ya kiimani inayopelekea kuishi kwa kupendana, kuaminiana, kusaidia kwa hali na mali wakati wa furaha na hata wakati wa shida na kufanya watu wake kujizolea sifa kubwa Duniani kote ya ukarimu.
Lakini jambo kubwa la kushanga hali hiyo imebadilika mara moja, kwa sasa Zanzibar na watu wake wameingia doa lililopelekea kuchafua sifa iliyopendezesha haiba yao ya muda mrefu ya ukarimu.
Doa hilo linatokana na kushamiri kwa kasi matendo ya udhalilishaji wa kijinsia na ukatili kwa wanawake na watoto ambapo kwa sasa si ajabu tena kusikia katika vyombo mbalimbali vya habari matendo hayo yaripotiwa mara kwa mara, na unaposikia taarifa hizo zikiripotiwa, mara nyingi zile zinazohusu watoto wadogo ndio huchukua nafasi kubwa.
Kwa mujibu wa takwimu za mpango kazi wa taifa wa Zanzibar kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto wa mwaka 2017/2022, ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar, asilimia tisa ya watoto wa kiume na asilimia sita ya watoto wa kike Zanzibar hudhalilishwa kimwili na kingono wakiwa chini ya umri wa miaka 18.
Takwimu hizo zinaeleza kuwa kati ya watoto 10 waliokumbwa na udhalilishaji, mtoto mmoja ameripoti kwenye vyombo vya kisheria na kupatiwa huduma zinazostahiki huku ikionesha kuwa nusu ya watoto wa kike na wa kiume waliokutana na vitendo hivyo wamesimulia walichotendewa.
Kushamiri kwa vitendo vya udhalilishaji Zanzibar kumesababisha jamii na hata Serikali kuwa njia panda ambapo hadi sasa bado hawajapata muarobaini hasa wa kukomesha vitendo hivyo licha ya kuwa kila kukicha wanakuja na mikakati mbalimbali ya kukabiliana navyo.
Hivi karibuni kumekuwa na tishio kubwa la kuwepo na kuongezeka kwa vitendo vya ushetani vinavyofanywa na baadhi ya watoto wa kike kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja pamoja na kushiriki mapenzi kinyume na maumbile kutokana na sababu mbalimbali.
Jambo hili si la leo limekuwepo kwa miaka mingi visiwani hapa kama Wanaharakati,Jamii na wanasiasa wanavyoeleza.
JUMAZA WAELEZA
Sheikh Ali Abdallah Amour ambaye ni Katibu wa Kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji kutoka Jumuiya ya maimamu Zanzibar (JUMAZA), anasema kwamba wamefanya tafiti mbalimbali toka mwaka 2014 hadi hivi sasa ambapo wamebaini kuwepo kwa ushetani huo wa watoto wa kike kushiriki mapenzi ya jinsia moja pamoja na kushiriki mapenzi kinyume na maumbile.
Sheikh Amour anasema kupitia katika tafiti hizo wamejiridhisha kwamba tatizo hilo linatendeka kunzia kwenye shule za maandalizi hadi kwenye jamii ambao huko ndipo kwenye uwoza mkubwa.
Anasema kwamba, tumegundua kuwa watoto wa kike hufanya mapenzi kinyume na maumbile ambapo mchezo huo huupa jina la ‘Help Me’ ikiwa na maana umemsaidia kutopata ujauzito na kuchunga bikra yake.
“Tafiti zetu tumegundua mambo mengi sana katika jamii yanatendeka ambayo ni kunyume na maadili kabisa lakini jambo hili kwa watoto wetu wa kike nahisi lichipukuia hasa katika maeno ya ufukweni ambapo mchezo umekuwa maarufu hadi kupewa na jina la ‘Help Me’, anasema Sheikh Amour.
Anaeleza kwamba, tunapoelekea tumebaini kwamba unaweza kuwakuta mabinti wadogo wakiwa na usichana wao lakini tayari wameshaharibiwa kinyume na maumbile ambapo athari zake ni kubwa sana.
Hata hivyo anaelezea kuwa, tatizo hilo huanzia katika mashuleni, kwenye fukwe na baadhi ya maeneo ya Hoteli za kitalii ila katika maeneo ya mijini ndipo hasa kunaonesha kuwa kuna kadhia hii kwa wingi.
“Kwa ujumla tatizo ni kubwa tulitembelea shule za maandalizi na msigingi 74 ambapo tumebaini kuwepo kwa vitendo mbalimbali kama vile Ushoga (Ubaradhauli), watoto wa kike wakiwa tayari kushirki katika mapenzi wao kwa wao,wao na wanaume hata mapenzi kinyume na maumbile (liwati),”anaeleza.
Anaongeza kuwa kati ya shule 74 shule 10 ndizo wamekosa maelezo ya kuthibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo.
WANAHARAKATI WANENA
Sheikh Nassoro Hamadi Omar ambaye mmoja wa wanaharakati Zanzibar anasema kuibuka kwa kasi jambo hilo katika jamii linatokana na mpango maalumu ulioletwa kwa lengo la kuharibu utamaduni wa Zanzibar.
Anasema kushamiri kwa vitendo hivyo visiwani hapa haukuja kwa bahati mbaya na kwamba umeletwa na baadhi ya watu kwa makusudi kwa lengo la kukuza kutokana na maslahi yao binafsi.
“Kuwepo kwa vitendo hivi kuna watu wanalipwa na kutumia kila aina ya nyenzo ili liweze kusambaa na vizazi vyetu viwezekuharibika,”anasema.
Anaongeza kuwa watu hao wanatumia kila aina ya nyenzo katika kulikuza jambo hilo ambapo wanatumia utaalamu, fedha na hata sayansi ya teknolojia kubwa katika kulikuza na kulisambaza jambo hilo.
“Wakati tukiwa tunapanga kumaliza jambo hili na wao hivyo hivyo wanapanga namna ya kuliendeleza na wanalipana kwa fedha nyingi sana,” anasema.
Nae Bi Amina Yusuf anasema suala hili limekithiri kwa kiasi kikubwa Zanzibar inaonekana kuna watu wapo wanafurahikia kuwepo jambo hili licha ya kuwa wanaoumia ni watoto wadogo ndani ya visiwa hivyi.
“Uwepo wa suala hili wanaomia na kuathirika ni watoto wetu, inaonekana kuna watu tena wakubwa wapo katika kulishabikia suala hili kwa maslah yao binafsi” anasema Bi Amina.
JAMII INAELEZA
Masoud Bakari Masoud mkaazi wa Raha leo Unguja anakiri kuwepo kwa vitendo hivyo katika eneo analoishi na kueleza kwamba kuwa matendo hayo sasa yamekuwa yakifanywa hadharani na watoto wadogo wa kike ndio wamekuwa wakishiriki katika vitendo hivyo.
“Jamii yetu sasa sijui imeingiwa na mdudu gani maana hapa raha leo watoto wadogo ndio wanashiriki matendo hayo, watoto wa Skuli na wengine tunaambiwa kuwa kuna mtandao upo kazi yake kuwauza hao watoto,” anaeleza.
Aidha aneleza kwa upande wake anahisi kuenea kwa vitendo hivyo, watoto kuogopa kupata mimba, kushamiri kwa mabaradhuli ambapo watoto wa kike ndio huwa marafiki zao, pamoja kuzuka kwa saluni za kike za hovyo.
“Katika kukomesha vitendo hivi kwangu mimi nahisi kwamba tuanze na hawa mabaradhuli ambao wanawafanya watoto wetu wa kike marafiki, tupige vita kuwa na saluni za kike hovyo maana hawa watoto wanapokwenda huko hujifunza mambo yasiyokuwa mila na desturi zetu,”anafafanua.
Nae Mariam Ali Mbwana anasema kuwa ni kweli katika jamii matendo hayo yapo na kila siku zikenda bado kupungua yanaongezeka pamoja na Viongozi wa Dini na Serikali kukemea kila kukicha.
WANASIASA WAELEZA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir ameeleza kwamba, ni kweli matendo hayo kwa sasa yapo mengi katika jamii licha ya kwamba hayakuanza hivi karibuni yamekuwa kwa muda mrefu sasa.
“Ni kweli haya mambo yapo na kila siku zikienda baada ya kupungua yanazidi kushika kasi pamoja na kwamba Serikali inakemea, watoto wetu sasa wakike sijui wamekumbwa na ushetani gani hadi kudiriki sasa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, kushiriki mapenzi kinyume na maumbile,” anaeleza Ameir.
Alisema, kwa mauno wake kwamba Jamii bado haiko tayari kushirikiana na Serikali katika kukomesha tabia hii sambamba na baadhi ya waajiriwa wa Serikali kujihusisha na tabia ya kupokea na kutoa rushwa.
“Mimi binafsi kwa muono wangu naona jamii haipo tayari kushirikiana na serikali katika kukomesha tabia hii ambayo kwa sasa inahila mbaya Zanzibar,” anaeleza.
Aidha anaeleza kwamba Sheria zizingatiwe upya bila ya kujali jinsia, kwani vitendo vya hivyo hufanywa na jinsia zote.
“Ushauri wa ujumla katika kukomesha matendo kama hayo visiwani Zanzibar, Sheria ziangaliwe upya bila ya kujali jinsia kwani wafanyaji wa matendo haya ni pande zote mbili, kwa Wanawake wamekuwa hawachukuliwi hatua na kupekelea kuhisi kama hausiki na kesi,” ameeleza.
Nae Katibu Mkuu wa Chama cha UPDP Hamad Ibrahimu anaeleza kwamba kukithiri kwa matendo hayo kwa watoto visiwani humo ni mpango maalumu uliosukwa wa kuharibu mila na Desturi za kizanzibar.
“Bila shaka vitendo hivi vimeletwa na wageni ni nadra sana kuona au kusikia maeneo ya vijiji au ng’ambo ya mji, wafanyaji wa vitendo hivi ni watu wenye pesa ambapo hueneza michezo hii ya kishetani na kuharibu jamii yetu,” anaeleza Katibu UPDP
Pia anaeleza kwamba, Serikali inapswa kuchukua nafasi yake kwa kushirkiana na Jamii kuweza kukomesha vitendo hivyo ambapo kwa sasa vinaonekana jambo la kawaida katika jami hususani maeneo ya mijini.
“Serikali kwa kushirikiana na jamii nzima inatakiwa kuchukua hatua madhubuti ili kuinusuru jamii na vizazi vijavyo, kukemea mchezo hii na kufanya tafiti na kuwachukulia hatua wale ambao waneneza kwa watoto wetu,” anaeleza.
SHERIA ZIPOJE
Kwa mujibu wa Sheria ya Adhabu Namba 6 ya mwaka 2018 inasema kwamba, Mwanamke au motto wa kike ambaye anatenda tendo la usagaji na mwanamke mwingine au mototo wa kike mwingine, ama mfanyaji au mfanywaji, atakuwa ni kosa na akitiwa hatiani atapewa adhabu ya kifungo kwa kipindi kisichopongua miaka mitano lakini kisichozidi miaka kumi.
SERIKALI YANENA
Mkurugenzi wa Elimu na Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar, Safia Ali Rijali anasema suala hilo la mapenzi ya jinsia moja lipo kwa kiasi kikubwa ambapo watoto wadogo wa shule za msingi na Sekondari hujihusisha nalo.
Anasema ni kweli suala hilo kwa sasa lipo hadi watoto kwa watoto wenyewe hufanyiana ambapo anaongeza kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo na kwamba ipo haja ya serikali kufanya kufanya utafiti maalumu ambao utabaini chanzo na chimbuko la vitendo hivyo.
Anasema endapo Serikali ikifanya utafiti huo ambao unahusu kushamiri kwa vitendo hivyo unaweza kubaini kuwepo kwa taasisi ambazo zinafanya kwa makusudi suala hilo kwa makusudi.
Mkurugenzi huyo anasimulia ushuhuda wa vitendo hivyo katika moja ya ziara zake visiwani Pemba kwenye shule moja ambapo aliwauliza kesi za udhalilishaji zikoje na kwamba wakamjibu kuwa katika shule hiyo kuna kesi za utoro wa misitu.
“Nikauliza watoto wa misitu ndio nini nikaambiwa ngoja tukuletee watoto hao walikuja kama watoto watano na wengine wakakimbia kutokana wanajua wanachokifanya sicho nikawauliza kirafiki huko misituni mnafanya nini mmoja akajibu wanafanya kitendo cha kulawitiana watoto wa kiume hivyo kwa watoto wa kike nayo hivyo hivyo yanatisha kwa kweli,”anasimulia
Anaongeza kuwa baada ya kupata hali hiyo akawambia watoto hao wataje watoto wanaofanyia na nikaletewa watoto saba ambao wanawaongoza kuwafanyia vitendo hivyo wenzao lakini jambo ambalo lilinisikitisha kati ya idadi hiyo ikaongezeka.
“Na jambo lililoniliza hadi watoto wa shule ya maandalizi wa umri wa miaka minne anasema ashawahi kufanyiwa mara tatu mwingine anasema mara nne niliumia sana kiasi nilichanganyikiwa,”anasema
ATHARI ZA KIAFYA
Kwa mujibu wa mtandao wa Afya Jmaii na Dk. Love Community anaeleza kwamba, Kufanya mapenzi ya jinsia moja kwa watoto wa kike pamoja na mapenzi kinyume na maumbile kuna madhara makubwa ya kimwili, kiakili, na kiafya.
“Ukifanya mapenzi kinyume na maumbile, ukifanya mapenzi jinsia moja hakuna faida yoyote isipokuwa kuna madhara makubwa ukizoea kufanya michezo hiyo mishipa yako inatanuka na kusababisha matatizo mengine wakati wa kujifungua,” anasema.
Anasema, Mwanamke yoyote anaekubali kushiriki michezo hiyo ana hatari ya misuli yake kulegea na kushindwa kusukuma motto wakati wa kujifungua, hata hivyo ukiona mwanamke anapenda kushiriki matendo haya ni kwa sababu ya ulimbukeni wa kujaribu kutaka kufanya kila anachojisikia,” anasema
Anaongeza kuwa, wanaofanya haya wengine wanafanya kwa kutaka kumridhisha mwanaume wake , kwa wanawake kwa wanawake wanakuwa na homon nyingi za kike kitu ambacho kinapelekea kuwatamani wanawake wenzao.
“Kwa watoto wana madhara makubwa ambayo yanaanza kuwaathiri kuanzia utotoni, katika makuzi yao hadi ukubwani na hasa wakati wa wakujifungua,” Anaeleza.
Mwisho
Pia soma: Mbona wanawake hawakemei Usagaji kama sisi tunavyokemea ushoga?