Mapenzi ya mbali: Je, ni upendo au ni mtego wa kunitawala kiakili?

Mapenzi ya mbali: Je, ni upendo au ni mtego wa kunitawala kiakili?

Shemagical

New Member
Joined
Oct 25, 2024
Posts
1
Reaction score
3
Habari, Naomba ushauri wenu moyo unauma sana. Nipo kwenye mahusiano ya mbali (LDR) kwa miezi minane sasa. Nampenda sana huyu mwanaume, kiasi kwamba muda mwingi nautumia kusali, kufunga na kumuombea, nikiamini labda ana majeraha ya huko nyuma yanayomfanya awe hivi alivyo sasa.

Kuna kitu kilitokea kilinitia hasira sana. Mwanzoni nilivumilia hakuomba msamaha ni mtu asiyejishusha kabisa, lakini ilipojirudia mara ya pili nikaona ni makusudi. Katika hasira nilimwambia "tuachane. Lakini usiku, nilitafakari, nilimmiss na kuona nilichukua maamuzi kwa hisia, nikaamua kushusha pumzi na kumuomba msamaha.

Badala ya kunielewa, alipotezea simu zangu. Nilituma texts nyingi sana (kutokana na pressure) mwisho wa siku akaniblock kila mahali. Ameniweka kwenye "block" kwa wiki nzima.

Sasa hivi ameni-unblock baada ya kuomba pia kwa namba ingine, lakini anafanya kama vile amenifanyia hisani au ananionea huruma. Anatoa maneno yanayoashiria kuwa "nilistahili" ile adhabu ya kuniblock. nimepotezea kwakuwa nampenda sitaki kuongelea kilichotugombanisha. Hata hivyo, mimi naona mabadiliko makubwa kwangu simuamini tena kama mwanzo. Nahisi kuna mtu mwingine pembeni, naona kama amechoka au anatumia upendo wangu kama fimbo ya kunionea kiburi na kunicontroll.

Mimi ni yule aina ya mwanamke anayependa "vibaya" (deeply), na kwa sasa siwazi kabisa kuwa na mtu mwingine.

Je Huyu mwanaume ananipenda kweli, au anafurahia tu nguvu aliyonayo juu yangu baada ya kuona nampenda sana?

Je mimi kuweza kukaa kimya inaweza rudisha heshima, ingawa najua itakuwa ngumu kwangu.
 
Achana nae hata kama inauma , kiufupi hakupendi hakutaki na kapata mwingine , mzuri , muelewa na anae mpenda kuliko wewe.

Hivyo fanya utaratibu wa kujifunza namna ya kujipenda wewe kwanza kabla ya kuwapenda wengine.
Screenshot_2026-01-29_195616.jpg
 
Pole sana binti,
Mapenzi siku zote upofu unapopendwa hupaoni hadi pakiondoka..
unang'ang'ania asiyekupenda ili iweje?
tupo wanaume tunaothamini mapenzi ya dhati kutoka kwa binti kama nyie please, achananae njoo kwangu taratibu tutaanza kutengeneza serious relationship.
Ninamanisha nilichoandika'*
 
Pole sana binti,
Mapenzi siku zote upofu unapopendwa hupaoni hadi pakiondoka..
unang'ang'ania asiyekupenda ili iweje?
tupo wanaume tunaothamini mapenzi ya dhati kutoka kwa binti kama nyie please, achananae njoo kwangu taratibu tutaanza kutengeneza serious relationship.
Ninamanisha nilichoandika'*
😅😅😅😅predatory behavior
 
Achana nae hata kama inauma , kiufupi hakupendi hakutaki na kapata mwingine , mzuri , muelewa na anae mpenda kuliko wewe.

Hivyo fanya utaratibu wa kujifunza namna ya kujipenda wewe kwanza kabla ya kuwapenda wengine. View attachment 3538436
Sisi wazee wa michuzi yani pisi ikitoka tu tayari naanza kuchatisha nyingine. Hata kama imeenda sokoni tu, ikijichanganya kuhama mkoa ndo itakula kwakwe mpaka immalize
 
Endelea na maisha yako. He doesn't care for you as much as you care for him
 
Yaonesha wewe ni kero.
Unataka attention sana.
Muda wote ku-chat au calls.
Unapenda kunyenyekewa na kuombwa msamaha.
Umri wako au malezi vinaweza kuwa sababu.
Insecurity pia yaweza kuwa sababu.
 
Back
Top Bottom