Habari, Naomba ushauri wenu moyo unauma sana. Nipo kwenye mahusiano ya mbali (LDR) kwa miezi minane sasa. Nampenda sana huyu mwanaume, kiasi kwamba muda mwingi nautumia kusali, kufunga na kumuombea, nikiamini labda ana majeraha ya huko nyuma yanayomfanya awe hivi alivyo sasa.
Kuna kitu kilitokea kilinitia hasira sana. Mwanzoni nilivumilia hakuomba msamaha ni mtu asiyejishusha kabisa, lakini ilipojirudia mara ya pili nikaona ni makusudi. Katika hasira nilimwambia "tuachane. Lakini usiku, nilitafakari, nilimmiss na kuona nilichukua maamuzi kwa hisia, nikaamua kushusha pumzi na kumuomba msamaha.
Badala ya kunielewa, alipotezea simu zangu. Nilituma texts nyingi sana (kutokana na pressure) mwisho wa siku akaniblock kila mahali. Ameniweka kwenye "block" kwa wiki nzima.
Sasa hivi ameni-unblock baada ya kuomba pia kwa namba ingine, lakini anafanya kama vile amenifanyia hisani au ananionea huruma. Anatoa maneno yanayoashiria kuwa "nilistahili" ile adhabu ya kuniblock. nimepotezea kwakuwa nampenda sitaki kuongelea kilichotugombanisha. Hata hivyo, mimi naona mabadiliko makubwa kwangu simuamini tena kama mwanzo. Nahisi kuna mtu mwingine pembeni, naona kama amechoka au anatumia upendo wangu kama fimbo ya kunionea kiburi na kunicontroll.
Mimi ni yule aina ya mwanamke anayependa "vibaya" (deeply), na kwa sasa siwazi kabisa kuwa na mtu mwingine.
Je Huyu mwanaume ananipenda kweli, au anafurahia tu nguvu aliyonayo juu yangu baada ya kuona nampenda sana?
Je mimi kuweza kukaa kimya inaweza rudisha heshima, ingawa najua itakuwa ngumu kwangu.