Mapenzi ya mtandaoni yameniangushia kwa binti mwenye ulemavu, hakika huyu ndiye chaguo la moyo wangu

Kwa muda mrefu nimekuwa mpweke ila siku za karibuni kwenye mtandao nikawa niko busy na dada mmoja mzuri sana.

Basi tukaona kuna haja ya sisi kuonana kwani niko Dar na Yeye yuko Dar. Tukapanga kukutana naye Slipway.

Ijumaa jioni baada ya saa za kazi nikawa nimepiga kambi Waterfront Bar, nikaangiza kinywaji changu huku nikimsubiri mrembo.

Haikuchukua muda mrefu, angaingia msichana mrefu mweupe. Nikamkaribisha kwa hug moja matata sana.

Ule ulemavu wa mkono wake uliokatwa baada ya yeye kupata ajali, kwangu sijaona kwamba ni kasoro wala dosari. Nimeona ni chachu ya mimi kumpa moyo wangu wote, kumpenda zaidi na kumtunza kikamilifu.

Huyu binti sitaki nimuache, daima amekuwa akilini mwangu. Sijawahi kupenda namna hii.

Namuomba Mungu aliimarishe penzi letu hata tuufikie mwisho mwema
all the best bro make sure humchezei tu
 
Amenifukuza kwenye Uzi wake. Ngoja nisicomment. Ila najua alinielewa [emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji28] kitendo cha kumuanzishia uzi na kuelezea maumbile ya mwenzake tayari ni "shida".

Vinginevyo angekaa kimyaa tu maana inaonekana kama amempa msaada...

Yote kwa yote miili yetu sisi wanadamu ni haribifu, muda wowote kiungo chochote kinaweza kufa kama sio kufa kabisa mwili mzima.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa mpweke ila siku za karibuni kwenye mtandao nikawa niko busy na dada mmoja mzuri sana.

Basi tukaona kuna haja ya sisi kuonana kwani niko Dar na Yeye yuko Dar. Tukapanga kukutana naye Slipway.

Ijumaa jioni baada ya saa za kazi nikawa nimepiga kambi Waterfront Bar, nikaangiza kinywaji changu huku nikimsubiri mrembo.

Haikuchukua muda mrefu, angaingia msichana mrefu mweupe. Nikamkaribisha kwa hug moja matata sana.

Ule ulemavu wa mkono wake uliokatwa baada ya yeye kupata ajali, kwangu sijaona kwamba ni kasoro wala dosari. Nimeona ni chachu ya mimi kumpa moyo wangu wote, kumpenda zaidi na kumtunza kikamilifu.

Huyu binti sitaki nimuache, daima amekuwa akilini mwangu. Sijawahi kupenda namna hii.

Namuomba Mungu aliimarishe penzi letu hata tuufikie mwisho mwema
Safari njema.
 
Ni suala la muda tu ila sisi sote ni walemavu watarajiwa, kama unampenda kweli wewe kunjua moyo na uyaache mapenzi yafuate mkondo wake.
 
Kila la heri mkuu, hata mlemavu Ni binadamu Kama wengine na anahaki ya kupenda na kupendwa.
 
Ni kama umepanic baada ya kutokumwelewa kipenzi Analyse .......kulalamika alimaanisha yaan ni km unalalamika juu ya kumpenda binti mwenye ulemavu, au ni kama haujalalamika vile......
Kama nilimwelewa ama sikumwelewa, sikutaka yawe makubwa, nikaomba hisani yake, aendelee na shughuli zake nyingine za ujenzi wa taifa. Kwani kuna tatizo?
 
Hongera, kila lakheri zisiwe nyege tu ndo zinakufanya umpende alafu baadae umuache
 
Back
Top Bottom