Mapenzi ya mtandaoni yameniangushia kwa binti mwenye ulemavu, hakika huyu ndiye chaguo la moyo wangu

Mapenzi ya mtandaoni yameniangushia kwa binti mwenye ulemavu, hakika huyu ndiye chaguo la moyo wangu

Kwa muda mrefu nimekuwa mpweke ila siku za karibuni kwenye mtandao nikawa niko busy na dada mmoja mzuri sana.

Basi tukaona kuna haja ya sisi kuonana kwani niko Dar na Yeye yuko Dar. Tukapanga kukutana naye Slipway.

Ijumaa jioni baada ya saa za kazi nikawa nimepiga kambi Waterfront Bar, nikaangiza kinywaji changu huku nikimsubiri mrembo.

Haikuchukua muda mrefu, angaingia msichana mrefu mweupe. Nikamkaribisha kwa hug moja matata sana.

Ule ulemavu wa mkono wake uliokatwa baada ya yeye kupata ajali, kwangu sijaona kwamba ni kasoro wala dosari. Nimeona ni chachu ya mimi kumpa moyo wangu wote, kumpenda zaidi na kumtunza kikamilifu.

Huyu binti sitaki nimuache, daima amekuwa akilini mwangu. Sijawahi kupenda namna hii.

Namuomba Mungu aliimarishe penzi letu hata tuufikie mwisho mwema
Wao huwa hawanaga huruma. Yaani hawi na mtu kwenye mahusiano kisa Cha huruma. Na ndio Mana wakishapata mahala pazuri kukuacha yaani Ni within picosecond.

Hypergamy is baked into the female brain. It works ruthlessly and swiftly. If she sees a better option, she won't hesitate to jump from her current branch to a higher branch,
 
Hongera mkuu..ubarikiwe sana..Mungu akawape furaha daima
Unaona yule dada alieolewa na yule kaka anaetembea kwny wheel chair yani kiuno chini hawezi lolote but still ameolewa na wanaishi kwa raha nawafatilia instagram yao...Mungu anabariki na kuongeza kipato chao..na wana mtoto by now..so kila kitu kinawezekana...ni UPENDO TUU.....
 
Ishi nae tu, kikubwa upendo. Siku hizi kuna viungo vya bandia vya miili ya binadamu. Mkijaaliwa kuupata mkono mapenzi yatakuwa mara mia. Mungu awatangulie...[emoji120][emoji120]
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Tusiwe tunasema bas tukionana,tuwe tunasema tukioana au tusiseme kabisa
 
Kwa muda mrefu nimekuwa mpweke ila siku za karibuni kwenye mtandao nikawa niko busy na dada mmoja mzuri sana.

Basi tukaona kuna haja ya sisi kuonana kwani niko Dar na Yeye yuko Dar. Tukapanga kukutana naye Slipway.

Ijumaa jioni baada ya saa za kazi nikawa nimepiga kambi Waterfront Bar, nikaangiza kinywaji changu huku nikimsubiri mrembo.

Haikuchukua muda mrefu, angaingia msichana mrefu mweupe. Nikamkaribisha kwa hug moja matata sana.

Ule ulemavu wa mkono wake uliokatwa baada ya yeye kupata ajali, kwangu sijaona kwamba ni kasoro wala dosari. Nimeona ni chachu ya mimi kumpa moyo wangu wote, kumpenda zaidi na kumtunza kikamilifu.

Huyu binti sitaki nimuache, daima amekuwa akilini mwangu. Sijawahi kupenda namna hii.

Namuomba Mungu aliimarishe penzi letu hata tuufikie mwisho mwema
Kama umempenda huna haja ya kutaka hata ushauri. Kipendacho moyo dawa mwanangu. Ila uangalie mambo mengi zaidi ya sura na ulemavu. Wapo wengi wana ulemavu usioonekana kirahisi kama vile tamaa ya pesa au wale vijikabila vinavyopenda kufanya uzinzi na kila ndugu eti kwa kudumisha mila.
 
Back
Top Bottom