Dah! Basi hao wanaokupiga matukio wanakupiga matukio madogo mpaka somo alikuingii
Mimi nilipigwa tukio la kwanza mpaka moyo wangu ukabadilika kutoka wa nyama hadi kua wa chuma.
Sasa hivi sijui mtu anifanyie tukio gani la kuniliza.
Uzuri ulionao, elimu, moyo, tabia njema na kazi unayomiliki haikufai kumng'ang'ania mtu anayekusumbua.
Uzuri wote huo halafu unamlilia mtoto wa mtu!
Ebu jikaze vaa vizuri nenda Sehemu nzuri yenye watu wa maana kapate msosi huku unapulizwa na upepo.
jinsi upepo utakavyokua unakupuliza ndivyo na wewe umpulize huyo mtu atoke ndani ya moyo na akili yako. Kuna wanaume wazuri wa maana wanakusubiria huku nje.🥂