Mapenzi yawe ni ya muda maalumu tu ili kuepusha mateso ya kihisia ya muda mrefu

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Ushahidi unaonesha kuwa hata mapenzi yaanze kwa nguvu kubwa kiasi gani lakini bado kamwe hayatodumu na kubaki na nguvu hiyo hiyo kwa muda wote.

Inapotokea Wawili wamependana basi waingie makubaliano rasmi, kwa mfano wakubaliane kwamba wanahitaji uhusiano wao huo udumu kwa muda gani na iwapo basi baada ya muda huo kufika na wakaona bado wanahitajiana waingie makubaliano upya.

Kuwe na category za mapenzi, kwa mfano kama watahitaji Mtoto au Watoto au ni good time tu, kama Watahitaji kujumuisha familia zao au ni wao wawili tu, waainishe namna ya kuwatunza Watoto au Mtoto kama watapata, ikibidi kuwe kabisa na bima maalumu kwa ajili ya kuhakikisha elimu ya Mtoto/Watoto iwapo baadae kila mmoja ataamua kupita njia yake.

Ukifuatilia kwa makini hata kwa wale wanaoruhusu Ndoa za mitala mara nyingi Wanaume hutumia hiyo kama kichaka cha kuhalalisha kuwapa kisogo Wenza wao na kwenda kuanza mapenzi mapya...ni bahati mbaya sana hii humnufaisha Mwanaume zaidi na kumuacha Mwanamke njia panda.

Tunateseka kwa sababu tumekuwa Viumbe tunaopenda maisha ya kinafiki kupita kiasi, tupo tayari kusikia na kuishi uongo na tunauogopa ukweli...Mwenza wako anapokwambia anakupenda wewe jiulize atakupenda hivyo hivyo kwa muda gani?.

Mapenzi ya kudumu yabaki tu kati ya Watoto na Wazazi wao au Waumini na Viongozi wao wa kiimani, ie wanaoamini uwepo wa Mungu basi si mbaya kujiapiza huko lakini sio kwa Mwenza wako.

Hebu kaa chini usikilize wimbo kama huu wa "Lady in my life" wa Michael Jackson au nyimbo zote unazozijua zinazompamba Mwanamke na kumdadavua kama kitu cha thamani kuliko thamani yenyewe na bado huishia kulizwa, hivi ni Mwanamke gani asiyetamani kuambiwa maneno matamu hivi?...lakini swali kuu litabaki "Ni maneno ya kweli na ya kumaanisha?"...labda huenda ni ya kweli na ya kumaanisha lakini basi ni kwa wakati huo tu na haitokuwa hivyo muda wote.

LADY IN MY LIFE by MICHAEL JACKSON

"There will be no darkness tonight, lady our love will shine, Lighting the night, Just put your trust in my heart, and meet me in paradise, now is the time Girl, You are every wonder in this World to me, a treasure time won't steal away"

"So listen to my heart, lay your body close to me, let me fill you with my dreams, I can make you feel alright, and baby through the years, gonna love you more each day, so i promise you tonight, that you will always be the lady in my life".

Maneno kama haya hakika Mdada ukiambiwa utavimba kichwa, lakini jiulize itakuwa hivyo wakati wote au yata expire na yatahitaji kuambiwa tena mwingine?.

Wawili (Couple) muwe confortable kuambiana maneno yote matamu yaliyopo Duniani, kubembelezana, kudeka kwa kila mmoja lakini huku mkikubali kwamba hiyo halitobaki hivyo milele.
 
Nakubalibna na wewe mkuu, tatizo watu wa dini hawatakubali huu ukweli wako.

Wataishia kukwambia Mungu atatusaidia kudumu pamoja milele, wakati kila siku hata wachungaji tunaona wanaachana.
 
Ushahidi wa mapenzi ya milele umebaki kama ndharia ila kiuhalisia inawatesa sana Wanajamii.
 
Hapa hakuna ukweli wowote, Hakuna cha kupungua hisia Ni Tamaa na Ubinafsi unasumbua watu, kwani Mababu zetu waliwezaje kuishi mpaka uzeeni?

Inamaana Mungu aliyeumba ndoa hakujua kuwa kuna kupungua hisia ninyi saivi ndo wavumbuzi wazuri mmetoka chimbo na uvumbuzi wenu?

Maisha yenyewe Ni miaka 40 average (20-60) ndo mko active alaf ni kelele za kutosha, hv huamini kuwa kuna mapepo yanajishughulisha kuua ndoa?
 
Hizo tamaa ndiyo kupungua hisia kwenyewe mkuu.

Kwenye swala la "Mungu kuumba ndoa" napata ukakasi.
Mungu yupi huyo aliumba ndoa?

Yule wa waislamu aliwaruhusu kuoa wake wanne.
Huyu Mungu wenu karuhusu mke 1 kama mke wa dawa, hajaruhusu kuachana mpaka kifo.
 
Sasa Tamaa ni kwa sababu watu wamekuwa wanajiendekeza Sana, hawajali, hawana UPENDO.

Mungu ni mmoja tu Mkuu hiyo mingine ni miungu mkuu...
 
Sasa Tamaa ni kwa sababu watu wamekuwa wanajiendekeza Sana, hawajali, hawana UPENDO.

Mungu Ni mmoja tu Mkuu hiyo mingine ni miungu mkuu...

Sasa huyo Mungu wenu mbona ameshindwa kuwafanya watu "wasijiendekeze?"

Kwanini huyo Mungu wenu ameshindwa kuwawekea upendo watu ndani yao ili wasishikwe na tamaa?
 
Hapa hakuna ukweli wowote, Hakuna cha kupungua hisia Ni Tamaa na Ubinafsi unasumbua watu, kwani Mababu zetu waliwezaje kuishi mpaka uzeeni?

Inamaana Mungu aliyeumba ndoa hakujua kuwa kuna kupungua hisia ninyi saivi ndo wavumbuzi wazuri mmetoka chimbo na uvumbuzi wenu?

Maisha yenyewe Ni miaka 40 average (20-60) ndo mko active alaf ni kelele za kutosha, hv huamini kuwa kuna mapepo yanajishughulisha kuua ndoa?
Sasa kuna haja gani ya kumtamkia Mwenza wako kwamba yeye ameshika pumzi zako na bado unafika wakati hutaki kumuona.

Pointi yangu hapa ni tuache hizi kudanganyana ili hali tukijua hatumaanishi.

Ni bora muambiane ukweli kuwa tangu mmeonana amekuvutia hivyo unamuomba muwe wote kwa mwaka au miaka mtakayokubaliana, ule mvuto uki expire basi kila Mtu achukue ustaarabu wake badala ya kuanza kutukanana na kutishiana kuuwana.
 
Sasa huyo Mungu wenu mbona ameshindwa kuwafanya watu "wasijiendekeze?"

kwanini huyo Mungu wenu ameshindwa kuwawekea upendo watu ndani yao ili wasishikwe na tamaa?
Kazi ya Mungu sio kukufanya, amekupa uhuru uamue utakutana nae kule mbele siku ya hukumu...
 
Amempa nani uhuru wa kuamua?

Mimi sijapewa uhuru wa kuamua.

Uhuru gani huo wa kuamua halafu baada ya kuamua aliyekupa uhuru wa kuamua akuchome moto eti kisa "hukuamua kwenda kwake"
Huo siyo uhuru.

Uhuru wenyewe ungekuwa hivi, anayeenda kwa Shetani aende,
anayeenda kwa Mungu aende pia. baada ya hapo hakuna cha vitisho tena.
kila mtu atunze watu wake.

Sasa mambo ya kusema "ukienda kwa shetani nitakuchoma moto" uhuru gani huo sasa?
 
Hapa hakuna ukweli wowote, Hakuna cha kupungua hisia Ni Tamaa na Ubinafsi unasumbua watu, kwani Mababu zetu waliwezaje kuishi mpaka uzeeni?

Inamaana Mungu aliyeumba ndoa hakujua kuwa kuna kupungua hisia ninyi saivi ndo wavumbuzi wazuri mmetoka chimbo na uvumbuzi wenu?

Maisha yenyewe Ni miaka 40 average (20-60) ndo mko active alaf ni kelele za kutosha, hv huamini kuwa kuna mapepo yanajishughulisha kuua ndoa?
Kusema kirahisi tu kwamba ndoa za mababu zetu zilidumu bila ushahidi wowote unatupa wakati mgumu kukuamini . Huenda babu na bibi yako uliwaona wako pamoja uzeeni we ukaweka conclusion Kwamba ndoa za zamani zilidumu
 
Labda una silka ya ubishi ila inajulikana ndoa za zamani zilidumu...

Ndoa kudumu ni akili za wanandoa wote ku'fix' matatizo na sio kuyakimbia...

Siku hz watu hawako tayar kutatua changamoto wao ni kukikmbia tu...
 
Amempa nani uhuru wa kuamua?

Mimi sijapewa uhuru wa kuamua.

Uhuru gani huo wa kuamua halafu baada ya kuamua aliyekupa uhuru wa kuamua akuchome moto eti kisa "hukuamua kwenda kwake"
Huo siyo uhuru.

Uhuru wenyewe ungekuwa hivi, anayeenda kwa Shetani aende,
anayeenda kwa Mungu aende pia. baada ya hapo hakuna cha vitisho tena.
kila mtu atunze watu wake.

Sasa mambo ya kusema "ukienda kwa shetani nitakuchoma moto" uhuru gani huo sasa?
Mkuu, hv gari inayotumia diesel umeambiwa na mtengenezaji kuwa ukitumia petrol halitofanya kazi, ikiwa unajali na unapenda gari lako Ni kwann ulazimishe kutumia Petrol...
 
Huyo mtengenezaji wa gari ni bora mara elfu kuliko Mungu.

Zipo gari mbili, diesel na petrol, ni uhuru wangu kuchagua gari la petroli au dieseli.

nikichagua gari la petrol ni juu yangu, nikichagua la diesel ni sawa pia.
huo ndiyo uhuru sasa.

ila mtengenezaji angeniambia kuwa, "chagua gari moja kati ya haya, usipochagua gari la petrol nitakuchoma moto"
hapo angekuwa hajanipa uhuru,
na hicho ndicho alichofanya mshikaji wenu Mungu.
yaani kama hujamchagua yeye eti atakuchoma jehanamu.
sasa huo si ujinga.
 
Mkuu hata ikiwa una hasira labda kutokana na mapito katika maisha yako, si vyema kumuita Mungu mshkaji...

Binadamu tunabadilika huenda mwezi ujao ukarudi kutazama post yako na ukajichukia...

Uhuru umepewa kwa maana unapomfuata shetani utakuwa mahali atakapokuwepo. Uhuru unao...
 
Mapito kila mtu anapitia kwa namna yake mkuu!
Mimi simlaumu mungu kwa lolote lile,
nimlaumu vipi wakati hayupo?
Mimi mungu hajawahi kunisaidia wala sina shida naye kwa chochote kile.
Mara zote nikipata matatizo wanadamu ndiyo hunisaidia.
Mimi naishi maisha yangu mwenyewe,
Ili niishi nayategemea mazingira yanayonizunguka na siyo huyo mshikaji wenu uchwara.
 
Back
Top Bottom