Mapigano makali yaibuka mpakani na Israel. Makombora ya Hamas yatua miji ya kusini ya Israel huku makubaliano mapya kuhusu misaada ikifikiwa

Weweee ni mwoga balaaa hata kovu la kiwembe mwilini mwako hakuna
Heheeee [emoji3]
Nakumbuka kuna mwaka wakati nipo zangu chuo
Natoka zangu nipo njiani sina hili wala lile kulikua na maandamano
Kinondoni makaburini pale nilishuka ghafla nasikia mabomu nilichapa mbio asee zabalaa maana sikutegemea kwakweli nikaingia ndani nyumba hata siijui
Kufika mule wenyewe wanakula pilau na juisi safi kabisa mida kama hii
Nikaambiwa vipi kijana nikawaambia natoka zangu chuo naona mabomu yanarindima nimekuja kujistiri
Nikasikia grace (jina silikumbuki ila walikua wakristo) leta glass moja na sanahani tumepata mgeni
Wenyeji kama waliona tumboni nikaekewa mzigo wakutosha nikaubonda pale mzee yule akanambia ngoja ngoja kidogo hapa patulie
Kweli kama saa nane kasoro kidogo nikasepa zangu
Allah ampe khairat yule mzee na familia yake
Vita sio maskhara mzee [emoji3][emoji1787][emoji3]
 
Sisi wabongo bado Sana kwenye violence
 
Tukiacha na ushabiki hawa HAMAS wanatisha Sana sidhani kama kuna kundi lingine wanaweza KUPIGANA huku wameshikia mateka kwa zaidi ya miezi 3... kwasababu eneo ambalo wanapigana vita ni dogo sana kama wilaya ya kigamboni lkn Israel anahangaika nao mwanzo mwisho
Nawakubali sana Hammas na Taleban hao ni noma sana
 
Tukiacha na ushabiki hawa HAMAS wanatisha Sana sidhani kama kuna kundi lingine wanaweza KUPIGANA huku wameshikia mateka kwa zaidi ya miezi 3... kwasababu eneo ambalo wanapigana vita ni dogo sana kama wilaya ya kigamboni lkn Israel anahangaika nao mwanzo mwisho
Eneo hilo halina milima mikubwa wala misitu.Zaidi ni hayo mahandaki waliyojenga.
Kinachoshangaza ni kuwa wamezingirwa kwa miezi 3 na sasa ndio wamekatiwa kila kitu.
Naamini mwenye njaa anakuwa mkali zaidi kuliko aliyeshiba.
 
Vita ni mbinu na mikakati Leo hii kundi ambalo lilikuwa linaonekana si lolote si chochote, linamtoa jasho moja ya majeshi bora kabisa duniani.[emoji3]

Hili la Hamas linanikumbusha jinsi Wasomali walivyo wafurusha majeshi ya USA katika ardhi yao.
Kwa Somalia ilikuwa ni tukio moja tu ambapo waliangusha helkopta ya Marekani na walipozikokota maiti za wamarekani mtaani ndio ikawa shida kule Marekani na wakaamua kujiondokea zao.
Hamas bwana !.Wanapiga mpaka vifaru vya ghali na vya kisasa kwa RPG tu.
Mwanzoni kuna watu hawakuamini lakini sasa wengi wamejionea wenyewe kwa macho yao na waisrael wamethibitisha.
 
Tukiacha na ushabiki hawa HAMAS wanatisha Sana sidhani kama kuna kundi lingine wanaweza KUPIGANA huku wameshikia mateka kwa zaidi ya miezi 3... kwasababu eneo ambalo wanapigana vita ni dogo sana kama wilaya ya kigamboni lkn Israel anahangaika nao mwanzo mwisho

Kupigana na magaidi yaliyoahidiwa bikira peponi ni vita ngumu sana!

Kenya na alshabaab mpaka leo wameshindwa kuwamaliza, Bokoharam kule Nigeria bado wanatamba.

Iran pamoja na kuwa mfadhili mkuu wa ugaidi duniani lakini bado anasumbuliwa na ISIS pamoja na Jaish Ul Adl.
 
Kaeneo kama Kigamboni ila kana utitiri wa watu isingekuwa huruma ya IDF kuepusha maafa kwa raia basi wiki nyingi Hamas wote wangekuwa kuzimu wananehemeka na bikra zao
 
Hawa hamas mipango yao waliipanga vipi, kaeneo kadogo kama gaza, jeshi kubwa la israel imeshindwa kupata mateka mpaka leo.
Mji umegeuzwa kifusi lakini bado unasikia wanashambulia.. Wapo gaza kweli hawa.!? [emoji848]
Lakini mimi najiuliza hawa Hamas mahesabu yao waliopiga yapo vizuri kweli thamani ya wapalestina 24000 waliouawa na 75% ya gaza iliyoharibiwa ni sawa na mateka 130 na wayahudi 1200 waliowaua?
 
Vita ni mbinu na mikakati Leo hii kundi ambalo lilikuwa linaonekana si lolote si chochote, linamtoa jasho moja ya majeshi bora kabisa duniani.[emoji3]

Hili la Hamas linanikumbusha jinsi Wasomali walivyo wafurusha majeshi ya USA katika ardhi yao.
Mbona huwasifii Ukraine walivyo wabishi kuitetea ardhi yao kwa mrusi hadi leo kashindwa kumaliza vita
 
Lakini mimi najiuliza hawa Hamas mahesabu yao waliopiga yapo vizuri kweli thamani ya wapalestina 24000 waliouawa na 75% ya gaza iliyoharibiwa ni sawa na mateka 130 na wayahudi 1200 waliowaua?
Naimani walijua kabisa balaa litakalokuja.
Hata mimi hapa kwa kigaza kile sioni ajabu alichofanya palestina, kwa nguvu zile za kijeshi utegemee eti kaGAZA kale kasiharibiwe.

Shida kwa kiGAZA kile kilivyo kidogo na ubora wa jeshi la israel nilitegemea saa hizi aidha gaza wameshaichukua HAMAS hawapo ama wameshapata mateka ama vyote.
Au HAMAS hao mateka wameficha nchi nyingine? 🤔
 
Kupigana na magaidi yaliyoahidiwa bikira peponi ni vita ngumu sana!

Kenya na alshabaab mpaka leo wameshindwa kuwamaliza, Bokoharam kule Nigeria bado wanatamba.

Iran pamoja na kuwa mfadhili mkuu wa ugaidi duniani lakini bado anasumbuliwa na ISIS pamoja na Jaish Ul Adl.
Magaidi nahisi Wana mioyo tofauti na hii ya kwetu
 
Mbona huwasifii Ukraine walivyo wabishi kuitetea ardhi yao kwa mrusi hadi leo kashindwa kumaliza vita
Kwa kulinganisha basi ujasiri wa Hamas bado hauna mfano wake.Kidogo inaweza kuwa ni jeshi la Vietnam.
Ukraine wanapata misaada ya mapesa na silaha bora kutoka Marekani.Ni nchi imepoteza maeneo muhimu ya kiuchumi lakini bado ina mipaka mingi ya kupokelea silaha
Ama kwa Hamas katika miezi hii mitatu hakuna msaada ulioingia kwao zaidi ya dua kutoka kwa waislamu.Halafu zaidi ya hayo hata wanachokula na kunywa hakieleweki.
Wapiganaji wa ukraine kule Azovstal hatimae walitoka chini ya kiwanda cha chuma walikokuwa wamejificha na kujisalimimisha kwa jeshi la Urusi,Hicho kitu hakijaonekana kwa Hamas.Huwa hawajulikana kama wako hai au wamekufa kwenye mahandaki yao lakini anayekuja juu anatoka na bunduki kuwatafuta majeshi ya Israel
Huo ni ushujaa haujapata kutokea na si kawaida,
 
Back
Top Bottom