Mapinduzi Afrika: Wananchi wengi wanapenda Utawala wa Kidemokrasia kuliko wa Kijeshi, hawapendi Mapinduzi

Mapinduzi Afrika: Wananchi wengi wanapenda Utawala wa Kidemokrasia kuliko wa Kijeshi, hawapendi Mapinduzi

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Afrika imekumbwa na msururu wa mapinduzi ambayo yanatishia kuirudisha nyuma miaka ya 1980 na enzi za utawala wa kijeshi.

Burkina Faso, Chad, Guinea, Sudan na Mali zote zimeshuhudia serikali ikipinduliwa na nafasi yake kuchukuliwa na jeshi.

Hali inaweza kuwa ya kutisha zaidi, kwa sababu majaribio yaliyofeli ya mapinduzi yameripotiwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na siku chache zilizopita, Guinea-Bissau.

Kwa kila nchi ambayo inaongezwa kwenye orodha hii, sauti zinazodai kuwa demokrasia haifanyi kazi - na haiwezi kufanya kazi - katika Afrika inakua zaidi.

Kwani, kupinduliwa kwa marais wa kiraia kulifuatiwa na sherehe za mitaani katika baadhi ya nchi huku wananchi wakishangilia kuangushwa kwa viongozi waliochaguliwa.
Maelezo ya video,

Mapinduzi Afrika

Lakini wakati inajaribu kutafsiri mfululizo wa mapinduzi kama ushahidi kwamba demokrasia katika Afrika inakufa, hilo litakuwa kosa.

Hata katika nchi ambazo mapinduzi yamefanyika, wananchi wengi wanataka kuishi katika demokrasia na kukataa utawala wa kimabavu.

Zaidi ya hayo, licha ya kuchoshwa na jinsi siasa za vyama vingi zinavyofanya kazi, kwa wastani demokrasia huzalisha ukuaji wa juu wa uchumi na kufanya kazi nzuri zaidi ya kutoa huduma za Umma, kulingana na utafiti katika Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani.

Kinyume chake, tawala za kijeshi zina historia ndefu ya kutumia vibaya haki za binadamu huku zikishababisha mdororo wa kiuchumi.

Wafuasi hawa wa timu ya soka ya Mali walishikilia picha ya kiongozi wa mapinduzi Kanali Assimi Goita kabla ya mechi ya hivi majuzi ya Kombe la Mataifa ya Afrika. (AFP)

Kwa njia nyingine, Afrika inaweza na inapata faida ya kidemokrasia - tatizo linakuja pale viongozi wanaodaiwa kuwa wa kidemokrasia wanaanza kutumia mikakati isiyo ya kidemokrasia kujiweka madarakani kinyume na matakwa ya watu wao.

Hili ni jambo muhimu. Katika nchi kama Guinea na Mali, viongozi hawakupoteza umaarufu kwa sababu walianzisha demokrasia ya kweli ambayo ilishindwa kwa sababu mfumo huu wa serikali hauendani na hali halisi ya Kiafrika.

Badala yake, marais walipuuza uungwaji mkono kwa sababu walidhoofisha sifa zao za kidemokrasia katika muktadha wa kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu na - katika yaliyojiri Burkina Faso na Mali - uasi wa kijihadi.

Hili linadhihirika iwapo tutavuka vichwa vya habari kuuliza ni kwa nini baadhi ya mapinduzi ya hivi majuzi yamesherehekewa hadharani.

Nchini Guinea, Rais wa zamani Alpha Condé alibadilisha katiba kwa utata mwaka 2020 ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu madarakani.

Huu ulikuwa mkakati usiopendwa na watu wengi, hasa kwa sababu si kura ya maoni ya katiba au uchaguzi mkuu ambao alishinda ambao ulikuwa huru na wa haki.

Bw Condé pia alizidi kuwa mtu wa kimabavu katika miezi iliyotangulia mapinduzi, akiwafunga jela na kusababisha ghasia dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa na wanaharakati wanaoipinga serikali.

Vile vile, Rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta alishutumiwa kwa udanganyifu katika uchaguzi wa wabunge wa 2020.

Mbali na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ufisadi na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, hii ilidhoofisha uhalali wake wa binafsi.

Katika nchi zote mbili, viongozi wa kiraia walipoteza umaarufu kwa sehemu kwa sababu walitoka kwenye demokrasia, sio tu kwa sababu raia walipoteza imani nao.

Kwa hakika, inaeleza kwamba ingawa watu wengi waliunga mkono mapinduzi yaliyowaondoa Bw Condé na Bw Keïta, tafiti za hivi karibuni zaidi zilizofanywa na Afrobarometer ziligundua kuwa 76% ya Waguinea na 70% ya Wamali wanakataa utawala wa kijeshi.

Kwamba tafiti hizo hizo pia zimegundua kuwa uungwaji mkono wa demokrasia uko katika 77% nchini Guinea, 70% Burkina Faso na 62% nchini Mali - ushahidi zaidi kwamba raia waliunga mkono uingiliaji wa kijeshi kwa matumaini kwamba ingefungua njia kwa njia bora zaidi ya serikali ya kiraia, si kwa sababu wanatamani kuishi chini ya utawala wa kimabavu.

Kwa kweli, pale ambapo mapinduzi yameonekana kunyakua michakato ya demokrasia, yamekuwa hayapewi umaarufu mkubwa.

Waandamanaji wa Sudan wanaendelea kuhatarisha maisha yao kutaka kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi

Nchini Sudan, kwa mfano, maelfu ya watu waliingia barabarani kuandamana kupinga unyakuzi wa mamlaka ya kijeshi mwaka wa 2021 ambao ulidhoofisha uhamishaji wa madaraka mikononi mwa raia kufuatia kuondolewa kwa kiongozi wa muda mrefu Omal al-Bashir mwaka wa 2019.

Licha ya ukweli huo,kwamba mamia ya watu wamejeruhiwa na takribani 79 kuuawa, watu wa Sudan wanaendelea kudai haki zao za kidemokrasia.

Sababu moja kwamba demokrasia inaweza kubaki kuwa mfumo wa kisiasa unaopendelewa kwa jamii nyingi za Kiafrika - hata katika nchi ambazo bado haijafikiwa - ni utendaji mbaya wa serikali za kimabavu.

Rwanda mara nyingi inatajwa kuwa mfano wa kile cha "mtu mwenye nguvu" anaweza kufanya katika muktadha wa Afrika - kuleta ukuaji wa uchumi na kupunguza rushwa.

Rwanda ni kitovu cha teknolojia ya hali ya juu lakini hakuna nafasi ya kuikosoa serikali

Kwa ujumla, ukosefu wa uwajibikaji unaotokea chini ya madikteta na tawala za kijeshi husababisha rushwa kubwa na sera ya kiuchumi isiyofaa.

Kwa hiyo, kwa wastani demokrasia za Kiafrika hufikia viwango vya juu vya ukuaji wa uchumi huku zikifanya kazi nzuri zaidi ya kutoa huduma za umma.

Pia wana uwezekano mdogo wa kukumbwa na migogoro inayoharibu na kufanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Utendaji mbaya wa aina za serikali za kimabavu katika ardhi ya Afrika, na hamu ya ulimwenguni pote ya kuwa na sauti katika maamuzi yanayoathiri maisha yetu wenyewe, inasaidia kueleza ni kwa nini uungwaji mkono wa demokrasia unabaki juu.

Kwa upande mwingine, hii ni sababu moja kwamba jeshi kwa kawaida huhalalisha vitendo vyao kwa kudai kwamba zilinuiwa kurejesha utawala wa sheria na kuokoa demokrasia kutoka yenyewe.

Sababu nyingine bila shaka ni haja ya kujaribu na kuepuka kulaaniwa na vikwazo vya kimataifa kwa kuahidi kurejea chaguzi za vyama vingi na utawala wa kidemokrasia.

Hata hivyo kwa kushawishi demokrasia kwa utekaji wa kijeshi halali, wapangaji mapinduzi wanaunda fimbo kwa migongo yao wenyewe.

Katika matukio mengi, ingawa si wote, viongozi wapya wa kijeshi huishia kuchelewesha kurejea kwa utawala wa kiraia.

Katika baadhi ya matukio, hii ni kwa sababu wanafurahia manufaa ya binafsi ya kuwa mamlakani na hawataki kuwaacha.

Katika mengine, ni kwa sababu wana miradi ya kisiasa wanayotaka kukamilisha ambayo inachukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Hata hivyo baada ya kuahidi kuandaa njia kwa ajili ya serikali imara zaidi na shirikishi, jambo hili bila shaka linakatisha tamaa wananchi wanaounga mkono demokrasia hadi pale viongozi wa mapinduzi wenyewe wanapokabiliwa na hatari ya kupinduliwa.

Udhibiti wa kijeshi hauwezekani kutoa njia ya ufanisi na hii ni hatari, kwa sababu kila mapinduzi hudhoofisha taasisi za kidemokrasia na kurejesha nguvu ya bunduki badala ya nguvu ya sanduku la kura.

Kwa hiyo kutafuta njia ya kuondokana na hali ya sintofahamu na usalama kutahitaji kujenga taasisi imara za kidemokrasia zinazoweza kustahimili ghilba za viongozi wa kisiasa, si za kimabavu zinazowatenga wananchi na kwenda kinyume na matarajio yao.

Leonard Mbulle-Nziege ni mchambuzi wa utafiti katika taasisi ya Africa Risk Consulting (ARC) na Nic Cheeseman ni profesa wa demokrasia katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

Chanzo: BBC
mapinduzi Afrika.png
 
Afrika imeshindwa kuwa na mifumo thabiti ya kisiasa inayoweza kuwafanya watawala wawajibike kwa wananchi na badala yake watawala wanajiona kama miungu watu.

Afrika bado tuna watawala walioko madarakani pasipo na ridhaa kamili ya wananchi au kama ipo basi ni ridhaa feki kwani wako madarakani kutokana na chaguzi bandia wanazoandaa na kusimamia wenyewe.

Kwa mantiki hiyo basi ni vigumu sana kwa mapinduzi ya kijeshi kumalizika katika bara hili hali ambayo itaendelea kuwepo mpaka tutakapokuwa na mifumo thabiti ya kiutawala na sio hii ya kumfanya mtawala aonekane kama Mungu.
 
Afrika imeshindwa kuwa na mifumo thabiti ya kisiasa inayoweza kuwafanya watawala wawajibike kwa wananchi na badala yake watawala wanajiona kama miungu watu.

Afrika bado tuna watawala walioko madarakani pasipo na ridhaa kamili ya wananchi au kama ipo basi ni ridhaa feki kwani wako madarakani kutokana na chaguzi bandia wanazoandaa na kusimamia wenyewe.

Kwa mantiki hiyo basi ni vigumu sana kwa mapinduzi ya kijeshi kumalizika katika bara hili hali ambayo itaendelea kuwepo mpaka tutakapokuwa na mifumo thabiti ya kiutawala na sio hii ya kumfanya mtawala aonekane kama Mungu.
Kwa Mara ya Kwanza umeongea pointi.usiwashabikie hao NATO wenyewe wanapenda waafrika wawe kwenye hii Hali ili wawe wanachota rasilimali kirahisi.
 
Tunapenda uongozi tunaouweka wenyewe kwa ridhaa yetu ya wengi kwa njia ya kupiga kura na sio kutawaliwa.

Mambo ya utawala yaliisha mara baada ya kupata Uhuru.
 
Back
Top Bottom