Mapinduzi Cup: Waandishi wa habari za michezo mnatia aibu,pamoja na wale wa Azam media

Mapinduzi Cup: Waandishi wa habari za michezo mnatia aibu,pamoja na wale wa Azam media

Acheni Ulimbukeni nyie pimbi. Kwani mmeambiwa Azam anarusha Matangazo kwa Kiingereza???
Nendeni CNN ya Marekani mtutajie Watangazaji wanaojua Kiswahili basi maaana naona mishipa ya Shingo imewatoka sana.
Unapishana na uelekeo wa dunia mkuu
 
Kwa nini tusiwe kama Uingereza?
Kocha au mchezaji ukisajiliwa Tanzania lazima ujifunze kiswahili.
England hakuna kocha au mchezaji anayehojiwa kwa lugha yake, lugha ni moja tu, English.
Antonio Valencia wa Manchester United amekaa miaka 10 na mpaka anaondoka hakuwahi kujua kiingereza
 
Acheni Ulimbukeni nyie pimbi. Kwani mmeambiwa Azam anarusha Matangazo kwa Kiingereza???
Nendeni CNN ya Marekani mtutajie Watangazaji wanaojua Kiswahili basi maaana naona mishipa ya Shingo imewatoka sana.
Upimbi siachi, Azam wanarusha matangazo ya mpira kwa lugha ya kiswahili na kiingereza baadhi ya mechi kama ulikua haujui.

Mechi ikimalizika kwa upande wa kiswahili sasa wanaenda kuwahoji makocha, unakuta anataka aulize jambo flani anakwama kuuliza anaishia kujikanyaga kanyaga tu hadi makocha wanawacheka mfano ni Lwandamina & "Uchebe"
 
Kwa anayefuatilia michuano ya Mapinduzi Zanzibar atakuwa shahidi wa hili,post match interview kwa makocha,hasa mfano wa yule wa Azam,George Lwandamina anayetumia lugha ya malkia (English),waandishi wanashindwa kumuuliza maswali na hata wakimuuliza unaona kinyaa kabisa ukizingatia inakuwa Live.

Najiuliza mtu kama mwandishi wa habari unashindwa hata kuangalia wanachofanya wenzio kwenye vituo vikubwa vinavyorusha mchezo wa mpira? Nikweli hiyo lugha si yetu ila kwanini hata usijiandae kwa maswali yako mawili au matatu......yaani wanamuuliza maswali Lwandamina mpaka anacheka kwasababu hayaeleweki.Kuna vijana wengi wenye uwezo mzuri sana mtaani wapo,hasa nyie Azam media fanyeni recruitment vizuri,mnatia aibu sana inapotokea mahojiano na asiye mswahili.

Na nyie waandishe acheni uvivu,jifundisheni basi......saizi dunia ni kama kijiji ingieni You tube huko mjifunze.
Kilikuja na melikebu hicho cha malkia.
 
Ni mjanja anaongea english ili asiulizwe maswali tatanishi
 
Back
Top Bottom