Ok
Nimesoma hiyo link yako. Nimeona pia kuwa Kenya wanatumia Usd 1.3billion kujenga plant huko Mombasa. Hiyo itazalisha ton 84,000 kwa mwaka. Mahitaji ya Kenya ni 480,000 kwa mwaka. Hii inaonyesha mahitaji ni makubwa kuliko upatikanaji wa steel. Hapo hapo wamesema serikali ya Kenya inahamasisha uwekezaji kwenye kuchimba iron ore ndani mwao.
Hii kitu haiwezi kutushinda. Chuma ghafi tunacho na makaa tunayo. $1.5 bln haiwezi kutushinda. Hapo kwenye kuzalisha umeme, kishistoria viwanda vya chuma huwa havihitaji umeme. Labda siku hizi vimekuja vipya ambavyo vinateknolojia kubwa au viko automated.
Tunaweza kuzalisha chuma na faida yake ni kubwa sana. Zamani haikuwezekana kujenga majengo marefu wala madaraja imara. Jamaa anaitwa Carnegie akaumiza kichwa jinsi ya kupata chuma imara. Akaenda kwa wataalamu akakuta wanatengeneza steel lakini njia waliyokuwa wanaumia ilikuwq ya gharama sana hivyo waliweza tengeneza steel kwaajili ya vijiko, visu na vitu vidogovidogo. Aliwaambia kama anaweza pata chuma imara hivyo kwaajili ya Daraja. Wakamwambia gharama yake itakuwa kubwa sana. Akawaambia watafute njia ya kuzalisha kwa bei ndogo. Wakaingia kazini.
Wakatoka na majibu yaliyowezesha madaraja ya chuma na skyscrapers kuwepo hadi leo. Penye nia pana njia. Tunajua kabisa tunahitaji chuma, lazima tukizalishe kwa njia yoyote ile. Umuhimu wa kuzalisha chuma ni kama kuzalisha umeme au kujenga barabara, vinaonekana kama ni gharama kubwa lakini hufunguq maelfu ya fursa.
Hizi ndio 'mindsets' za hatuwezi!
Mkuu, inaelekea hujui kuwa hicho chuma cha Liganga na mkaa wa Mchuchuma ni mradi uliotakiwa uwe tayari unazalisha vifaa hivyo siku nyingi tu kama urasimu ungepigwa marufuku kuuchelewesha,; kwani wawekezaji walisha-'commit' kuutekeleza siku nyingi. NDC na mChina walikuwa tayari kuutekeleza mradi huo. Haieleweki vikwazo vinatoka wapi hasa!
Being "realistic" sio sababu ya kuwa na uoga wa kufanya jambo linaloonekana lina mafaa makubwa kwa taifa.
Kwani "economies of scale" zinapatikana huko Australia pekee, sisi hatuwezi tukatumia 'economic advantages' nyingine katika bidhaa hiyo ili tushindane katika soko la chuma?
Soko la Afrika yote hii hatuwezi kulitumia kwa kupata soko hilo kupitia AfCFTA?
Hakuna anae kataa umuhimu wa huo uwekezaji alikadhalika hili sio swala la chicken and egg conundrum, which appeared first.
Mwingine anadai kuna wawekezaji walijitokeza as far as I know wachina Mchuchuma walikuwa interested na makaa ya mawe for importation purposes ila sio kujenga kiwanda cha chuma na kama wangekuwa na nia izo sidhani kama wangezuiwa or else leta ushahidi hata wa article.
Having said that ndio maana nikasema nyie watu inabidi muwe realistic mtu anaona article inasema kiwanda cha chuma huko halipo quote vimetumia gharama za $1.3-1.5 billion + uwekezaji wa umeme kwenye icho kiwanda cha Nigeria na ndio kwanza vinauwezo wa kuzalisha tonne 20K kwa mwezi.
Ujenzi wa SGR yote mpaka kuisha ni $3billion dollars mpaka sasa hata nusu atujafika serikali hoi, huyo anaetuambia kila siku tunajenga kwa hela zetu siku hizi anawaambia wachina mtu-kopeshe tumalize mradi wazi wazi.
Halafu nyie mna suggest serikali ingetumia kwanza almost $1.5 billion kujenga reasonable size steeel plant, ikimaliza hapo itafute hela za kujenga SGR huku ikiwa na deni ambalo inabidi itafute vyanzo vingine vya mapato kuligharamia, wakati ikianza kujenga SGR mradi ukiisha unaanza kuwaingizia mapato na kuna direct effects za kuchochea uchumi mahala utakapo pita kuwaongezea mapato mengine ya kodi na kulimudu deni.
Unaanza kutambaa, kusimama na mwisho kutembea and not otherwise; kwa mapato ya sasa we have to prioritise.
Zama za kina Andrew Carnigie watu hela walikuwa wanatengeneza wenyewe wakishirikiana na private kama hakina Morgan Stanley ndio maana ikawa raisi hao watu kufanya hiyo miradi. Hata kesho US wakiingia vitani wana amuru tu central banks zao kuchapa notes, wanunua silaha na kuingia vitani sisi hatuna uwezo huo.
South Africa one of biggest producers wa iron ore kashindwa tengeneza icho kiwanda cha kuhudumia soko la Africa iwe sisi kwa hali yetu ya sasa.
Sisemi atukihitaji hiko kiwanda ila kwa uchumi wetu wa sasa hizo hela can yield better return in other investments to propel growth for now; huko mbele sawa.