Brelim Skoro_
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 15,188
- 37,742
Iwe inablock Matusi asee ...maana kuna Bwana mmoja huyo ni Kiwanda kikuu cha matusi humu ndani.
Je, umewahi kujiuliza mustakabali wa mijadala yetu hapa JamiiForums utakuwaje? Fikiria ulimwengu ambapo kuandika hoja nzito, kufanya utafiti wa kina, na kujibu mada mbalimbali kunakuwa rahisi, haraka, na kwa ubora wa kiwango cha juu zaidi.
Mimi na wenzangu (timu nzima) tunayo furaha kuwatangazia kuwa kuanzia wikendi hii, tunaleta mapinduzi hayo mikononi mwenu! Tunazindua zana mpya za Teknolojia ya Akili Unde/Mnemba (AI) hapa jukwaani.
Lengo letu si kubadilisha asili ya mijadala yetu inayoongozwa na binadamu, bali ni kuwapa uwezo zaidi ili kufanya mazungumzo yenu kuwa hai na yenye tija zaidi.
Zana hizi mpya zimeundwa kuwa rahisi sana kutumia na zitawapa faida zifuatazo mara moja:
1) Majibu Mahiri na Msaada wa Papo Hapo: Pata mapendekezo ya haraka ya kujenga hoja zako na msaada wa kimawazo unapokwama kuandika. Zitaokoa muda wako sana!
2) Utafiti wa Haraka: Kusanya taarifa na ukweli (facts) kwa haraka zaidi bila kulazimika kuondoka kwenye uzi.
3) Uchambuzi wa Picha: Unaweza kuweka picha na AI yetu ikakusaidia kusoma na kuchambua yaliyomo ndani yake kwa kina.
4) Kutengeneza Picha: Unahitaji picha maalum kusindikiza bandiko lako? Sasa utaweza kuiagiza AI itengeneze picha papo hapo kulingana na maelezo unayoyatoa. Hapa, inabidi uelewe 'prompt engineering' kwa kiasi ili kupata matokeo chanya.
Kingine kilichopo, ni kurahisisha kwa wageni kufanya translation ya mjadala instantly kwa lugha wanayoelewa.
Pia, kuna kuandaa kufanya summary ya mjadala mzima kwa mtu ambaye anakuta ameachwa ili ajue nini kinajadiliwa ili aweze ku-engage accordingly.
Tungependa wanajamvi wote mpate nafasi ya kufurahia mabadiliko haya.
Tunaomba mzijaribu kwenye mada zenu kisha mtupatie mrejesho wa kweli kabisa—iwe ni sifa, changamoto mlizokutana nazo, au mapendekezo ya nini tuboreshe. Tafadhali, weka maoni yako yote kwenye huu uzi maalum. Mawazo yako yanatusaidia kuboresha zaidi.
Asanteni kwa kuendelea kuifanya JamiiForums kuwa sehemu bora na salama kwa fikra huru. Tukutane kwenye mijadala wikendi hii!
Nawatakia wakati mwema.
Nadhani tushirikiane to push our Govt kuondoa such restrictions sio kwa JF tu bali kwa mitandao yote.Bwana Max Mello ni lini tutatumia Jf bila vpn ???
Bwana, bwanaaaa so far akili unde iko vizuri kwenye hizi AI suggestions za replies, hata kwenye mambo yetu ya raha haipo nyuma.Karibu mkuu wangu.
Asante kwa mrejesho
Nadhani tushirikiane to push our Govt kuondoa such restrictions sio kwa JF tu bali kwa mitandao yote.
Tunajaribu upande wetu, ila nanyi wananchi msichukulie kama ni jambo la
Sawa mkuu nimekuelewa,vipi mkuu hauna buku hapo mkuu kidogo nipate kuishi mwana jf mwenzio mkuu??.!!Nadhani tushirikiane to push our Govt kuondoa such restrictions sio kwa JF tu bali kwa mitandao yote.
Tunajaribu upande wetu, ila nanyi wananchi msichukulie kama ni jambo la kuachwa lipite tu.
Si ungemuomba ajira Ana kampuni ujue eehSawa mkuu nimekuelewa,vipi mkuu hauna buku hapo mkuu kidogo nipate kuishi mwana jf mwenzio mkuu??.!!
Sawa mkuu,mi nataka buku tu mkuu…Si ungemuomba ajira Ana kampuni ujue eeh
Kwahiyo Ajira au kazi hutaki mkuu ?Sawa mkuu,mi nataka buku tu mkuu…