Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

sasa nimeelewa rasmi kuwa mapinduzi ya zanzibar hayakuletwa na nyerere wala rafiki yake karume kumbe yaliletwa na mwanamapinduzi john okero mzanzibar mwenye asiri ya uganda nyerere na karume nao pia walimpindua okero kijanja
 

Activisty,
Watu walokuwa karibu na Okello na wanamfahamu vyema hawaamini kama
kitabu kile kaandika yeye.
 
Historia hii ni kwa mujibu wa CUF haijulikani kwngneko ni ujinga kuiamini
 
Activisty,
Watu walokuwa karibu na Okello na wanamfahamu vyema hawaamini kama
kitabu kile kaandika yeye.

Historia inatuambia kitabu kimeandikwa na yeye, watu waliokua karibu na yeye sio hawaamini bali imewalazimu kutokuamini ivyo kutokana na uwoga waliojazwa
 
Historia inatuambia kitabu kimeandikwa na yeye, watu waliokua karibu na yeye sio hawaamini bali imewalazimu kutokuamini ivyo kutokana na uwoga waliojazwa

Activisty,
Halikupata kuwa suala la woga.
Woga wa kuogopa kitu gani au kumuogopa nani.

Nakueleza kitu ninachokijua.
Mimi ni mwandishi na nimeandika vitabu kadhaa.

Halikadhalika nimekuwa Msaidizi Mtafiti wa Dr. Harith Ghassany wakati
anatafiti na kuandika, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Tumepita kwingi, tumesoma mengi na tumesikilizishwa mengi...
Okello tumemfahamu vyema kabisa...

Okello hakuwa na uwezo wa kuandika kitabu kile.

Badawiy Qullatein
alikuwa rafiki yangu na kanieleza mengi
kuhusu Okello.

Naamini unamjua Qullatein...

Ikutoshe tu katika vyeo vya kijeshi alijichagulia cheo cha, ''Field
Marshal.''

Wala Okello hakupatapo kujua nini maana ya ''Field Marshal'' wala
kujua kuwa cheo hicho alikuwanacho Tito wa Yugoslavia na wala
hakupatapo kujua Field Marshal Tito alikipataje cheo hicho.

The Fifth Offensive...Second World War, Partisan Army...

Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ina vichekesho vya kila aina.
Hiki cha Field Marshal Okello kimefurtu ada.

Labda nikuulize kitu.

Kabla ya kitabu kile wewe umepata kuona chochote alichoandika
Okello?

Kama kuandika kuhusu mapinduzi angeliandika Abdulrahman
Babu
siyo Okello.

Babu hakuandika hadi anaingia kaburini.
Jiulize kwa nini...

Majibu tunayo.

Okello
ni mtu mjinga wale jamaa zake wangelikwenda Nuremburg
Okello ndiye angening'izwa kwa ushahidi wake mwenyewe.

Msome Ghassany anavyoeleza ''blanketi'' alilovishwa Okello na hilo
''blanketi,'' likamwenea khasa...

Wenye shughuli yao wakicheka hadi machozi yanawatoka.
 
Mwaka 1993 nilisoma kitabu The Zanzibar Revolution cha mmoja wa viongozi wa mapinduzi hayo John Okello.
Anaeleza kuwa hawakuwa na huruma hata kwa wanyama wa wale waliowaita maadui. Ndani ya siku 3 waliokufa Watu 5000. Kuna clip kwenye YouTube type tu Zanzibar revolution utaziona na vile maiti walivyotapakaa Mitaani. Tazama pia post facebook ya Mtatiro j. Walioitwa maadui hawakuwa na silaha zozote na waliuawa tu kama wadudu. Tangu 1993 nimeyaona mapinduzi hayo kama MAUAJI tu, hivi ni sawa wananchi milioni 45 kuacha kazi na kusheherekea tukio hili lenye utata. Tujadili ukweli tuache kudanganywa.
 
khaaaa we ulitegemea mapinduzi ya kutoa mabeberu yaweje. hebu kajikumbushe ya ufaransa
 
ndugu yangu fanya kazi ulishe familia viongozi wetu hawa wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawasikii
 
Mzee kwahiyo kunasiku mtalianzisha ilikulipiza kisasi maana mpo ndani ya chungu

tutairejesha kwa wazanzibar bila ya hata bakora....hii ni nchi ya waislam na uislam unashika nguvu umma utaelewa wakati ukifika watasema sasa hapana hio hio kura itawaondoa
 
Japo habari hii ni kweli watanzania hawtaamini sababu wameshiba maji ya bendera ya uongo. Kwa wachambzi na waliosomea world history mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa mauaji tu ya KIMBARI.
 
Someni historia ya dunia na mapinduzi duniani Yale ya Zanzibar ilikuwa ni chuki baina ya makundi hakukuwa na beberu mle mmeshiba propaganda tu. Waliuawa ni raia wema sio sultani Wala tarishi wake. Raia wadogo kabisa tena wazanzibari.
 
tutairejesha kwa wazanzibar bila ya hata bakora....hii ni nchi ya waislam na uislam unashika nguvu umma utaelewa wakati ukifika watasema sasa hapana hio hio kura itawaondoa

Kwahiyo mtu asiye Muislamu anapoteza Uzanzibar wake?
 

Tatizo ni kuwa ukweli wa mapinduzi anaujua Mohamed Said na Harith watu wengine wote walikuwa wajinga na vipofu wakati mapinduzi yanatokea
 
Last edited by a moderator:
Mapinduzi ya Zanzibar walifanya askari wa Nyerere,hizi story zingine za akina Okello sijui nini ni brainwash tu
 
Mapinduzi ya Zanzibar walifanya askari wa Nyerere,hizi story zingine za akina Okello sijui nini ni brainwash tu

Simple like this unaweza kutushawishi kweli? Kwanza unamjuwa John Okelo? Pitia google kwanza ndio urudi hapa.
 
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…